Tanzania ina kiongozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ina kiongozi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shaycas, Feb 21, 2009.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Je wajua TANZANIA HAINA KIONGOZI?
  Angalia kiongozi lazima achukue hatua na wafuasi wajue nini kiongozi wao anataka na awaongoze katika kufikia malengo aliyo mema kwa ustawi wa taifa.je nani amefanya hayo.
  Tupeana mawazo,kuna sifa nyingi za kiongozi ambazo naona wanaojiita viongozi wa taifa hili hawana.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hakuna kiongozi, period
   
 3. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kuna watawala,ambao wanafanya kila wawezalo kutawala milele!!Mkulu wa kaya alisema kuwa chama chao ni kwa ajili ya kutawala,so inabidi wahakikishe wanaendelea kutawala.Ilikuwa ni katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 32 ya chama hicho!
   
 4. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kiöngozi awe wa mfano wa kuigwa kwa maana ni bora.Sio kiongozi unaiga kwa wafuasi,yanayo fanyika sasa baadhi ya wanaojiita viongozi wanaiga kwa MWANANCHI(mtu mmoja)bila kuangalia maslahi ya wengi
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Tanzania ilikuwa haina kiongozi kwa muda,kwa sababu Rais alikuwa Chairman wa AU,he was too busy saving the world.
   
 6. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kiongozi ni lazima awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha rasmi.HII NI KATIKA KUJIELEZA,kwa hilo hatumpati mtu kwani wanojiita viongo wanajua kuongea tu bila kujieleza.
  Kwenye tume ya MWAKYEMBE,jamaa aliambiwa ajieleze yeye akasema ah jamani mimi ni mbuzi wa kafara.JE TUNAONGOZWA NA MBUZI?Mwingine nae tena kaombwa ajieleze kwanini asijiuzulu kwa kutoa tamko ambalo linapingana na utawala wa sheria,du hii ndio ilikuwa kali maana JAMAA aliamua KULIA.
  Ukija kwenye kuandika sasa, maawee hakuna kitu.Nadhani mnakumbuka ambavyo alishindwa kusoma kile alichoandika mwenyewe,aliye kuwa waziri wa miundo mbinu.
  Hata kiongozi akiambiwa aandike maelezo kuhusu utendaji wake wa kazi utasikia oh Mheshimiwa wiki moja uliyonipa kuandika hayo maelezo haitoshi niongeze japo mwezi mmoja.
  Kituko zaidi ni pale kiongozi anapo kuwa safarini kikazi,ukimuuliza kitu utasikia nipo nje ya ofisi siwezi kujibu.Swali Je angekuwa likizo ingekuaje?
  VIONGOZI WETU NI LONGOLONGO,HAWANA FACTS WANAZO AMINI NDIO MAANA HAWAWEZI KUJIELEZA KIMAANDISHI NA KWA MANENO(kuongea) ZAIDI YA MAJUNGU
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini kiongozi yupo ila watendaji ndo hawapo na hii inatokana na mfumo wa kichama kuwa mtendaji lazima atoke ndani ya chama tawala!
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wengi tuna kadi za chama ila wengi si waumini wa sera za chama ni waumini wa sera zetu binafsi (kujinufaisha mimi, ndugu, jamaa na rafiki). Hili ndilo linafanya watendaji kutokuwa na TIJA. Lakini chama chetu kina misingi bora kabisa(kama ilivyoainishwa kwenye katiba na Ilani za uchaguzi) ila wengi wa sisi wanachama hatuna misingi kabisaaa(vichwani tumejaa mawazo ya kuona ya leo; ya kesho anajua mungu). Tukiangalia nje ya chama chetu na kujali utaifa zaidi ya uchama wetu, basi tunaweza pata 20% ya viongozi wa kuwa waendelezaji wa sera za chama chetu na 80% kuwa defected, rejects.

  Ila kuna watanzania wengi hawana chama au wapo vyama vingine; hawa wanaweza kuwa watendaji wazuri sana kama watapewa nafasi na kujaza hiyo 80% ya rejects wa sasa.
   
  Last edited: Feb 24, 2009
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  unaweza tofautisha kiongozi na mtendaji.?kiongozi anatoa maelezo na kusimamia jambo fulani lifanyike kama ambavyo anataka wakati mtendaji anapokea maelezo ya nini kifanyike na kwa namna gani.
  Usichanganye kiongozi na mtendaji.
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma thread vizuri. Haina maana ya kiongozi kama physical being, hapa mtoa mada anazungumzia leadership qualities. Zitafute . Zinatoafutiana na utawala .

  Tunapaswa kuongozwa na sio kutawaliwa. :confused:
   
 11. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri kuelimishana kuliko kupingana bila kueleweshana.Umefanya mzuri kumjulisha jamaa
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Bwana/Bi mdogo punguza kasi. Usidandie gari kwa mbele soma vizuri post yangu uielewe kabla ya kutaka kunipa shule ambayo mimi niliipata siku nyingiii. Katiba ya nchi yetu inawapa viongozi ambao ni wanasiasa kuteua watendaji. Hawa wanaweza kuwa kwenye siasa au kwenye taaluma. Kwa kuwa viongozi wamejaa ubinafsi katika uteuzi hawazingatii TIJA (Output) bali ni uhusiano na anaye teuliwa. Hivyo kufanya utendaji kuwa wa kiulaji zaidi ya kiufanisi na uwezo wa mtendaji kwa kazi aliyoteuliwa kwayo. Nafikiri nimekusaidia kutafuna hapo.
   
 13. f

  fmesanga Member

  #13
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna viongozi thabiti serikalini, kwa vile wengi wamepata nafasi hizo kwa njia ya rushwa. Mtoa rushwa ni kielelezo kwamba hana sifa za kumfanya apate nafasi anayotaka, hivyo pesa hutumika. Hivi karibuni imegundulika kwamba viongozi wetu wengi wakiwemo wabunge wana vyeti vya kumaliza vyuo vya kughushi: shahada kuanzia ya kwanza hadi ya uzamivu. Inatisha. Kiongozi anayegushi vyeti hana maadili, na hivyo hawezi kutenda kazi itakiwavyo. Anakuwa mbabaishaji na muovu.

  Kughushi vyeti vya shule ni kosa la jinai. Inashangaza kwamba serikali hailivalii njuga swala hilo. Oh, si rahisi kwa vile hao hao walioko serikalini ndio wenye vyeti hivyo. Tufanye je jamani kabla nchi haijazama kabisa katika nyanja zote? Jibu ni wanacnhi kuwatema viongozi wa aina hiyo kupitia njia za uchaguzi. Tuhamasishane tuinusuru nchi yetu na matapeli.
   
 14. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu fmesanga, umetoa jambo muhimu ambalo kweli lingeweza kuwa "jibu"......lakini katika nchi yetu umasikini umeenea sehemu kubwa sana...hivyo hawa hawa "so called" viongozi wanazitumia pesa za kifisadi na kuzisambaza katika maeneo mbali mbali yenye umasikini......na matokeo yake wanachaguliwa ......halafu ....tunarudi pale pale.
   
 15. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hizi ni sifa chache kati ya nyingi anazotakiwa awe nazo.
  Atumie ujuzi alionao kwa manufaa.
  Awe muadilifu kwa watu na mali.
  Awe anachukua hatua yeye mwenyewe bila kushawishiwa.
  Asihodhi madaraka.
  Ahakikishe kuwa,maagizo anayo toa yameeleweka na yanafuata.
  Awe anajua shida na matatizo ya wafuasi na kufanya kila linalo wezekana.
  TUTAENDELEA
   
Loading...