Tanzania imenufaika na Betting

Tanzania imenufaika na Betting

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,447
Reaction score
2,094
Kodi ya michezo ya kubahatisha imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 131.99 kwa mwaka 2020/21 kufikia Shilingi bilioni 260.21 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 97

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma , GBT, Daniel Ole Sumayan ambaye ameongeza kuwa kupitia ukuaji huo fursa za ajira katika sekta ya michezo ya kubahatisha zimekuwa zikiongezeka kila mwaka. Hadi kufikia mwezi Juni 2025, ajira zilifīkia zaidi ya 30,000 ikijumuisha ajira rasmi na zisizo rasmi

Kwa upande wa uwekezaji wa nje (Foreign Direct Investment) umefikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 66.7 kimeingizwa nchini kutoka kwa wawekezaji wapya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita

Soma pia: Dkt. Mwigulu: TSh. Bilioni 17.42 zakusanywa kwenye betting Tanzania

"Moja ya faida za Sekta ya Michezo ya kubahatisha ni namna ilivyoratibiwa vema na kustawi na hivyo kuchangia ipasavyo katika maendeleo nchini”, amesema

Ametaja faida ambazo zimepatikana ni pamoja na makusanyo ya kodi yanayofikia Sh.Bilioni 922.95, na kuanzishwa kwa Bahati Nasibu ya Taifa ambayo inatarajia kuongeza mapato ya Serikali. Sekta hiyo pia imechangia Sh. Bilioni 53.8 kuendeleza michezo nchini sambamba na wawekezaji kutoka nje wa Sh.Bilioni 66.7

1754989661604.png


Chanzo: EATV
 
means wakamalia walio wengi wanaliwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom