Tanzania imeiacha mbali Korea ya Kaskazini kiuchumi

Kwa kipimo gani kwamba Korea Kaskazini ni taifa lililoendelea? Kwa utafiti upi?

Kwa mujibu wa tafiti za mashirika makubwa ya kiuchumi duniani na yenye kuaminika, Korea Kaskazini ni nchi inayoendelea. Sawa na Tanzania ambayo pia ni nchi inayoendelea. Developing countries!
Wewe unaamini pia kwenye nchi 7 tajiri duniani uchina haimo?

Miaka ya nyuma tuliambiwa Japan ni nchi ya pili kwa uchumi duniani baada ya kuiangusha ujeremani.
Sasa je china imezidiwa na Japan,German,France,Italy.
 
Shida ya NK sio vikwazo ni utawala wa wendawazimu tangu kuanzishwa kwa nchi hiyo.
JamiiForums1434033461.jpeg
 
Wewe unaamini pia kwenye nchi 7 tajiri duniani uchina haimo?

Miaka ya nyuma tuliambiwa Japan ni nchi ya pili kwa uchumi duniani baada ya kuiangusha ujeremani.
Sasa je china imezidiwa na Japan,German,France,Italy.
Jikite kwenye mada, acha kupuyanga.
 
Mkuu kuna mambo mengine wala haina haja ya kuanza tafiti mpya.
Korea Kaskazini ni taifa lililoendelea utajifananishaje na sisi tunaoendelea.
Bajeti yetu haitimii mpaka nchi wahisani watupe chochote.
Korea Kaskazini bado inapewa hadi msaada wa Chakula na China.
China ni wabahili sana wa kutoa misaada kwa nchi nyingine ila nusu ya msaada wote wa China nje ya nchi huelekeza Korea Kaskazini. Bila msaada wa China Korea Kaskazini ita collapse kabisa na kuwa failed state kitu ambacho China haitaki.
 
Tanzania ni nchi ya wendawazimu, huwezi fananisha watu wenye akili wakorea na wendawazimu.
 
Mtoa mada huna akili kabisa, kwamba Tanzania ya Chief Hangaya imeipiku Korea

Yale yale ya Nigeria kuipiku Iran

Jf ina majinga na mleta mada ni mmojawapo
 
North Korea budget yote inaishia kwenye ulinzi huku sekta zingine zikibaki hoi kwa sababu Kiduku anachoangalia ni namna gani asipokonywe ugali mdomoni.

Mambo mengine ya uchumi na maendeleo sio kipaumbele chake hayo yanawahusu jirani zake akina South Korea na Japan.

Nashangaa hata Tanzania eti GDP yetu haijafika USD 100 B pamoja na tambo za kila mara za ccm na bado tunazidiwa hata na Kenya. Hiyo GDP yetu ya USD 50 B ni sawa na ya kata moja tu kule Marekani.
 
Natamani sana kujua uchumi na maisha halisi ya NK ukiachana na propaganda za magharibi.
Kama huamini endapo tu ukashuhudie. Bajeti kubwa ya kijeshi haiwezi ikaifanya uchumi wa Korea Kaskazini uwe mzuri lazima watakuwa wachovu tu kwani hakuna chochote cha maana wanachouza nje kwani januari mpaka januari wanawaza vita tu kwamba watavamiwa na Marekani. Bure kabisa.
 
Yaani ujira tu kwa Mbangaizaji kitaa wa kuweza kupata mkate wake angalau mara moja kila siku (let alone milo mitatu) na kuweza kulipia pango lake la mbavu za mbwa (let alone huduma za maji na umeme wa uhakika) zingempendeza zaidi kuliko hizi ngonjera za level ya uchumi.....
 
Chek mambo hayo jamaa tumewaacha mbali sana kiuchumi kweli uchumi wa kati kiboko

GDP yetu ni dola bilioni 50

Wakati yao North Korea ni bilioni 18 tu

Huku kenya wao ikiwa ni bilioni 70

Korea ya kusini wao wana 1.65 trilioni dollar GDP.

Wakati Japan gdp yao ni 5008 trilion dollar.

Kweli dunia haina usawa.


View attachment 1720557View attachment 1720558
Hatuna uchumi wa kuunda yale makombora mzee.

Hatyna uchumi wa mradi wa Nuclear

Wala hatuna uchumi wa kuvumbiana na USA na kuhimili vikwazo vya kimataifa.

Huu uzi umetujazia server.

Google kama google
 
Kama huamini endapo tu ukashuhudie. Bajeti kubwa ya kijeshi haiwezi ikaifanya uchumi wa Korea Kaskazini uwe mzuri lazima watakuwa wachovu tu kwani hakuna chochote cha maana wanachouza nje kwani januari mpaka januari wanawaza vita tu kwamba watavamiwa na Marekani. Bure kabisa.
We bado unaongea kwa mtazamo wa kimagharibi.
 
Back
Top Bottom