Kwa sasa Nchi haijatenga fungu la kwenda kuvamia Somalia, isipokuwa ina budget ya kutosha ya kwenda kupiga wavamizi wa Nyamongo Barrick Mine na migodi mingine kwani huko ndiko zinapopatikana fedha kwa wingi, huko baharini acha tu Wasomali waendelee na kazi yao kwani wanajitafutia riziki. Lakini pia napenda kukutoa wasiwasi Mheshimiwa Mwana JF kwamba ikiwa Serikali itaishiwa fedha za kuendeshea nchi basi itafanya utaratibu wa kwenda kuwapiga MACHINGA ili wakimbie waache mizigo yao kisha serikali itaifishe, kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imejikusanyia kiasi cha Tsh. 1.7 trilioni kama Stimulas package kwa mwaka wa fedha 2012/2012. na serikali inategemea kwenda kupiga palipona machinga wengi kama vile Arusha, Mwanza lakini pale Daressalaamu ikiwa MACHINGA watahamia Machinga complex basi kipigo kitapungua na mapato yatapungua pia. Nashukuru.