Tanzania: Idadi ya watu yavuka 58,000,000. Ni zaidi ya makisio ya awali ya NBS!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Ripoti ya UN inaonyesha idadi ya watu nchini Tanzania imefikia zaidi ya milioni 58.

Takwimu za NBS kwa mwaka 2012 zilikisia kuwa miaka mitano baadae Tanzania ingekuwa na watu takribani milioni 52 mwaka 2017.

Kinachoshtua ni kuwa ongezeko hili ni zaidi ya asilimia 12 kiwango ambacho ni kikubwa na kuacha maswali kama takwimu za NBS zinatakiwa kuendelea kutumiwa na watafiti au ‘wajisogeze’ na kujipatia takwimu wanazoona zitafaa.

Swali langu: NBS iliwapa ruksa UN kutangaza taarifa hizi? Au sheria ya Takwimu itawagusa nao?

d4602eba96680335e04f2a1f0660022b.jpg
 
Toba we!
hiyo sheria imeshazinduliwa au bado..?
isijekuwa hata ukijaza 1+1=5 unatiwa mbaroni! tuambizane maana takwimu ni takwimu tu.
 
Hongereni watanzania kwa kuzaana. Ila huku tunapoenda ni bora jitihada zikawekwa kuhakikisha idadi ya watu haiongezeki sana maana kwa population hii, hatuna uchumi stahimilivu wa kuwapatia watu wote hao mahitaji ya yao ya kila siku na hasa ukizingatia kuwa siku hizi binadamu wanaishi maisha marefu zaidi kuliko zamani.
Hili litakuja kuwa na athari kubwa sana hasa hawa watoto wakikua maana ajira itakuwa ni kizungumkuti...
 
Yawezekana mtindo wa ukusanyaji wa takwimu zetu za Sensa bado una kina Ngoswe wengi tuu. Vile vile elimu juu ya Faida za sensa haiwafikii wengi hivyo coverage halisi ya sensa haifikiwi.

Nafikiri taarifa za UN zaweza kuwa karibu na ukweli zaidi.
 
Mhmm Invisible huogopi kufungwa?! Kwani NBS nao takwimu zao ni za MAKISIO au mkono umeteleza?! Mhmm nitasubiri nione kama msemaji wa serikali hatokanusha hii.
 
Back
Top Bottom