BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 5,010
- 10,940
Ninaliandika hili kwa tahadhari kubwa sana, natamani hata niandike kwa wino mwekundu kisha niligongelee muhuri wa mahakama ili kutilia mkazo.
Nchi hii haina madaktari wala wanaojiita wataalamu wa afya. Hawapo kabisa, hakuna hata mmoja. Nitaeleza.
Mwaka 2020 kulizuka kitu kilichopewa jina la corona. Tukapigwa timbwili la maana tukaambiwa tujifungie uvunguni hakuna kutoa pua nje, ati la sivyo tutaangamia.
Kila mtu akabaki amejibanza kama kifaranga, hata wanaojiita wataalamu wa afya wote wakafyata mikia huku wamejicha nyuma ya milango.
Kuna rafiki yangu mmoja anajiita daktari bingwa, anafanya kazi muhimbili nikamfwata nikamuuliza hili swala limekaaje, akaniambia hata wao hawajui cha kufanya, wanasubiri NOTES (MADESA) kutoka Ulaya. Bila kupewa NOTES ZA KUSOMA kutoka Ulaya hawajui cha kufanya.
Nikagundua kumbe yote wanayoyafanya na kuyaweza ni yale tu waliyoyakariri kwenye vitabu na kwenye NOTES za TWISHENI. Nasikia kuna jamaa yao wa PCB anafundishaga TWISHENI YA UDAKTARI hapo sijui mchikichini!
Kwahiyo likitokea jambo ambalo halipo kwenye NOTES ZAO za kukariri shuleni, TWAFA! Tumekwisha!
Mimi nilijua daktari ni mtu mwenye utambuzi, mwenye elimu pevu ambaye anaweza kung'amua jambo lolote kwa kadiri ya linavyokuja. Kumbe wao wanasubiri kusoma NOTES kutoka Ulaya.
Na hivi juzi, walikuwa wanasubiri kupewa NOTES kutoka WHO ili waelezwe corona ni nini! Wenyewe kama wenyewe hawawezi kufanya lolote mpaka wasome NOTES za Ulaya. Wanakwambia "tunasubiri maelekezo kutoka China".
Bila Magufuli ndugu zangu tungeangamia! Hawa wanaojiita madokta ni watu wa kutafuna mshahara tu na kujitwika makoti makubwa ya danganya toto.
Cha kushangaza, chanjo zilivyoletwa tu, wakakurupuka kwa kasi kutoka mafichoni ati wanajidai kutoa elimu kwa umma!!! Ati wanaelimisha!