Tanzania has started to build its own helicopters

Mmmmh kama tumeshindwa kutengeneza Stik......hongera zao ila mm binafsi siwez kupanda! Sipandi ng'ooo
 
Mmeanza kuwa na idea mieiz miwili iliyopita na leo tayari mna protptype na mnaomba certificate ya kuruka...MmmhH hicho ni kicheko cha mwaka... kwani hao magwiji wa uengenezaji inawachukua miaka kadhaa just ku design tu na michoro hata kbla ya kutengeneza prototype..naona watu wanatucheka tulivyokuwa majuha
 
Aisee tuseme tuu R.I.P. wale watakaotangulia kuipanda
 
Tungeanza na baiskeli kwanza....maana hapo ni kama wana nunuwa kila kitu then wao wanaunganisha tu
 



Sangora wapo Mkuu. Wapo Nyasa wanaunda meli sahvi Google sangoro marine transport wamepewa mrad Wa kuunda meli pale Nyasa
 
Tungeanza na sindano za kushonea, vijiti vya meno, baiskeli, pini n.k..kwa helikopta sijui....
 
Kuna kipindi nilihisi kizazi hiki hatutakuja kushuhudia Tanzania yenye neema...ila sasa naonza kuona a bright light at the end of the
tunnel....hope in the horizon!

Mwelekeo mzuri. Jitihada hizi zifanyike pia kwenye viwanda mbalimbali vya kati haiwezekani hata viwanda vya kusindika nyama anpeww mgeni waka uwezo huo upo ndani ya mikono yetu.

Tanzania ya viwanda lazima mtanzania awe mdau namba moja akipewa fursa ya upendeleo.
Kwa minajili hii tutajenga uchumi wa wazalendo ambao watakuwa na maamuzi sahihi juu ya uchumi wao watakao tetea maslahi ya taifa lao dhidi ya changamoto ya mabadiliko ya uchumi wa dunia.
 
Ni hatua ya kupongezwa sana. Hongereni wataalam wetu, na ninawatakia mafanikio.
 
Sawa lakini iwe imara isijelipuka angani
 
Dah nimefurahi sana aisee dah tutafika kutengeneza attack and jet fighter hongera sana. Mungu nibariki tanzania
 
Tungeanza na baiskeli kwanza....maana hapo ni kama wana nunuwa kila kitu then wao wanaunganisha tu
Kuunganisha kwenyewe lazima wachakachue, badala ya super glue watatumia gundi ya kuzibia pancha
 
Acheni uzuzu tz ubavu huo hakuna eti building helicopter say assembling helicopter mnawezatengeneza rotor craft nyinyi mnachukua engine Volkswagen's kazi yenu kudizaini body kama yalivyo mabasi kama yutong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…