Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,110
- 18,327
- Thread starter
- #21
Mkuu umesema kweli kabisa.. nakubaliana na wewe 100%. Kuna watu hawajui nini maana ya milo mitatu. ila wanashiba hadi kusaza na hawanunui chakula. wana mihogo, viazi, ndizi, maziwa etc. kisha mtu anakuja eti unaishi chini ya dolla 1? Propaganda mbaya sana hiiMtoa mada yuko sahihi,tatizo kundi kubwa zaidi la Wa Tanzania hawafikiri bali hukariri. Nitatoa mifano michache kuthibitisha sisi si maskini ila akili za baadhi ya wenzetu zimejazwa ujinga huo. Tuanze na vyakula. Nenda vijijini;Pima wanakula nini ,mara ngapi kwa siku na gharama ya wanachokula. Vipe thamani vyakula hivyo kwa fedha ya kwetu na watawala wa Dunia. Thibitisha je sisi ni maskini? Usihangaike eneo lako la kupima ukaenda eneo la ukame au mafuriko tu,au ukatumia jamii ya wavivu kutuma. Pima watenda kazi wasiosubiri serikali kuwasimamia . Jamii tunayoiita maskini na inakula mlo mmoja uhalisia ni huu ufuatao. Asubuhi hula matunda embe,ndizi,papai,pera na baadhi hunywa uji au chai. Wapimaji hawamhesabu aliyekula tunda badala ya chai kuwa kapata kifungua kinywa. Kwao bila chai hujapata mlo wa asubuhi. Wapo wa Tanzania asubuhi hula dona la nguvu,mboga za majani na maziwa.Hawanywi chai,kwa kuwa kipimo kilichopo ni chai asubuhi tunawahesabu hawajapata kifungua kinywa. Najiuliza kipi kina faida kubwa kiafya? Umiliki wa mali. Ukiacha " tuliong'ang'ania mjini" ni wapi ukiondoa Kilimanjaro utamkuta Mtanzania hawezi kuipata ekari moja ya ardhi yake? Thamani ya ardhi hiyo nani kaipima? Tuwatawanye wawili wasio na kitu ila wana nguvu na akili. Mmoja apelekwe Kenya mmoja aletwe Tanzania tuwape miezi 6 walete taarifa ya kuipata ardhi. Elimu. Tumetelemka mno. Tuliwahi kufikia 95% ya jiwa Tanzania kujua kusoma na kuandika. Tukadeka tumeharibu hadi tunaudhi chanzo in kusubiri misaada. Sisi si maskini tubadili mtazamo wetu.