Tanzania haipo kati ya nchi masikini duniani

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
TANZANIA HAIPO KATI YA NCHI MASKINI DUNIANI

Kila ninapo soma habari za tanzania nakutana na maelezo kwamba Tanzania ni moja ya nchi maskini sana dunia, miaka nenda rudi bado wanatuita maskini.

Swali ninalo jiuliza kwanini watupangie au kwanini watuite maskini, hii inanikumbusha watu ambao nilikutana nao shuleni ili kuniweka chini yao basi wataniambia sina akili kabisa na mjinga kabisa.

Ukisoma wikipedia kuhusu Tanzania utakutana na sentensi hii (Tanzania is one of the poorest countries in the world)

Baada ya kufanya utafiti nikagundua kutoka ktk kundi hili au kutoka ktk dimbwi la kuitwa maskini ni jukumu letu watanzania, lazima tufike mahali tukatae kwa vitendio na kujua wapi tunatakiwa kuwa.

Nimejaribu kutafuta baadhi ya source nikaona tanzania haipo kati ya nchi kumi za mwisho maskini. Mfano unaweza soma hapa. Top 10 Most Poorest Countries In The World 2015

Lakini pamoja na kuona baadhi ya source zinaitoa Tanzania ktk listi ya nchi maskini nimepata maswali yakujiuliza kama ifutavyo

1. Nani atapigania haki ya tanzania kufutwa kwenye listi ya nchi maskini kama walivyo fanya kenya

2. Kwa nini na sisi wenyewe watanzania tusikatae kuitwa maskini, fikra ambayo inatufanya tufanye mambo kimaskini, wote mmemsikia waziri wa fedha siku chache zilizo pita akisema eti haiwezekani kujenga reli kwa fedha zetu za ndani, hayo ni mawazo ya kimaskini kabisa.

3. Je serikali ina mpango gani wa kujipima yenyewe badala ya kutegemea mashirika ya nje kutupimia vitu kama GDP , etc.

hii vita ya kuukata umaskini inabidi ifanywe kwa umoja na umahili mkubwa , kwa kutangaza Tanzania kama nchi ambayo si maskini kwa kutumia vyombo vyote vya habari kama Internet, forums etc, Kila tunapo taja tanzania lazima tueleze kuwa tanzania si nchi maskini, nchi yenye utajiri mwingi, yenye amani etc

Kwanini turuhusu watu wengine kututangaza kwa ubaya?

Tanzania si nchi maskini wala moja ya nchi maskini.

Nawasilisha
 
Nahisi watanzania tunaoishi leo tunapambana sana japo fursa ni chache

Nawaza tu kama kizazi chetu hiki kingeishi miaka ya 1930 kurudi nyuma nahisi Tanzania ya leo isingekua hii ukiachia ufisadi na ujinga umasikin mwingi tumeupokea kwa wazee wetu!
 
TANZANIA HAIPO KATI YA NCHI MASKINI DUNIANI

Kila ninapo soma habari za tanzania nakutana na maelezo kwamba Tanzania ni moja ya nchi maskini sana dunia, miaka nenda rudi bado wanatuita maskini.

Swali ninalo jiuliza kwanini watupangie au kwanini watuite maskini, hii inanikumbusha watu ambao nilikutana nao shuleni ili kuniweka chini yao basi wataniambia sina akili kabisa na mjinga kabisa.

Ukisoma wikipedia kuhusu Tanzania utakutana na sentensi hii (Tanzania is one of the poorest countries in the world)

Baada ya kufanya utafiti nikagundua kutoka ktk kundi hili au kutoka ktk dimbwi la kuitwa maskini ni jukumu letu watanzania, lazima tufike mahali tukatae kwa vitendio na kujua wapi tunatakiwa kuwa.

Nimejaribu kutafuta baadhi ya source nikaona tanzania haipo kati ya nchi kumi za mwisho maskini. Mfano unaweza soma hapa. Top 10 Most Poorest Countries In The World 2015

Lakini pamoja na kuona baadhi ya source zinaitoa Tanzania ktk listi ya nchi maskini nimepata maswali yakujiuliza kama ifutavyo

1. Nani atapigania haki ya tanzania kufutwa kwenye listi ya nchi maskini kama walivyo fanya kenya

2. Kwa nini na sisi wenyewe watanzania tusikatae kuitwa maskini, fikra ambayo inatufanya tufanye mambo kimaskini, wote mmemsikia waziri wa fedha siku chache zilizo pita akisema eti haiwezekani kujenga reli kwa fedha zetu za ndani, hayo ni mawazo ya kimaskini kabisa.

3. Je serikali ina mpango gani wa kujipima yenyewe badala ya kutegemea mashirika ya nje kutupimia vitu kama GDP , etc.

hii vita ya kuukata umaskini inabidi ifanywe kwa umoja na umahili mkubwa , kwa kutangaza Tanzania kama nchi ambayo si maskini kwa kutumia vyombo vyote vya habari kama Internet, forums etc, Kila tunapo taja tanzania lazima tueleze kuwa tanzania si nchi maskini, nchi yenye utajiri mwingi, yenye amani etc

Kwanini turuhusu watu wengine kututangaza kwa ubaya?

Tanzania si nchi maskini wala moja ya nchi maskini.

Nawasilisha

Mkuu unakimbia kivuli chako mwenyewe! au kwa kuwa wewe unaishi masaki?
 
Mkuu .. tunaaminishwa tuu kwamba sisi ji maskimi ili tuwe na fikra za kimaskini. lakini sisi sio maskini
Ni kweli tunapaswa kubadili mind set zetu kwamba sisi siyo masikini. Hata hiyo reli ya kati ya standard gauge tukiamua kila mtanzania achangie angalau tu. Shs. 1000/ trion 45 zitapatikana ambazo zinatosha kabisa kujenga reli hiyo. Uwezo huo tunao na wapo wengi tu watatoa hata laki moja au zaidi. Wasiwasi wetu ni kuwa michango hii inaweza tafunwa na wachache, mafisadi.
 
Kuna mtu alikua anaruka kila siku kwenda kulia njaa ughaibuni, Sasa wewe ulitaka wazungu waamini vipi? Sio kwamba wao wanaitangaza Tz masikini bali ni viongozi wa ccm kwa ajili ya mitumbo yao.
 
Ukweli ni kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini Dunia, kusema kuwa hatupo katika nchi 10 masikini zaidi duniani siyo sababu ya sisi kutokuwa masikini,

Kwa kuangalia tuu kwa kawaida sisi tupo nyuma sana kwa maendeleo ya nyaja zote, kiuchumi, kijamii na kisiasa, ebu jaribu kuangalia Huduma za kijamii zinazotolewa Tanzania ni za hali ya chini sana, ukienda mashuleni hapafai, hospitalini huko ndipo usiseme mashrika na taasisi za serikali zimechoka kila idara.

Nikiwa nasafiri kwa Basi kutoka dar to mwanza nikifka mikoa ya kati singda tabora na baadhi ya sehemu za mwanza na shinyanga nikiona watu walivyochoka na maisha nawaza sana
 
Lipa deni la taifa, sijui hata kama unajua tunadaiwa kias gani, Ondoa njaa za kijinga kijinga kama dodoma wakati kuna maghala ya taifa, bajeti zetu zisitegemee misaada, ongeza pato la mtanzania kwan most tunaishi under 1$ per day. Then ukimaliza nenda kamuulize Mzee Mwinyi, Mkapa, na Kikwete kwanini bado tuko maskini?
 
Endelea kuota ndoto tu kuwa Tanzania sio nchi masikini sana duniani...ukija aamka ndo utafahamu ni kwa nini ni moja ya nchi masikini sana...NB. Tanzania sio Daslama pekee.
 
Kuna mtu alikua anaruka kila siku kwenda kulia njaa ughaibuni, Sasa wewe ulitaka wazungu waamini vipi? Sio kwamba wao wanaitangaza Tz masikini bali ni viongozi wa ccm kwa ajili ya mitumbo yao.
Hilo ndilo tatizo.. ameacha dhahabu huko shinyanga anakimbiza bakuli kuchangisha apate madawati wakati mbao zimejaa nchi nzima. Wazungu wameturoga
 
Lipa deni la taifa, sijui hata kama unajua tunadaiwa kias gani, Ondoa njaa za kijinga kijinga kama dodoma wakati kuna maghala ya taifa, bajeti zetu zisitegemee misaada, ongeza pato la mtanzania kwan most tunaishi under 1$ per day. Then ukimaliza nenda kamuulize Mzee Mwinyi, Mkapa, na Kikwete kwanini bado tuko maskini?
Tatizo la viongozi wetu wao ndio wa kwanza kuamini kiwa nchi zao ni maskini.. wanatumia muda mwingi kutbeza bakuli badala ya kufikiri jinsi ya kuondoa majanga kama njaa.. sehemu ambazo zinakumbwa na njaa kuna matatizo mawili.. moja watu wavivu na pili mvua sio za kuaminika.. mfano dodoma kwanini serikali isifanye kampeni kichaa ya kupanda miti mkoa wote na baada ya miaka mitano tuu tatizo limeisha.. uvivu ni kupeleka jwtz wawafundishe kazi.
 
Ukweli ni kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini Dunia, kusema kuwa hatupo katika nchi 10 masikini zaidi duniani siyo sababu ya sisi kutokuwa masikini,

Kwa kuangalia tuu kwa kawaida sisi tupo nyuma sana kwa maendeleo ya nyaja zote, kiuchumi, kijamii na kisiasa, ebu jaribu kuangalia Huduma za kijamii zinazotolewa Tanzania ni za hali ya chini sana, ukienda mashuleni hapafai, hospitalini huko ndipo usiseme mashrika na taasisi za serikali zimechoka kila idara.

Nikiwa nasafiri kwa Basi kutoka dar to mwanza nikifka mikoa ya kati singda tabora na baadhi ya sehemu za mwanza na shinyanga nikiona watu walivyochoka na maisha nawaza sana
Tanzania sio nchi maskini.. tatizo tunashindwa kujipambanua. umesha ona mtu ana mbuzi elfu 1 lakini hana hata banda la kuishi akajisitiri.
Pia baada ya kuaminishwa kuwa maskini basi na ubungo wetu umeganda hapo.
Ukiangalia unakuta kweli nhi maskini lakini haya ni matokeo ya ukoloni. tumeaminishwa miaka nenda rudi. majanga yetu tuu ndio utayakuta kqemye vyombo vyao vya habari.. mambo mazuri hawaya tangazi kabisa kama njia ya kutufanya tubakie hapo.
Nasikitika sana kuona hadi vyoo vya shule tunaomba msaada?
Viongozi waamke na kuanza mikakati mikubwa sio hii ya kimaskini..
 
Ila ni nchi omba omba nikiwa na maana inategemea misaada katika bajeti yake
Omba omba ni tabia na sio kwamba wewe ni maskini. Na hilo ndilo wazungu wamebana akili zetu. ukisha anza tabia ya ombaomba huachi. ni aibu kuomba wakati unamilima imejaa dhahabu
 
Mtoa mada yuko sahihi,tatizo kundi kubwa zaidi la Wa Tanzania hawafikiri bali hukariri. Nitatoa mifano michache kuthibitisha sisi si maskini ila akili za baadhi ya wenzetu zimejazwa ujinga huo. Tuanze na vyakula. Nenda vijijini;Pima wanakula nini ,mara ngapi kwa siku na gharama ya wanachokula. Vipe thamani vyakula hivyo kwa fedha ya kwetu na watawala wa Dunia. Thibitisha je sisi ni maskini? Usihangaike eneo lako la kupima ukaenda eneo la ukame au mafuriko tu,au ukatumia jamii ya wavivu kutuma. Pima watenda kazi wasiosubiri serikali kuwasimamia . Jamii tunayoiita maskini na inakula mlo mmoja uhalisia ni huu ufuatao. Asubuhi hula matunda embe,ndizi,papai,pera na baadhi hunywa uji au chai. Wapimaji hawamhesabu aliyekula tunda badala ya chai kuwa kapata kifungua kinywa. Kwao bila chai hujapata mlo wa asubuhi. Wapo wa Tanzania asubuhi hula dona la nguvu,mboga za majani na maziwa.Hawanywi chai,kwa kuwa kipimo kilichopo ni chai asubuhi tunawahesabu hawajapata kifungua kinywa. Najiuliza kipi kina faida kubwa kiafya? Umiliki wa mali. Ukiacha " tuliong'ang'ania mjini" ni wapi ukiondoa Kilimanjaro utamkuta Mtanzania hawezi kuipata ekari moja ya ardhi yake? Thamani ya ardhi hiyo nani kaipima? Tuwatawanye wawili wasio na kitu ila wana nguvu na akili. Mmoja apelekwe Kenya mmoja aletwe Tanzania tuwape miezi 6 walete taarifa ya kuipata ardhi. Elimu. Tumetelemka mno. Tuliwahi kufikia 95% ya jiwa Tanzania kujua kusoma na kuandika. Tukadeka tumeharibu hadi tunaudhi chanzo in kusubiri misaada. Sisi si maskini tubadili mtazamo wetu.
 
Mpaka mwishoni mwaka miaka ya 90 China ilikuwa ikihesabiwa kama nchi maskini na iliwekwa ktk kundi la nchi zinazostahili kusaidiwa,mfadhili mkuu wa China alikuwa Germany. Leo hii China ni nchi tajiri sana duniani.Siri no nini?they didn't cry out complaining why they're called the poor country? They worked hard instead,with the goals they set and ambitions for higher success they had they finally got there where they are today,the economic giant. Let's keep crying and complaining while doing nothing to improve our people's lives and country's economic wellbeing in general.
Mkuu unakimbia kivuli chako mwenyewe! au kwa kuwa wewe unaishi masaki?
 
TANZANIA HAIPO KATI YA NCHI MASKINI DUNIANI

Kila ninapo soma habari za tanzania nakutana na maelezo kwamba Tanzania ni moja ya nchi maskini sana dunia, miaka nenda rudi bado wanatuita maskini.

Swali ninalo jiuliza kwanini watupangie au kwanini watuite maskini, hii inanikumbusha watu ambao nilikutana nao shuleni ili kuniweka chini yao basi wataniambia sina akili kabisa na mjinga kabisa.

Ukisoma wikipedia kuhusu Tanzania utakutana na sentensi hii (Tanzania is one of the poorest countries in the world)

Baada ya kufanya utafiti nikagundua kutoka ktk kundi hili au kutoka ktk dimbwi la kuitwa maskini ni jukumu letu watanzania, lazima tufike mahali tukatae kwa vitendio na kujua wapi tunatakiwa kuwa.

Nimejaribu kutafuta baadhi ya source nikaona tanzania haipo kati ya nchi kumi za mwisho maskini. Mfano unaweza soma hapa. Top 10 Most Poorest Countries In The World 2015

Lakini pamoja na kuona baadhi ya source zinaitoa Tanzania ktk listi ya nchi maskini nimepata maswali yakujiuliza kama ifutavyo

1. Nani atapigania haki ya tanzania kufutwa kwenye listi ya nchi maskini kama walivyo fanya kenya

2. Kwa nini na sisi wenyewe watanzania tusikatae kuitwa maskini, fikra ambayo inatufanya tufanye mambo kimaskini, wote mmemsikia waziri wa fedha siku chache zilizo pita akisema eti haiwezekani kujenga reli kwa fedha zetu za ndani, hayo ni mawazo ya kimaskini kabisa.

3. Je serikali ina mpango gani wa kujipima yenyewe badala ya kutegemea mashirika ya nje kutupimia vitu kama GDP , etc.

hii vita ya kuukata umaskini inabidi ifanywe kwa umoja na umahili mkubwa , kwa kutangaza Tanzania kama nchi ambayo si maskini kwa kutumia vyombo vyote vya habari kama Internet, forums etc, Kila tunapo taja tanzania lazima tueleze kuwa tanzania si nchi maskini, nchi yenye utajiri mwingi, yenye amani etc

Kwanini turuhusu watu wengine kututangaza kwa ubaya?

Tanzania si nchi maskini wala moja ya nchi maskini.

Nawasilisha
Nina kubariana na Wewe kwa 100% nimejaribu kutembelea nchi nyingi lakini nikagudua Tanzania ni nchi tajiri sana mpaka sasa sijaona umasikini Hata kidogo wa mali, ila nimegundua umadikini wetu nj kubweteka kutopenda kufanyakazi, na watu kutowajibika ipasavyo. Tanzania ni nchi ya neema iliyojaa maziwa na asali,
 
Ukweli ni kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini Dunia, kusema kuwa hatupo katika nchi 10 masikini zaidi duniani siyo sababu ya sisi kutokuwa masikini,

Kwa kuangalia tuu kwa kawaida sisi tupo nyuma sana kwa maendeleo ya nyaja zote, kiuchumi, kijamii na kisiasa, ebu jaribu kuangalia Huduma za kijamii zinazotolewa Tanzania ni za hali ya chini sana, ukienda mashuleni hapafai, hospitalini huko ndipo usiseme mashrika na taasisi za serikali zimechoka kila idara.

Nikiwa nasafiri kwa Basi kutoka dar to mwanza nikifka mikoa ya kati singda tabora na baadhi ya sehemu za mwanza na shinyanga nikiona watu walivyochoka na maisha nawaza sana
Mkuu jaribu kujitafakari mwenyewe pili watu mnapenda kusikiliza propaganda. Tukiangaria huduma za kijamii wewe nini mchango wako kwa taifa lako? Na je unawajibika ipasavyo?
 
Back
Top Bottom