Tanzania haijui inachofanya EAC

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
'Tanzania haijui inachofanya EAC'

Boniface Meena

WABUNGE wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, wamesema Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kutokuwa na mipango madhubuti ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo.

Wabunge hao walisema hayo jana, walipokuwa wakijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayooingwozwa na Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Mmoja wa wabunge hao, Janet Mmari, aliiambia Kamati ya Lowassa kuwa Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kushindwa kujipanga kama inavyofanywa na nchi nyingine.

Alisema nyingine za jumuiya hiyo zimejipanga vizuri na zimekuwa zikiwasaidia wabunge wake."Serikali ya Kenya imejipanga kuwaeleza wananchi wao na kutumia vizuri fursa za jumuiya. Sisi bado tupo nyuma na hata bajeti yetu ni 'kiduchu',"alisema Mmari.

Aliiomba kamati hiyo iwasaidie ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kuwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo, zimejipanga katika kuwasaidia wafanyabiashara wao, kutumia vizuri soko la pamoja.

Sebtuu Nassoro, alisema tatizo kubwa ni kwamba Tanzania kushindwa kujipanga ndani ya jumuiya hiyo na hivyo kusababisha isijuie inachokifanya."Hatujajipanga ndiyo tatizo letu, ndani ya jumuiya,"alisema Nassoro.Dk Amani Kabourou, alisema kuwa Tanzania hakuna elimu yoyote inayotolewa kuhusu nchi nyingine zinavyofanya kufanikisha mambo yao, ndani ya jumiya.

"Huwa hatuna mkutano na waziri mkuu wala rais, kama ilivyo kwa wenzetu wa Kenya ambao huwa wanakaa nao na kupanga mikakati kwa kuwa wanajua wanachokitaka,"alisema Dk Kabourou.Kwa upande wape, Dk Didas Masaburi, alisema wabunge wa Tanzania hawajui wanaripoti wapi baada ya kutoka katika Bunge la Jumuiya.

"Ni wakati muafaka sasa kujua sisi tunaripoti wapi, hatuna usafiri wala mwandishi hata hii taarifa ni mwenyekiti kaandaa mwenyewe,"alisema Dk Masaburi.

Alisema hajawahi kuona Bunge linaripoti kwa wizara kama inavyofanyika hapa nchini kwa wao kuripoti katika Wizara ya Afrika Mashariki.Dk Fortunatus Masha, alisema kuwa Tanzania iko nyuma sana kwa kuwa wananchi hawana elimu ya kutosha kujua nini wanapaswa kukifanya.

"Elimu kwa wananchi tuko nyuma, wananchi lazima waelimishwe kuhusu masoko ya nchi hizi,"alisema Dk Masha.
Wakati akitoa taarifa yake kwa kamati hiyo, Mwenyekiti wa wabunge wa jumuiya hiyo, Kate Kamba, alisema umuhimu wa Tanzania katika jumuiya hiyo ni kuwa na bandari kubwa.
 
Thursday, 24 March 2011 21:25

Source
Mwananchi

Inasikitisha sana kuona tuko kwenye jumuia ambayo hatujui faida yake na hata hao wanaotuwakilisha hawajui wako kwa faoda gani? Hii ni Aibu kwa Taifa ikiwa umekaa katika Bunge la EA hujui unawakilisha nini. Sasa wakiwa hao wanaotuwakilisha hawajui wapo kwenye Bunge kwa niaba ya nani, je sisi wananchi tusemeje? Inasikitisha sana, bora tujitoe kwenye huo muungano kama hatujui au hawajui wanamuakilisha nani. Serikali ya vilaza ina matatizo mengi mno, nchi ipo kwenye msiba, Natamani kulia jinsi ninavyoiona nchi yangu inachezewa na watu wasiojua kuongoza na wala hawajui wapo katika serikali kwa ajili ya nini.:angry:
 
Malengo ya Tanzania kwenye jumuiya ya Africa Mashariki ni yale ya mwaka 1967-77, kushirikiana kwa ajili ya ukombonzi wa Afrika na siyo malengo ya kufaidika kiuchumi. Ndio maana hata viongozi hawaoni faida za kiuchumi zitakazotokana na EAC ni kama tumaburuzwa tu. Wananchi ndo giza kabisaaaaa.

Kipindi cha nyuma nilisoma thread moja ya Waziri Sitta iliyohusu kuwa na mfumo wa elimu unofanana. Bado hata hapa tunachangamotonying mno kuweza kufanikisha lengo hili kwa ufanisi. Kwanza walimu wetu, vifaa na miundo mbinu. Hili wazo ni zuri lakini kwetu tunahitaji kujipanga vizuri sana kwani wezetu mitaala yao kiasi fulani ipo katika ukaribu na ya kimataifa. Inawezekana ikawa kucopy na kupaste na huku kwetu ni kuestablish upya kabisa. Kwa hiyo, tunahitaji kujipanga zaidi kuliko nchi zingine zote za Afrika Mashariki la sivyo tutakuja kumezwa katika maeneo yote.
 
Dawa ni kujitoa. Ili tumalizane na mafisadi kwanza. baada ya hilo nadhani tunaweza kuwa makini na jumuiya. kwa sasa wala hatuna habari nayo.....
 
Ningeshanga kama wangekuwa wanajua wanafanya nini. Humu nchini tu hatujui tunafanya nini sembuse huko kwenye wajanja!
 
Matatizo ni yale yale tuu, sifa za kijinga thats all, yaani viongozi wetu hawana vision wala goals, ni watu wa kufuata mkumbo, EA ni bomu ambalo litakuja kulipuka soon, na itakuwa vigumu kujitoa kuliko kuvunja muungano feki wa tanganyika na zanzibar.
Kama tumeshindwa kuhudumia watu ndani ya tanzania ya sasa tutawezaje kuumudu muungano wa mataifa 5.
Tunasema ardhi ni kwaajili ya watz tuu, huku tunawapa wageni lease ya miaka 99. F@#$%%%%
 
Wewe unategemea nini wakati hata siku ile ya kugombea ubunge wa SADC tulishuhudia maduduz? Mnakumbuka wagombea walivyokuwa wakichemka, mtu anagombea ubunge wa SADC hajui kirefu cha SADC, hajui ilizaliwa lini, hajui malengo yake! Can u imagine? Basi na kwa EAC ni yaleyale 2.
 
Masikitiko makubwa sana haya. Ninachojua mimi ni kwamba Wakenya ni kama mfuga kuku anayemvizia kuku (Tanzania) aingie bandani apate kumkamata kwa kitoweo cha siku hiyo. Tunaburuzwa tu.
Tuombe muda tujipange,hatuna cha kupoteza tukichelewa.
 
Matatizo ni yale yale tuu, sifa za kijinga thats all, yaani viongozi wetu hawana vision wala goals, ni watu wa kufuata mkumbo, EA ni bomu ambalo litakuja kulipuka soon, na itakuwa vigumu kujitoa kuliko kuvunja muungano feki wa tanganyika na zanzibar.
Kama tumeshindwa kuhudumia watu ndani ya tanzania ya sasa tutawezaje kuumudu muungano wa mataifa 5.
Tunasema ardhi ni kwaajili ya watz tuu, huku tunawapa wageni lease ya miaka 99. F@#$%%%%

Bangussilo tuliza munkari kama Presida mwenyewe hajui kwanini nchi ni maskini sasa 'wafuasi' kujua kwanini tupo EAC si ni muujiza.Hata hivyo wamejitahidi kuleta HQ hapa ili ikakamilika tu tuvunje ndo ya kulazimishana walau tu offset hasara tuliyopata 77!:A S clock:.
 
Dawa siyo kujitoa kwenye jumuiya. Kujitoa siyo suluhu. Suluhu ni kuweka bidii katika kuweka mikakati madhubuti..hatujachelewa bado. Mawazo ya kukimbia tutaonekana waoga na watu wasio na vipaumbele.
 
Tuondoe chama fisadi ili tujipange vizuri zaidi, wenzetu wanafikiria maendeleo kama nchi sisi tuna watu wanao fikiria zaidi kujinufaisha wao Binafsi.

Peoples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Matatizo ni yale yale tuu, sifa za kijinga thats all, yaani viongozi wetu hawana vision wala goals, ni watu wa kufuata mkumbo, EA ni bomu ambalo litakuja kulipuka soon, na itakuwa vigumu kujitoa kuliko kuvunja muungano feki wa tanganyika na zanzibar.
Kama tumeshindwa kuhudumia watu ndani ya tanzania ya sasa tutawezaje kuumudu muungano wa mataifa 5.
Tunasema ardhi ni kwaajili ya watz tuu, huku tunawapa wageni lease ya miaka 99. F@#$%%%%
Pamoja kamanda..
 
Nimekuwa nikisizitiza sana,tuwe makini na viongozi wetu wanaotuwakilisha nje,most of them are unpatriotic,dumb na hawajui ni nini hasa maslahi ya Taifa letu.It is very dangerous,mazingira hata ya mtu kama Masha kuteuliwa au kuchaguliwa tu ilikuwa ni kulipa fadhila na kuiadhibu CHADEMA iliyokuwa na the best candidate by that time prof.Baregu.

Like the saying goes,people perish for lack of knowledge,Tanzania is perishing,not cattle will appreciate our presence because we are losing despite all our endowments.

Our people says-that only a foolish man will a prefer sulking a hard knot to bubbly bosoms,we have all,yet we are scavenging.
 
Dawa siyo kujitoa kwenye jumuiya. Kujitoa siyo suluhu. Suluhu ni kuweka bidii katika kuweka mikakati madhubuti..hatujachelewa bado. Mawazo ya kukimbia tutaonekana waoga na watu wasio na vipaumbele.
Hee mkuu! kwa hiyo unaona muhimu kwetu ni tusionekane waoga??? Ukweli ni kuwa hatuna VIPAUMBELE, anayebisha aviweke hapa.. Mi siku zote huwa najiuliza kwa nini BWM alikomalia huo uchuro wa kuungana, labda wakubwa walimlazimisha. Kama nakumbuka vizuri watanzania wote wa mipakani waliukataa muungano huo. Ingefaa zaidi kama nchi hizi zingeboresha mahusiao badala ya kukimbilia huo uchuro wa kuungana. Sasa tusubiri kuungana na Malawi na Zambia! Hee kuna na Mozambique kule kusini!! Hata wao si ni majirani zetu wazuri...???
 
Dawa siyo kujitoa kwenye jumuiya. Kujitoa siyo suluhu. Suluhu ni kuweka bidii katika kuweka mikakati madhubuti..hatujachelewa bado. Mawazo ya kukimbia tutaonekana waoga na watu wasio na vipaumbele.

Napenda kutoa maoni yangu katika hili la EAC...Mimi sipingi Tanzania kuwepo huko but......Kwahakika viongozi wetu wanatupotosha,hawaweki mazingira mazuri ya sisi kushiriki vyema katika hili shirikisho,angalieni elimu yetu,viongozi wetu ni wahuni tu halafu wanatudanganya tusilalamike tujipange kupambana...Utambana wakati maandalizi wa mapambano ni duni? Hapo tunadanganyana tu....
 
‘Tanzania haijui inachofanya EAC’

By admin– March 25, 2011Posted in: Mikoa Mbalimbali

Na Boniface Meena
WABUNGE wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, wamesema Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kutokuwa na mipango madhubuti ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo.
Wabunge hao walisema hayo jana, walipokuwa wakijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayooingwozwa na Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
Mmoja wa wabunge hao, Janet Mmari, aliiambia Kamati ya Lowassa kuwa Tanzania haijui inafanya nini katika jumuiya hiyo na kwamba hiyo inatokana na kushindwa kujipanga kama inavyofanywa na nchi nyingine.
Alisema nyingine za jumuiya hiyo zimejipanga vizuri na zimekuwa zikiwasaidia wabunge wake.”Serikali ya Kenya imejipanga kuwaeleza wananchi wao na kutumia vizuri fursa za jumuiya. Sisi bado tupo nyuma na hata bajeti yetu ni ‘kiduchu’,”alisema Mmari.
Aliiomba kamati hiyo iwasaidie ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kuwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo, zimejipanga katika kuwasaidia wafanyabiashara wao, kutumia vizuri soko la pamoja.
Sebtuu Nassoro, alisema tatizo kubwa ni kwamba Tanzania kushindwa kujipanga ndani ya jumuiya hiyo na hivyo kusababisha isijuie inachokifanya.”Hatujajipanga ndiyo tatizo letu, ndani ya jumuiya,”alisema Nassoro.Dk Amani Kabourou, alisema kuwa Tanzania hakuna elimu yoyote inayotolewa kuhusu nchi nyingine zinavyofanya kufanikisha mambo yao, ndani ya jumiya.
“Huwa hatuna mkutano na waziri mkuu wala rais, kama ilivyo kwa wenzetu wa Kenya ambao huwa wanakaa nao na kupanga mikakati kwa kuwa wanajua wanachokitaka,”alisema Dk Kabourou.Kwa upande wape, Dk Didas Masaburi, alisema wabunge wa Tanzania hawajui wanaripoti wapi baada ya kutoka katika Bunge la Jumuiya.
“Ni wakati muafaka sasa kujua sisi tunaripoti wapi, hatuna usafiri wala mwandishi hata hii taarifa ni mwenyekiti kaandaa mwenyewe,”alisema Dk Masaburi.
Alisema hajawahi kuona Bunge linaripoti kwa wizara kama inavyofanyika hapa nchini kwa wao kuripoti katika Wizara ya Afrika Mashariki.Dk Fortunatus Masha, alisema kuwa Tanzania iko nyuma sana kwa kuwa wananchi hawana elimu ya kutosha kujua nini wanapaswa kukifanya.
“Elimu kwa wananchi tuko nyuma, wananchi lazima waelimishwe kuhusu masoko ya nchi hizi,”alisema Dk Masha.
Wakati akitoa taarifa yake kwa kamati hiyo, Mwenyekiti wa wabunge wa jumuiya hiyo, Kate Kamba, alisema umuhimu wa Tanzania katika jumuiya hiyo ni kuwa na bandari kubwa.
 
Kama muungano mzuri basi huo wa EAC tutaona,,teh teh teh,,na sisi wazanzibari tunahisi kama munavyohisi nyie wabunge,,wazanzbari hatuoni haja ya kuwa na muungano wa jamuhuri ya tanganyika na zanzibar,,hauna maslahi kwa pande zote mbilii,,,,haiwezi kani mmoja avunje utaifa wake na kuvaa koti laa muungano,kwa hiyo upande mmoja unaumizwa na muunganoo,,,

Pia muungano hakukuwa na katiba hapo awali kulikuwa tu na makubaliano,lakini kwa ujanja mukaweka yale mambo ndani ya katiba ya tanganyika,na kuita tanzania,huu usanii tutauvunjia mbali muunganoo,,,kama mzuri upo wa EAC jiungeniii
 
Hii habari imenisikitisha sana, as brief as it is! Tunajipeleka wenyewe kwenye mdomo wa chatu kama mbwa! Kuyafanyia kazi haya itachukua miaka mingine mitano!
 
Inasikitisha sana kwa huyu mbunge wa Afrika Mashariki Didas Masaburi kulalamika kuwa hawajui waende kuripoti kwa nani baada ya vikao vyao vya bunge!! Ikumbukwe kwamba wao kama wabunge walichaguliwa na wabunge wa bunge la Tanzania kwenda kuiwakilisha nchi yetu huko; hivyo basi ni dhahili kuwa kwa kutumia busara kidogo tu wao wanatakiwa kwenda kutoa taarifa zao kwa BUNGE la Tanzania[ specifically kamati ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa ya bunge la Tanzania]. Hii inaonesha wazi kuwa uwezo wa hawa wabunge wa ccm waliochaguliwa kutuwakilisha huko ni duni.
 
Back
Top Bottom