Dua ya kuiombea nchi yetu na kuliombea Bunge - husomwa hivi:
Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sana dua ya kuliombea Bunge inaposomwa na Spika au Naibu wake. Siku zote nimekuwa na mashaka kama kweli kinachoombwa ndicho hasa kinachohitajika na Wabunge wetu. Pamoja na upungufu uliomo kwenye dua hii nadhani hili la kuomba kuongezewa hekima na busara kwa wabunge haliombwi ipasavyo.
Nijuavyo ni kwamba mtu huongezewa kitu ambacho anacho tayari ila anahitaji nyongeza. Sidhani kama baadhi ya wabunge wetu wana hekima na busara kiasi cha kuhitaji nyongeza. Matokeo yake aliye na hekima huongezewa (kama inavyoombwa) na asiye nayo hapewi (maana hakuna cha kuongeza). Kwa maana hiyo wale wabunge wachache ambao huongezewa hekima na busara huwa wanapishana kwa mbali sana na wale ambao hawana, na hii huleta mgongano na mabishano makubwa yasiyo na tija.
Nimelazimika kusema haya kutokana na hoja ya hivi karibuni ya wabunge kutaka kuongezewa posho. Hivi kweli wabunge wetu, hayo ndio maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu?
Waheshimiwa wabunge, ombeni mjaliwe hekima na busara kama vile anavyoombewa Rais wetu. Ili yule asiye navyo apewe angalau kidogo.
Wakatabahu,
Maamuma.
(Msisitizo ni wangu)"Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia, Umeweka katika Dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki yako itendeke.
Twakuomba, uibariki nchi yetu idumishe uhuru, umoja, haki na amani, Umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora.
Utuongezee hekima na busara, sisi Wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa kujadili kwa dhati, mambo yatakayoletwa mbele yetu leo, ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu. Amina."