Tanzania Daima yasikitisha!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Daima yasikitisha!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by masopakyindi, Apr 5, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,900
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Kwa gazeti lililojipatia sifa hapa nchini Tanzania Daima inaelekea halina sifa za watu makini hasa kwenye uhariri na uchambuzi wa habari.
  Mimi ni msomaji mzuri sana wa habari karibu zote na hata maoni ya wahariri na nina tabia ya kuwapigia simu waandishi au wahariri wa karibu vyombo vyote ninapoona msimamo au habari haina ukweli au inakinzana na uchambuzi wa habari yenyewe.

  Leo tar 5 April katika maoni ya Tz Daima kuna Tahriri inayosema "Serikali iwafukuze wamachinga kwa kuwapa maeneo mbadala".

  Nikampigia simu mhariri wa habari kwa simu iliyoainishwa gazetini mwao,(jina,simu na namba siitaji).
  Nikampa maoni yangu kuwa
  • kimsingi biashara ya machinga ni ukiukwaji wa ulipaji kodi
  • kwamba kutafutiwa sehemu nyingine ni swala lisilowezekana, kama ilivyo machinga complex
  • kwamba vitu vyote vinavyouzwa na machinga vimeagizwa nje na machinga ni outlet ya kutolipa kodi

  Majibu niliyopata hapo ya kusikitihsha kwa mtu ambaye anapaswa kujua kukubali au kutokubali maoni.Yakaanza matusi na shutuma kuwa "nyie watu wa system ndio mnaua nchi, mmefeli kuendesha nchi, mjinga we usinipigie tena, na mimi nimesafiri huko ulaya na ninajua"

  It was no use.
  Baada ya hapo nikamwambia asante ndugu
  Akanijibu usinipigie tena.

  Ndio Tanzania Daima -Sauti ya Watu
   
 2. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 848
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Masaburiiiiiiiii!!
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama ulijibiwa hivyo basi alikengeuka kidogo huyu mhariri isipokuwa alitakiwa akuleze kwa ufasaha zaidi . Mimi nakubaliana naye kwa mantiki moja tu kwamba wamachinga lazima wapate eneo moja ambalo ni rasmi ili wafanye shughuli kwa umakini
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,900
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Ndilo nilikuwa najaribu kumweleza kwamba juhudi hizo, kama za Kujenga Machinga Complex zimeshindikana, kabla ya mvua ya negative comments na kwa ujumla kujionyesha kuwa yeye ni mjuaji kwa vile ametembea sana duniani.

  Kwa msingi huo sioni jinsi gazeti hili linvyoweza kutoa kitu chenye umakini unaohitajika kueleimisha wananchi.
  Mbaya zaidi badala ya kupokea maoni-Sauti ya Wananchi-inasema usinipigie tena.
  Tanzania Daima Sauti ya nani sijui!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Serikali ya kistaarabu ikiwatimua watu wake mahara inawaonesha pa kwenda!
  Walikuwa wapi wakati watu wanaanza biashara pale sasa leo biashara zimeshamili wanawatimua bila ya kuwaonesha pa kwenda!
   
 6. b

  benzoo Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila mtu ni binadamu kwa ubinadamu wake,hayo ni majibu ya mhariri uliyeongea naye nazan si gazeti lenyew....
   
 7. k

  kautipe Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuhuma hizo ni nzito. Ninawafahamu wahariri wote wa Tanzania Daima na hasa huyo wa habari. Nimelazimika kumpigia na kuongea naye. Kwa bahati mbaya, hajajiunga katika jukwaa hili. Alichosema ni hiki: nanukuu_ "NDUGU YANGU ASANTE KWA TAARIFA. NI KWELI NIMEPIGIWA SIMU NA MTU HUYO, NA MAZUNGUMZO YETU YAMECHUKUA TAKRIBAN DAKIKA KUMI. KWANZA KATUPONGEZA KWA KAZI NZURI, LAKINI AKASEMA ANAPINGANA NA TAHARIRI YETU. NIKAMSIKILIZA HOJA ZAKE ALIZOTOA KWA LUGHA YA UUNGWANA. LAKINI NILIPOMUULIZA LABDA KWA MAONI YAKE ATUPE SABABU YA KWA NINI WAMACHINJA WANAKIMBILIA MIJINI HASA DAR ES SALAAM, AKADAI HAWEZI KUJIBU SWALI HILO KWA VILE ANAJUA NINAKOTAKA KUELEKEA. NIKAMUULIZA NAELEKEA WAPI, AKAJA JUU AKIDAI SIPASWI KUMUULIZA BALI NATAKIWA KUSIKIA AKISEMACHO KWA SABABU YEYE NDIYE KAPIGA SIMU. SASA UKIISHA KAA KATIKA NAFASI HII, YAKUPASA UWE MAKINI NA MVUMILIVU. NAMI NIKAMRUHUSU AENDELEE. AKADAI KUWA TAHARIRI YETU NI YA KIPUUZI KWA SABABU TUNATETEA UJINGA WA MACHINGA WASIOLIPA KODI. FIKIRI NDUGU YANGU, KAMA HUYU MTU ANAAZA KUTUITA WAPUUZI NA TUNAOTETEA UJINGA, UNAMFANYAJE? NIKAMUULIZA KAMA YEYE ANA WATOTO ANAKUBALI, NIKAMUULIZA NI JUKUMU LA NANI KUWAPANGIA WATOTO WAKE KAZI ZA KUFANYA NYUMBANI KULINGANA NA UWEZO WAO, AKASEMA MAMBO YA NYUMBANI KWAKE HAYANIHUSU, NADHANI HAKUELEWA SABABU YA SWALI LANGU. NIKAMUUULIZA, JE, KIJANA ANAYETAFUTA HELA YA KULA KWA KUFANYA KAZI HALALI NA YULE ANAYEIBA YUPI BORA KWAKE? HAKUJIBU, NIKAMUULIZA, JE, KWAKE UNGEKUWA NA HASARA GANI KWA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA YA WAFANYABIASHARA KABLA YA KUWATIMUA? AKADAI KUNA JENGO LA MACHINGA, NIKAMUULIZA JE, WALIOPEWA NI KINA NANI? HAKUJIBU. NIKAMUULIZA ALISHAWAHI KUSAFIRI NJE YA NCHI NA KUONA WENZETU WANAWASAIDIAJE MACHINGA HAWA? SASA BADALA YA KUJIBU, AKADAI KUWA TUNATUMIWA NA MAADUI WA NJE KUONESHA KUWA SERIKALI INAKANDAMIZA WATU WAKE NA HASHANGAI KWA SABABU HILI NI GAZETI LA WAPINZANI, NA NINA UPEO MDOGO WA KUFIKIRI. SASA KAULI HIYO SIJUI KWAO UNAIONAJE? NI YA MTU MWENYE MAONI YA KUJENGA AMA ANA AJENDA YAKE? NDIPO NAMI NIKAMWAMBIA ASINIPIGIE SIMU TENA KWA SABABU TAYARI AMESHANIONA NINA UPEO MDOGO KUFIKIRI!" Mwisho wa kunukuu

  sasa kama ni kweli haya ndio uliyomwambia, sidhani kama ulitenda vema. Pili, umetushirikisha je, ulijua kama na yeye angeweza kuingia katika mjadala huu akajitetea? Nadhani haya pia ni matumizi mabaya ya forum
   
 8. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhariri TZ daima si kama LUSINDE tu
   
 9. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,900
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru sana ndugu yangu Kautipe kwa kufanya follow up juu ya hii issue.
  Kwa kweli allegations zangu zina thibitisha kile nilichokuwa nina allege , na pengine ni mtu na si gazeti ambalo halitaki kuchukua maoni ya wananchi.
  Na huwezi kuchukua maoni yale mtu unayayoyapenda

  Kwanza kabisa NAKANUSHA hicho hapo kwenye red, kwani SIKUWAHI KUKISEMA wala kuashiria kitu kama hicho.

  Kwa taarifa yake mimi vile vile ni Mwanahabari, nina Redio Yangu na ninanunua magazeti KARIBU YOTE kila asubuhi ili kurusha habari za magazeti hayo asubuhi.
  Hivyo nilisikitika kwa matusi na kwa kuallege mimi ni "mtu wa system".
  Maoni ni kitu cha bure you take it or leave it.

  Nimekuwa nikiwasiliana na wahariri wengi sana kufuatilia habari ili kuzirusha tena redioni, lakini tabia hii sijawahi kukumbana nayo,ndio maana nikamwambia asante bwana, kwaheri

  Kwa kulisaidia gazeti lake lisiingie malumbano nafikiria kuacha kulinunua ili kulitendea haki.
   
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu, mimi sauti yangu inafanana sana na Lusinde juzi nimepiga simu sehemu wakawa wamenifananisha basi wakaanza kuni-handle kimatusimatusi, watakuwa wamekufananisha na mpuuzi fulani wa System
   
 11. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kwa taarifa yako wahariri wa magazeti huwa wanarekodi mazungumzo yote wanayofanya, pamoja na hayo uliyofanya leo. Sasa wewe ukijifanya unakanusha utaumbuka. Kubali tu kwamba na wewe ulikuwa LUSINDE leo
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo tahariri ina tatizo kubwa moja, unaposema wamachinga watengewe eneo au maeneo unamaanisha kama wamachinga sio wafanyabiashara. Hii ni kwasababu wafanyabiashara wanayo maeneo waliyotengewe ya kufanyia biashara. hii ipo kila kona ya jiji na ipo kote Tanzania. sasa hilo eneo analolitaka la wamachinga ni lipi tena?

  Ni ukweli wa wazi kuwa wanachofanya wafanyabiashara wakubwa ni kuleta mizigo na kuwapa vijana wakauze kiholela mitaani bila utaratibu wowote wa kurekodi mapato na hivyo hawalipi kodi.
  Na mtu anaposema wamachinga watengewe eneo nitamuuliza, kwani wamachinga wako wangapi? litengewe eneo la watu wangapi? Maana mtu yeyote anaweza kuamua kuwa mmachinga leo hii. Ukimuondoa mmachinga mmoja unakuwa umetengeneza nafasi ya mmachinga mmoja kuingia mtaani kuuza bidhaa kiholela, so kutenga eneo sio utatuzi.
  Kitu kingine ambacho mhariri anashindwa kukielewa ni kwamba hawa vijana wamachinga leo ukiwapa eneo watalazimika kulipia gharama za uendeshaji wa eneo hilo pamoja na kulipa kodi na kununua stock toka kwa wafanyabiashara wakubwa. Hiki ndicho wasichokitaka hawa wamachinga. Mbona Mangis wakija mjini wanakodisha vibanda na sehemu za kufanya biashara, kwanini ishindikane kwa wamachinga?
   
 13. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Watu makini wamekuelewa vizuri hapa, kuacha kulinunua kunaingiaje hapa??? acha utoto wee ungesema uache kutoa maoni na sio kulikomoa kwa kutokulinunua. Ngoja nikuweke kwenye Ignore list ili nikutendee haki.........Tukubhakana bhaaa!!!!!!!!!
   
 14. n

  nketi JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama huna shughuli nyingine njoo nikukodishe mkokoteni ukasukume. Umesema wewe km wewe naamini akija wa upande wa pili tutasikia wewe ndo ulikuwa wa kwanza kuporomosha mitusi ....tuondolee upuuzi huu.
   
 15. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,900
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Du mkuu mimi thio Luthinde, lakini kama kanda hiyo ipo ni vizuri ikachezwa(bila editing)
   
 16. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,900
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Basi.. basi.. mzee... nimekuelewa, sasa naenda pata lanchi, nilikuwa na fundo shingoni, angalesye fijo umundu uju!
  Over and out
   
 17. k

  kautipe Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mhariri amenitumia tena maoni yake. Nimemshauri ajiunge na forum hii, ili iwe rahisi kwake kuwasiliana na wasomaji wake. Hata hivyo, ameniomba niseme haya: ndugu yangu, ninasoma maoni ya watu hapa. Ukweli nimefurahi sana kwa michango yangu. Kama Mhariri wa gazeti ni haki yangu na wajibu kuwapa wasomaji na watanzani fursa ya kutoa maoni yako na kero zao. Sio kila maoni yatanifurahisha, na hata yale yanayonikosoa ama kukosoa gazeti ni wajibu wangu kuyapokea na kuyatendea haki. Nisichokubaliana nayo ni LUGHA ZA KUKASHIFIANA. Kukosoana ni tofauti na kukashifiana. Ndio maana nasisitiza, ili kuleta amani, ni kumwomba anayekashifu asiendelee kunipigia, na pia akumbuke kwa kutumia simu ama hata nami gazeti langu kumkashifu mtu ni kosa la jinai na unaweza kuishitakiwa
   
Loading...