Tanzania Daima na Nipashe ni Mafataani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Daima na Nipashe ni Mafataani...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zomba, Jun 7, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya machafuko amma ya kiasa amma ya kijamii kwenye nchi, waandishi wa habari na hususan wahariri wa magazeti wanatakiwa wawe makini sana na kuwa mstari wa mbele kutuliza machafuko kwa kuandika na kutoa habari ambazo zitaelimisha zaidi na kupunguza machafuko, kwani wananchi wengi huamini kila kiandikwacho kwenye magazeti kuwa ndio ukweli.

  Nimesoma kwa masikitiko makubwa kabisa, kuwa magazeti ya Tanzania Daima na Nipashe yameweka picha moja inayoonesha mtu akitokwa na damu na kuandika (caption) kuwa picha hiyo ni ya machafuko ya Zanzibar ilhali hiyo picha ni ya zamani na ilipigwa Morogoro.

  Soma zaidi "Uchochezi wa Kutisha Zanzibar" ujionee jinsi haya magazeti yanavyofanya ufataani: annuur-116
   
 2. u

  uwemba1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Katika vyombo vya habari vinavyochochea na kufitinisha watanzania kidini ni gazeti la al nuur na radio Iman daima hueneza chuki za wazi dhidi ya wakristo na naamini ingekuwa ni za wakristo, basi waislamu wangeandamana kitambo sana. Back to topic
  1. Kwa mtazamo, wangu cjaona niamini au nisiamini coz hao al Nuur huwa wanabase upande wa kuutetea uislam na waislam na kukandamiza wakristo

  2. Huenda ni Kweli picha hiyo imepigwa eneo tajwa maana matukio ya hivyo yalitokea. Maana magazeti yote tajwa hayachapishwi na mtu mmoja na Hayana uhusianao wa direct kuchapa habari inayofanana inanifanya niyaamini.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mzalendo net imekuwa ni ubao kwa watu wa Zanzibar kukashifu Tanganyika.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  zomba, ufataani ndio nini? Halafu Alnuur si mlengo wake na maandishi yake unajulikana unaegemea upande gani? Binafsi nafikiri ungetumia reference nyingine.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hivi Radio iman bado ipo? Haijafungiwa 2!
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  No research No right to speak.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ufataani ni kutoa habari sehemu moja ukazipeleka kwingine halafu ukazijaza uongo kwa nia kabisa ya kuwafitinisha watu.

  Kutoa picha ya Morogoro na kusema ni ya Unguja na picha hiyo ni ya damu, ni ufataani mkubwa sana.

  Kuhusu reference, hivi Annur wakazue kuhusu Tanzania Daima na Nipashe hawaogopi kufungiwa / kushtakiwa? Fikiri!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Tanzania Daima na Nipashe ni Mafataani..."

  Hicho ndio kichwa cha habari.
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  mkuu sasa nan kabisha? Au ndo kusema shuhuli na mihadhara ndo imeshakuharibu akili! Wape I hapo bububu zenji.
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,770
  Trophy Points: 280
  Mafataani ni neno la lugha gani sheikh wangu?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kiswahili.
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,770
  Trophy Points: 280
  Limetoholewa kutoka lugha gani?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani Kiswahili kimetokea lugha ipi?
   
 14. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,285
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  zomba , embu elewesha watu maana ya kiswahili ulichotumia , nini maana ya "mafataani" ??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Soma post #7
   
Loading...