Tanzania bado ni nchi nzuri, Ila wenzetu hasa huku Norway Kuna kazi nyingi na pesa ipo

Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
2,191
3,711
Kabla ya safari yangu ya kuja huku Norway, nioikutana na maneno mengi ambayo sidhani Kama mengine Yana ukweli kwa kuwa Sasa hivi najionea kwa macho.

Watu waache kukatishaa tamaa wenzao ambao wanataka kwenda kuishi au kufanya kazi nchi za nje.ukweli pia Kuna ugumu huku Ila wasikatishwe Sana tamaa, wacha waende wakutane na ugumu huko mbeleni.

Nimejifunza mengi kutoka kwa sisi wabongo, wengi tuna chuki Sana, Mara nyingi hata humu nimejitahidi Sana kujishusha kwenye mambo ya wengine ili kutowakatisha tamaa Ila mwisho unaonekana na wewe huna lolote. Tuache haya mambo.

Baada ya kuja huku kitu pekee ambacho niliona sio Cha kawaida ni kupuuzwa kwenye vitu vingi na hawa watu, pia hakuna Sana Cha kujuana sana kila mtu na mambo yake.

Kazi zipo nyingi na pesa ipo ila uwe unafanya Sana kazi mbalimbali, nahisi hata ni maisha ya Europe yote. Tukiwa huku tufanye kazi tu tuache mengine.

Wiki iliyopita nilipata kazi(kibarua) kwenye kampuni flani hivi ya ujenzi, kazi ilikuwa ngumu maana zile ngumu ndio tunafikiriwa akina sisi japo zina pesa Sana.

Baada ya kufanya vizuri kwenye hako kakibarua, ile kampuni ikapata tena tender ya ukarabati wa sehemu flani hivi airport kule Oslo, nikachukuliwa tena huko. Nimejifunza vingi sana kwa ukweli.

Ushauri wangu tukiwa huku tuweke uaminifu mbele na kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka, tuache lawama na ujanja usio wa maana.
Haya maisha nilichagua mwenyewe kwa kutaka kuja kuona huku Kuna nini na maisha gani.

Kazi kazi hakuna kucheka Wala kupiga soga

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, huku usilete Sana ushikaji na wabongo utaokutana nao kwa kuwa wengi huwa ni Kama wanakunja hivi bila sababu.

Chini ni picha yangu na matukio mengine

Screenshot_20210523-185704_1.jpg
Screenshot_20210523-192259_2.jpg
Screenshot_20210523-191921_1.jpg
Screenshot_20210523-192408_1.jpg
 
Hongera sana mkuu

Na pia shukrani kwa kututia Moyo wenye mikakati inayofanana na hiyo !

Nina maswali mawili

1. Je ulishapata kazi ukiwa huku bongo au uliitafuta pindi ilipofika ?

2. Kazi gani zapatikana huko sana , kwa watu waliosoma, ? Na je ni level gani ya elimu watu hupendelea kuajiri?
 
Hongera sana mkuu

Na pia shukrani kwa kututia Moyo wenye mikakati inayofanana na hiyo !

Nina maswali mawili

1. Je ulishapata kazi ukiwa huku bongo au uliitafuta pindi ilipofika ?

2. Kazi gani zapatikana huko sana , kwa watu waliosoma, ? Na je ni level gani ya elimu watu hupendelea kuajiri?
Sikupata nikiwa humu
Achana na kazi za kisomi, maana unaweza usipate kabisa. Kazi za vibarua ndio nzuri na za haraka
 
1.unatumia simu gani kupiga hizo picha
2.nitafutie hela unitumie Kama nauli nikufuate huko Norway nifikie kwako Kisha unitafutie mishe mishe nitakuwa nikilipwa nakurudishia deni lako
Asante
1) simu kweli ninayo mbaya, alafu sijali sana
2) siwezi kufanya hivyo, wewe cha kufanya tafuta njia zako ufike
 
Mleta acha kupotiosha. Kwanza hupo mji gani? Niko hapa Norway miaka 12. Huwezi kufika Norway na kuanza kazi za ujenzi. Halafu hali imebadilika sasa hivi kwa ajili ya corona wewe ni muongo.

Halafu nahisi wewe ndo yule jamaa wa uzi wa ukraine ukatoka ukraine ukaenda norway halafu dogo halafu unawaomba watu hela miliob 7 uwasaidie waende Norway.

Na ni jana tu mpaka wa Norway na finland ulifunguliwa. Norway ilifunga mipaka.

Kwanini mpotoshe watu.

Hali ya kazi Norway siyo kama zamani.

Nijibu tu huko mji gani kwasababu Norway naifahamu yote.
 
Back
Top Bottom