Kuhusu maandamano na uwajibikaji wa wananchi katika kuiwajibisha Serikali au kupinga jambo wakiwa kama waTanzania kwa ujumla wao,hizi za kina Chadema na ACT Wazalendo na wengine kama wapo ni mwanzo ulio mbali na hali halisi inavyokuwa, Tanzania hatujakumbwa na baa la njaa ya kufa mtu, Tanzania haijakosa hela ya kulipa mishahara na mambo mengi ambayo yanawagusa wananchi wote kwa ujumla wao
Sasa ikiwa hali inayofanywa na CCM itaendelea kuteka uchaguzi na mataifa yanayoisaidia Tanzania kuona misaada yao inaishia njiani na watakaposimama kikamilifu kutoa hata ndururu kulisaidia bunge na serikali basi hapo joto la shida na kulipana mishahara litakuwa juu na kumgusa kila mtu na kutakuwa hakuna tena kuoneana aibu na kuvumiliana.
Kuwekewa vikwazo vya uchumi ni jambo hatari sana hasa kwa dunia ya leo ambapo nchi zinategemeana kwa shida na furaha,Tanzania hatujawahi kuwekewa jambo hilo,ikiwa nchi tajiri zikiwekewa vikwazo zinayumba itakuja kuwa Tanzania.
Ukiwekewa vikwazo hata Mwenyezi Mungu anaviongeza vikwazo,muhogo hauoti wala mvua hazipo inakuwa ni mswalie mtume tu,sana sana tutatumia akiba kwa miaka miwili mitatu na kufunga mkaja lakini kila siku inakuwa ngumu,vikwazo ni hatari kwa serikali,serikali nyingi huanguka.
Ipo kujikaza kuwa tutavuka lakini sio rahisi kama mnavyosema,chukulia serikali inakosa hela ya kulipa mishahara kwa muda wa miezi sita tu basi vumbi lake sio dogo, tutaanza kubeba hela kwenda sokoni kwa mikokoteni.