Kila nchi inayo matatizo yake kulingana na historia yake kisiasa. Kwa bahati nzuri, kitendo cha Mwalimu Nyerere kuachia madaraka kwa hiari kilituwezesha baadaye kurekebisha katiba na kuweka ukomo wa kipindi cha urais. Hivyo, haiwezekani sasa, hayo yanayofanyika Uganda kutokea Tanzania. Badala yake, tunayo matatizo ya aina tofauti. Tatizo letu kubwa ni wateule wachache kutuchagulia viongozi wakuu wa nchi yetu kwa maslahi yao binafsi zaidi kuliko ya umma. Katika orodha ndefu ya watiania ya urais kutoka ccm, kwa hakika kulikuwa na watu wazuri zaidi na wenye maono zaidi kuliko Dk. Magufuli. Demokrasia ilipindishwa kupita kiasi wakilengwa watu wawili, Membe na Magufuli tu. Wengine wote wakaenguliwa kwa vigezo mbalimbali kama umri, utajiri, ufisadi, nk. Hili ni tatizo kubwa.
Kwanza kusema Tanzania HAIWEZEKANI kutokea kiongozi wa kung'ang'ania madaraka baada ya muda wake kwisha, sio sahihi hata kidogo... kilichopo ni kwamba, hadi hapa tulipofikia tumekuwa tukipata viongozi ambao anagalau wanaheshimu suala la mihula 2.
Kuhusu akina Membe; hapa jamvini nimeshasema mara nyingi sana... majority kama sio wote hatumfahamu JK! Kutokana na kutomfahamu huku, wengi wetu tumekuwa tukipiga ramli over the past 5 years kuhusu nani JK anataka kumwachia madaraka! Tukimtoa Lowassa, awali kabisa watu walikuwa wanasema Asha-Rose Migiro eti kwa sababu tu Mwislamu mwenzake... sie wengine tukaona ni madai ya kipumbavu! Baada ya Migiro, watu wakahamia kwa Membe. Kuna mtu yupo karibu sana Membe na huwa naongea nae sana... huyu nae aliamini kabisa kwamba JK atamwachia kiti Membe lakini, ingawaje hakutaka kunisikia, nilimwambia wazi sioni ni namna gani JK anaweza kumwachia kiti Membe... angeweza kushawishiwa na dhamira lakini uhalisia ukamkataza kufanya hivyo!
Baadae alipoteuliwa Jaji Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume, watu wakarejea kwenye ramli zao na kusema ni mbinu za JK kumwachia kiti Lowassa kwa sababu Lubuva na Lowassa ni mtu na shemeji yake!
Baada ya ramli zote hizo, sote tunafahamu nini kimetokea kwa Migiro, Lowassa na Membe! It doesn't take a genius to know kwamba endapo JK angetaka basi Lowassa angeingia 5 bora lakini JK alifahamu Lowassa akigusa 5 bora asingekamatika tena... kwahiyo ramli za kutaka kumwachia EL kiti zina-prove zilikuwa wrong. Pamoja na hayo, tangu zamani kulikuwa na kila dalili za Lowassa kuhamia CHADEMA endapo angekatwa--- kwahiyo, suala la EL kwenda CHADEMA halikuwa surprise kwa JK na team yake!
But it doesn't take a genius either kufahamu kwamba kukatwa kwa EL kungesababisha hasira za wafuasi wa EL kuhamia kwa Membe... kwa imani ile ile kwamba JK alikuwa anamwandalia njia Membe! JK na think tanks wake walifahamu hili na kwa makusudi akaamua kumpeleka Membe kwenye kisiwa kilichojaa mamba wenye hasira za kukatwa Lowassa! Hapa JK akafanikiwa kumridhisha Membe na dada ake Salma na pia akafanikisha lengo lake la kwamba "hiki kina ni kirefu kwa Membe!" Hiki kina ni kirefu kwa Membe coz' walishatarajia EL kwenda CHADEMA endapo angekatwa CCM na Membe asingekuwa na ubavu wa kupambana na Lowassa wa CHADEMA!!
Huyo Migiro sidhani ikiwa hata wewe unaamini angeweza kufurukuta mbele ya Magufuli ndani ya vikao vya CCM! Kwa maana nyingine kumbe hata suala la Migiro nalo ilikuwa ni ramli tu sawa na ramli zingine zozote! Neno moja linalotosha kumwelezea JK ni UNPREDICTABLE!
Sasa tukija kwenye hoja yako kwamba ndani ya CCM kulikuwa na watu wazuri kimaono kuliko Magufuli; nakubaliana na wewe! Hata hivyo, hakuna hata mmoja miongoni mwao ambae alikuwa ana ubavu wa kushindana na Lowassa wa CHADEMA-- HAKUNA unless kama unaamini chaguo zuri la CCM lingekuwa ni Lowassa! Kama ndivyo unavyoamini, hapa sikubaliani na wewe...!!
Hao wote wasingekuwa na ubavu wa kushindana na Lowassa coz' CHADEMA waliwekeza sana Kanda ya Ziwa! Membe asingekuwa na ubavu wa kuzipata kura za kanda ya ziwa mbele ya Lowassa! In fact, ukishamtoa Lowassa, wote ambao waliomba ridhaa kupitia CCM, hakuna hata mmoja ambae angeweza kushindana na Lowassa kanda ya Ziwa zaidi ya Magufuli... kwa sababu ile ile ambayo imefanya Lowassa amgaragaze Magufuli kanda ya kaskazini!
Labda tukumbushane tu kwamba, Kanda ya Ziwa ( ONLY Shinyinga, Geita, Mwanza, Geita) walijiandikisha about 3.8 million. CCM sio wapumbavu waache mtu mwenye uwezo wa kuzipata hizo kura kwa wingi ambazo, kinyume chake zingeenda kwa CHADEMA!
And you know what?No matter how intelligent the candidate can be but the MAIN GOAL is to win election. Kv sidhani kama EL angekuwa ndo best candidate kwa CCM basi hapakuwa na mgombea mwingine yeyote ambae angeweza kuwahakikishia ushindi CCM zaidi ya Magufuri! Na wala usidhani mimi ni shabiki wa Magufuri... am not! Mimi ni shabiki wa Mwakyembe na Muhongo!!
Lakini tumalizie jambo moja-- wengine walienguliwa bila shaka, according to you, kwa uonevu!! Kwanza, tusijidanganye kwamba kuna kuna chama kinaweza kupitisha mgombea bila scrutinizating-- HAKUNA!! Na ikiwa tunataka pasiwepo scrutinizing, basi tunatakiwa kulalamikia uwepo wa vikao vya CCM hususani kile cha maadili kuliko kulalamikia watu kukatwa! Inawezekana vikao hivyo vikatumika vibaya lakini kusema uwepo wake unapindisha demokrasia; HAPANA! Nasema hapana kwa sababu, assuming mimi na wewe ni watu wa kawaida, basi si mimi wala wewe anayeweza kujigamba kwamba anamfahamu vizuri mtu kama Asha-Rose Migiro, Mwakyembe, Mwandosya, Jaji Ramadhani... hatuwafahamu hawa watu! Majority ya wale watu wa Mkutano Mkuu nao hawawafahamu vizuri hawa watu... and, in fact, hata wale wa Halmashauri Kuu ya Taifa nao, hawawafahamu hawa watu! What you need to excel beyond Kamati Kuu is your popularity; BASI! Even a DRUG dealer can be very popular beyond Mkutano Mkuu if not beyond Kamati ya Maadili, huku watu wakiwa hawafahamu kwamba ni drug dealer. Kwahiyo suala la kuchujwa haliepukiki hususani kwa jamii iliyokosa maadili kama ya kwetu. Jambo la msingi ni kutendeka kwa haki lakini huku nao wakifahamu kwamba their main goal ni kushinda!
Ikiwa 2012 CCM walimtaka Lowassa ajivue gamba basi ingekuwa ni kituko cha karne endapo wangempitisha kugombea urais wakati hapakuwa na tofauti yoyote kuhusu Lowassa wa 2012 na huyu wa 2015!