Tanza-trotters wenzangu , hili daraja uliliona wapi?

Tanza-trotters wenzangu , hili daraja uliliona wapi?

Wale wauza mabilinganya na samaki wakavu bado wapo pale Mkuu?
Ha ha ha!
Hao hawakosekani hapo Ruvu mkuu, ingawaje juhudi yao ya kulima ni ndogo saaana.
Ila pale Ruvu,samaki aina ya kambale ni mwaka mzima!
 
Serikali tunaishauri iliwekee ulinzi, maana hapo kuna tons kadhaa za chuma chakavu!!! Chezea mtanzania mwenye njaa ya maendeleo kwani kila mtu anataka atimize kwa vitendo ile kauri mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania ifikapo mwisho wa mwaka 2015.
 
Kwa nini waliweka hayo mapipa? Any technical reason please?

bila hayo mapipa pembeni magari mawili yanaweza kupishana hapo, but daraja lisingeweza kuhimiri uzito uliozidi kima fulani ambao ungeweza kupatikana kutokana na magari mawili yatakayopita kwa wakati mmoja yakipishania hapo darajani, ndio maana wakaweka pingamizi ili lipite gari moja kwa wakati!
 
Nakumbuka hata maeneo flan baada ya kutoka mikumi kuelekea ruaha lilikwepo kama hilo na mbele kuna kona za kufa mtu kueleke daraja mbili hadi Iyovi iyovi hivi.
 
Serikali tunaishauri iliwekee ulinzi, maana hapo kuna tons kadhaa za chuma chakavu!!! Chezea mtanzania mwenye njaa ya maendeleo kwani kila mtu anataka atimize kwa vitendo ile kauri mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania ifikapo mwisho wa mwaka 2015.
Mama Mdogo hilo daraja lilisha ondolewa siku nyingi na Tanroads kupelekwa sehemu nyingine nchini.
Swali la mapipa halijajibiwa!
 
Last edited by a moderator:
bila hayo mapipa pembeni magari mawili yanaweza kupishana hapo, but daraja lisingeweza kuhimiri uzito uliozidi kima fulani ambao ungeweza kupatikana kutokana na magari mawili yatakayopita kwa wakati mmoja yakipishania hapo darajani, ndio maana wakaweka pingamizi ili lipite gari moja kwa wakati!
Hayo mapipa yaliwekwa baada ya ukaguzi wa kitaalaam, kwa nini?
 
Kudhibiti uzito utakaopita hapo kwa wakati mmoja!
Exactly,
Hayo mapipa yaliwekwa ili kudhibiti uzito unaoweza kubebwa na daraja kwa wakati mmoja.
Ikumbukwe kuwa daraja hili lilijengwa muda mrefu sana uliopita na lilianza kuoza kwa kutu(chini ya daraja) hivyo basi kutokana na kuongezeka kwa uzito unaobebwa na magari , daraja lingeweza ku collpse wakati wowote.


Leo kupita hapo ni raha mustarehe-ukiacha matuta pande zote mbili wa daraja
 
Back
Top Bottom