Tanroads zigo kwa Waziri Kawambwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanroads zigo kwa Waziri Kawambwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Mtendaji Mkuu haivi na viongozi wa wizara
  [​IMG] Anafanya maamuzi makubwa bila baraka zao  [​IMG]
  Waziri wa Wizara ya Miundo Mbinu, Dk. Shukuru Kawambwa.  Shughuli ndani ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), haziendi sawa kutokana na kutoelewana kati ya Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Ephraem Mrema, na viongozi wakuu wa Wizara ya Miundombinu.
  Viongozi hao ambao inadaiwa kuwa Mrema amekuwa akifanya maamuzi bila kupata baraka zao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Omar Chambo na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa.
  Taarifa za uhakika kutoka wizarani, Tanroads na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, zinaeleza kuwa kutokana na Mrema kufanya maamuzi bila kupata ushauri wa Chambo na Kawambwa, mambo mengi hayaendi sawa.
  Kufuatia hali hiyo, wakandarasi wanaofanya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Tanroads pamoja na wale ambao wamekamilisha miradi hawajalipwa kutokana na misuguano hiyo.
  “Sisi mameneja wa mikoa ambao tulisimamishwa mwaka jana hatuthubutu hata kuomba miradi mipya kwa sababu utamwomba nani na mtendaji mkuu (Mrema) hataki kutuona? Tunaogopa kuomba miradi kwa sababu kwanza hatuna pa kuipeleka na hatutapewa pesa za kuitekeleza,” alisema meneja mmoja wa mkoa ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
  Taarifa kutoka Wizara ya Miundombinu zimeeleza kuwa Mrema amekuwa akifanya maamuzi ndani ya Tanroads kwa kisingizio cha kuagizwa na Rais jambo ambalo linamkera Chambo na kulazimika kumwandikia barua ya kumtaka ajieleze.
  Barua ya Chambo kwenda kwa Mrema ya Desemba 18, mwaka jana ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, inamtaka Mrema kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kutekeleza majukumu yake na maagizo bila kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
  “Tarehe 28, Oktoba, 2009, kupitia barua yako yenye kumb. TRD/CE/GEN/09/Vol.1/052d uliwajulisha washirika wa maendeleo kuwa ulishafanya mabadiliko ya watumishi Tanroads…hata hivyo, hatua ya kuwafahamisha washirika wa maendeleo ni uvunjifu wa taratibu kuhusu mabadiliko ya viongozi serikalini,” ilisema sehemu ya barua ya Chambo kwa Mrema.
  Barua hiyo ambayo inaonyesha Chambo alipeleka nakala yake kwa viongozi wa juu serikalini akiwemo Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi, inaeleza kuwa mabadiliko ya watumishi ndani ya Tanroads yaliyofanywa na Mrema mwishoni mwa mwaka jana yalikiuka maagizo ya Wizara ya Miundombinu ambayo ilimkataza Mrema kufanya hivyo.
  “Tarehe 30, Oktoba, 2009 uliwatangazia wafanyakazi kuwa umefanya mabadiliko ya viongozi Tanroads kinyume cha agizo langu kupitia barua yangu ya Oktoba 26, 2009. Oktoba 30, 2009 nilikuandikia barua yenye kumb. Na. MWC/PF.M.5489/11 nikikusisitizia usitishe mabadiliko ya wakurugenzi na mameneja wa mikoa mara moja, kutekeleza mabadiliko hayo kinyume na agizo langu ni uvunjifu wa nidhamu (insubordination),” alisema Chambo.
  Chambo anaeleza zaidi kuwa: “Kwa barua yako ya Novemba 9, 2009 yenye kumb. Na. TRD/CE/GEN/09/Vol.1/0529 ulidai kuwa mheshimiwa Rais alikuita na kukuagiza uendelee na mabadiliko ya viongozi kitu ambacho siyo kweli. Kwa kisingizio cha maagizo ya mheshimiwa Rais uliendelea kufanya mabadiliko ya viongozi Tanroads bila kujali agizo langu…aidha, hata kama uliitwa na Rais, ulitakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu kabla hujaitikia wito huo kwa lengo la kuzingatia mtiririko wa mawasiliano (chain of command) huu ni uvunjifu wa nidhamu.”
  Barua hiyo ya Chambo inaeleza bayana kwamba kiburi cha Mrema kimesababisha kazi za wakala kuzorota.
  “Kufuatia kutozingatia maagizo unayopewa na viongozi wako kumesababisha kazi za wakala kuzorota kutokana na watumishi kukata tamaa kwa sababu ya matatizo mengi ya kiutendaji yaliyopo katika wakala wa barabara,” alisema Chambo.
  Taarifa zinaeleza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, iliwakutanisha Februari 3 mwaka huu kwenye kikao mjini Dodoma kwa nia ya kumaliza tofauti zao.
  Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, ameliambia gazeti hili kuwa baada ya Chambo, Mrema na Dk. Kawambwa kupatanishwa, kamati iliwaagiza kukutana na bodi ya wakurugenzi ili kumaliza kasoro za mchakato wa ajira za watendaji wa wakala huo.
  “Lakini katika hali ya kushangaza, Katibu wa Kamati yetu alipindisha maagizo ya kamati…tumeshangaa kupata barua ya Chambo akiomba ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati,” alisema mjumbe huyo.
  Pamoja na mambo mengine, barua hiyo ya katibu wa kamati, Justina Shauri, namba BC50/73/01/34 ya Februari 8, mwaka huu, inataka mchakato wa kujaza nafasi mbalimbali za watendaji wa wakala huo uanze sasa na kukamilika baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba.
  “Kwa kuwa mchakato huo utachukua muda kukamilika, mtendaji mkuu wa Tanroads awateue haraka sana wale watakaokaimu nafasi za uongozi hadi hapo watakapopatikana watu wa kujaza nafasi hizo,” ilisema sehemu ya barua ya katibu wa kamati, ambayo hata hivyo, siyo ya kweli kwa mujibu wa mjumbe huyo.
  Kutokana na maagizo hayo yanayodaiwa kuwa ni ya kutunga, Chambo alimwandikia barua Mwenyekiti wa kamati hiyo kutaka ufafanuzi.
  “Tunaomba mheshimiwa Mwenyekiti utupe ufafanuzi namna ya Serikali kutekeleza yale yaliyoandikwa na katibu kwenye barua hiyo kwa sababu ama hayakutolewa na kamati yako ama yanakinzana na sheria za nchi,” ilisema sehemu ya barua ya Chambo namba JA230/317/01 kwenda kwa mwenyekiti wa kamati.
  Chambo ambaye katika barua yake ameonyesha kukerwa na kitendo cha katibu wa kamati kupindisha maagizo ya kamati, amelazimika kupeleka nakala ya barua hiyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa umma, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanroads.
  Tayari bodi ya Wakurugenzi wa Tanroads imeona hali ya wakala huo na kumwomba Waziri Mkuu kuingilia kati ili kuepusha hatari zaidi.
  Barua ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanroads ya Aprili 12, mwaka huu kwenda kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imeeleza jitihada zake za kunusuru Tanroads zimekwama na kumuomba Waziri Mkuu, kuingilia kati.
  Katika kile kinachoonekana Mrema hana sifa ya kushika wadhifa huo, mwaka 2008 baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimwandikia barua Waziri Kawambwa na Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia ili mawaziri hao wampe ushauri juu ya kushughulikia matatizo ya Tanroads.
  Barua ya Ghasia namba C/CA273/450/01/36 ya Oktoba 22, 2008 pamoja na mambo mengine, ilimshauri Waziri Kawambwa kumshauri Rais atengue uteuzi wake ili kuinusuru Tanroads.
  Barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilifafanua: “Kamati hiyo ikibaini utendaji wake wa kazi una mashaka au uteuzi wake una athari katika ufanisi wa taasisi anayosimamia, Rais ashauriwe kutengua uteuzi wake kwa madhumuni ya kuimarisha uongozi na ufanisi katika taasisi hii nyeti.”
  Kawambwa jana hakupatikana wakati Chambo alipopigiwa simu alisema yuko nje ya nchi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. D

  Divele Dikalame Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ya Tanroads yameshasemwa sana hakuna hatuwa yoyote inayochukuliwa shidi ya bwana Mrema, inadhihirisha kuna watu wanamlinda huyobwana kiswahili sanifu wanakula nae.
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  pamoja na utovu wa nidhamu tulishasema sana kuhusu huyu bwana Mrema jinsi anavyoingizia hasara Taifa ktk miradi.........mbalimbali ya barabara

  kwa Eng. Chambo.....Katibu Mkuu:
  Misuguano yenu isiwe sababu ya kutolipa malipo halali (certified) ya wakandarasi

  kwa Kamati ya Miundo Mbinu:
  Ujenzi ni idara mojawapo inayochukua sehemu kubwa sana ya bajeti ya serikali. Kuendekeza personalities eti "kupatanisha".......ni kulea maovu katika utendaji...............inabidi muwe wakali...............hapa mnachezea billions za wavuja jasho..........it appears you don't consider about walipa kodi and you talking about "kupatanisha"............mtu akichemka inabidi awajibishwe....PERIOD

  kwa Luhanjo na JK:
  Tengua uteuzi wa huyu Mrema.
   
 4. B

  Bobby JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ogah naomba niongezee kidogo;

  Kwa watanzania wenzangu;
  PIGA CHINI SERIKALI YA CCM ILIYOJAA KULINDANA NA UFISADI HUKU IKIWEKA KANDO MASILAHI YA WALIPA KODI NA WANANCHI KWA UJUMLA.Hata heading ya habari natamani ibadilishwe iwe "Tanroads Zigo kwa walipa kodi" kwani hiyo hasara ya mabilioni tunayopata ni sisi walipa kodi sio waziri.

  Halafu Tanzania eti haivi. kuiva ndio nini hii ni kazi ya wananchi jamani masihara kwenye kodi za maskini hawa wa Tanzania hayapaswi kuwepo.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  The only difference between those in power and normal civilian is that the former have platform, well informed and can use the platform to fool the later for the later depend on manipulated information from those in power.
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kelele zote Mrema yeye yuko kimya...hata picha yake sijawahi iona
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Huu ni upuuzi mtupu. Kikao cha kumpatanisha Mtendaji Mkuu, Katibu Mkuu na Waziri kilikuwa cha nini? Kama mtu anashindwa kutekeleza wajibu wake kikao cha nini cha kumpatanisha na viongoz wake? Kama kafanya " gross insubordination", Katibu Mkuu anaogopa nini kumsimamisha kazi? Hiyo bodi ( au chochote wanachokiita) ya Tanroad inafanya nini wakati wote huu? Ninavyojua mimi Chief Executive wa Tanroad hachaguliwi na Rais bali Waziri. Tanroad ni executive agency na sio idara ya serikali. Ndio maana katika masuala ya uongozi wa wakala huo, CE hatakiwi kutafuta ushauri wa Rais, Waziri au Katibu Mkuu. Contract ya ajira yake ni performance based na atapimwa kutokana na utendaji wake na sio jinsi alivyowashirikisha wakuu. Kisingizio kuwa aliagizwa hautakiwi kupewa uzito. Yeye anatakiwa awe Technocrat na sio mwanasiasa. Hawa jamaa hawatutendei haki.

  Amandla.....
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huyu ni binamu wa Sindibadi hata tuseme hadi kesho hawezi mfanya chochote!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Miye nilidhani ni Mchagga kumbe Mkwere...
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mchagga wapi mkubwa umesahau majina ya hawa wakwere? kama ya Songea mara Kawa mbwa, Ki' wete, ujue jimbo alilotoka Sindibadi kama mbunge ndo huyu aliingia na hadi sasa anaongoza kwa kuzungukia wizara nyingi kwa muda mfupi kuliko mawaziri wote wa sasa!
   
 11. k

  kisikichampingo Senior Member

  #11
  May 14, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi huwa napata kichefuchefu masuala ya Tanroads. Mporogomyi alimlipua Mrema hadi bungeni na haikusaidia kitu! Mnaonaje tukijadili hoja nyingine?
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Katibu Mkuu Chambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroads wamekosana lini tena, si juzi juzi tu baada ya Katibu Mkuu kuidhinisha mishahara mipya kwa wafanyakazi wa Tanroad, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroad akaidhinisha malipo ya "Honorarium" kwa Katibu Mkuu na wasaidizi wake ambapo takiri bani Milino 80 zilitumika kuwalipa kwa kutimiza wajibu wao wa kuidhinisha mapendekezo ya taasisi iliyo chini ya wizara wanaoyoiongoza.

  Gazeti la Raia Mwema liliripoti na kutoa photo copy ya cheki husika. Kam kuna mtu yoyote anakumbuka malipo haya atusaidie kupost hiyo stori kutoka Raia Mwema.

  Hawa wote ni wezi sasa wameibiana wanagombana kama vibaka baada ya uporaji, isipokuwa kugombana kwao badaa ya kukufanyia mitaani kama vibaka wanafanyia kati viyoyozi vinavyolipiwa na wavuja jasho wa nchi ambao wameambiwa hakuna pes za kuongeza mishahara.
  Asante
   
Loading...