TANROADS na Manispaa ya Ubungo shughulikieni suala la foleni Mbezi

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Pamoja na juhudi za Serikali kujenga barabara za lami eneo la Mbezi lakini hali ya foleni ni mbaya sana kutoka na kuingia barabara ya Kinyerezi.

Tatizo kubwa ni kuwa barabara imejengwa nyembamba sana haina hata sehemu ya dharura hivyo gari likisimama au kupata shida linasababisha foleni kubwa.

Tatizo la pili ambalo ndilo kubwa zaidi ni wafanya biashara wamachinga kugeuza barabara kuwa soko. Hawa wamejenga vibanda juu ya mifereji ya maji na kwenye maeneo ya watembea kwa miguu kiasi kwamba imekuwa shida sana kwa watembea kwa miguu kulazimika kupita barabarani sambamba na magari.

Wafanyabiashara wenye matoroli nao wanapanga matoroli yao siku nzima barabarani kabisa na ikifika jioni barabara nzima inajaa matoroli hivyo kuifanya barabara kuwa nyembamba zaidi na kusababisha magari kushindwa kupishana au kupitishana kwa taabu.

Wakati haya yana tokea viongozi wa TANROADS na Manispaa wako kimya kabisa wanasubiri ajali kubwa itokee ndipo waunde tume na kuanza kuwaondoa wafanya biashara hao barabarani na sehemu za watembea kwa miguu ambao ni waathirika wakubwa wa msongamano huu usio wa lazima.

Ifike mahali ijulikane nani anayepaswa kusimamia matumizi sahihi ya barabara na kwanini ameachia hali kufikia ilipofikia? Je TANROADS kazi yake ni kujenga tu lakini haihusiki na matumizi sahihi ya barabara hizi? Je manispaa ndio wasimamizi na wamechukua hatua gani? Au wote wana ngoja kauli ya rais?!

Utashangaa manispaa inakusanya ushuru kwa wafanya biashara hawa wa barabarani
 
Hilo eneo ilifaa lujengwe njia ya chini kwa kutumia hayo mabonde yaliyopo iwapo flyover itakuwa gharama

1606378987791.png
 
ilo la machinga nakuunga mkono kila kona wamekua kero hata sisi watembea kwa miguu hatuna raha ya kutembea make unaogopa kumwaga vitu vya machinga huku boda boda wanakukosakosa
 
Back
Top Bottom