Tanroad mnafeli wapi? Daraja siku 3 bado halipitiki?

Tanroad mnafeli wapi? Daraja siku 3 bado halipitiki?

Nilipomuona Magufuri asbhi pale ubungo jinsi alivyokuwa anamsikiliza Muhandis Mfugale nilihisi kitu maana alikuwa kama anampotezea hivi, kumbe alikuwa anaenda kumpa yake Morogoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuseme ukweli wizara ya ujenzi imepwaya sana pamoja na tanroad.

Pia sidhani kama tuna engineers wenye uwezo wa kutoa solution za haraka na zenye mashiko maana kazi ya engineer sio kupiga chepe bali ni kutoa solution za kihandisi na kisayansi kutatua matatizo kwa muda muaafaka.

Kama anavyo sema waziri mkuu ni aibu ya nchi siku 3 hakuna suluhu ya magari kupita kati ya dodoma na morogoro.

Kwanini baada ya daraja kuvunjika kusitafutwe njia mchepuko magari yapite wakati mnaendelea kutengeneza daraja?

Daraja hilo halihitaji kutengenezwa kama la muda inabidi litengenezwe la kudumu penhine bora kuliko lililokuwepo.

Mmeng'ang'ania kufukia kifusi na mawe ambayo mvua ikinyesha tena vitaobdolewa au daraja kutitia.

Inaonekana tanroad na wizara ya ujenzi hawaja jipanga kwenye majanga kama haya au kwa vile kamanda wenu JPM kapata kazi nyingine.

Nakumbuka kuna mwaka alillala site hapo morogoro hadi daraja likakamilika kwa wakati huku magari yakiendelea kupita.

Mapendekezo

1. Kwa mkoa wa morogoro Tanroad wabadilishe calvert za kutoka pipe culvert na kuweka box culvert au bridge culvert kwa madaraja yote ya mkoa wa morogoro.

2. Regional engineers wasimamiwe vizuri maana wengi hawayembelei barabara. Unakuta barabara ina shimo kubwa na lipo hata kwa miezi 6 wakati fedha za ukarabati zimekaliwa na engineers.

3. Kiundwe kikosi cha emergence kwa ajili ya majanga kama haya.

Nimekuhurumia sana eng kamwele unafanya kazi na watu wazito kuchukua maamuzi na wasio na ubunifu kwenye kazi zao.

View attachment 1377065

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu john kama vile anamuogopa Mfugale au macho yangu yanaona vibaya
 
Mkuu yawezekana una hoja. Ila hili unaloona kuwa daraja la Morogoro ambalo hadi waziri mkuu kafika, kwingine hali iko hivi:

Rusumo - Rusahunga njia kuu kwenda Dar taswira halisi ya awamu ya tano - ukweli mchungu

Barabara ya Rusahunga Benako: Imefunga tokea jana zaidi ya masaa 24 sasa

Kelele zimepigwa hadi tumekaa kimya. Maana kumpigia mbuzi gitaa ni shughuli pevu. Morogoro angalau manager tanroads kapata stahiki yake:

Meneja Tanroad arudishwa wizarani kwa kushindwa kukagua madaraja

Kwingine je?

Hali ya Chatto ni tofauti sana. Barabara zote mjini takribani ni za lami inayoambatana na mitaro swafi. Barabara zote kuu kuingia na kutoka Chatto hapo usiseme (japo hakuna magari kihivyo) lakini barabara hizi ziko utadhani uko Marekani. Vivyo hivyo kwa traffic lights zao - classic:
Hivi inakuaje Moshi pana magari Mengi kuliko chato lakin hakuna traffic lights, Ila chato Kuna traffic lights
 
Tatizo la Tanzania tunaingiza siasa kila sehemu hakuna injinia anaeweza kujenga daraja kwa siku tatu tusidanganyane

Hiyo nguzo tu ya zege kama itachimbiwa kwa ajili ya kubeba daraja siku 3 inakuwa bado haijakauka

Madaraja ya kujenga siku 3 ni madaraja ya kijeshi

Ilitakiwa jeshi wajenge hilo daraja la siku 3 kisha mainjinia wa tanroad wajenge taratibu daraja la kudumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa sasa serikali inahamia Dodoma inabidi zijengwe barabara nyingi zinazoingia na kutoka Dodoma

Sasa kama kabarabara chenyewe kamoja tu Dar Moro Dodoma ni hatari sana

Barabara haipitiki na last wk ndege ilitoka Dar kwenda Dom ilipofika Dom ikashindwa kutua kwa sababu ya ukungu ikabidi irudi Dar

La Dodoma llishashindikana
 
Walitakiwa wajenge daraja la muda au njia mchepuko ndio waendelee na mambo yao

Back
Top Bottom