Tani 4,852,851 za korosho ghafi zauzwa Lindi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
1574852904831.png

Tani 4,852,851 za korosho ghafi zimeuzwa katika minada miwili iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Lindi na Nachingwea mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.

Kaimu Mrajisi wa Vyama vya msingi vya ushirika mkoani Lindi, Robert Nsunza alisema tani 2,111 ziliuzwa katika mnada Nachingwea Jumapili. Wanunuzi walitaka tani 13,000.

Bei ya juu katika mnada huo ilikuwa Sh 2,812 na chini Sh 2,790 korosho ghafi. Zilizokuwapo katika maghala ya Ruangwa zilikuwapo tani 1,017, Nachingwea tani 323 na Liwale tani 770.

Nsunza alisema mnada huo ulisimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Runali kinachotoa huduma Wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale. Kampuni 17 zilishiriki mnada huo.

Alisema kampuni nane zilizoshinda mnada huo ni Kampuni ya Aiscon cashew nuts, Sunshine, Nafaka, CDGKL Nuts na Kasuga general MGM Royal nuts na Micromics cashew nuts.

Alisema mnada uliosimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao waliuza tani 2,741.832, mahitaji tani 8,913.437 za korosho. Alisema katika mnada huo, ghala la Buko zipo tani 117.851 daraja la kwanza na la pili tani 30. Bei ya juu ilikuwa Sh 2,697 na chini Sh 2,519 korosho ghafi za daraja la kwanza na daraja la pili bei ya juu Sh 2.329. Hapakuwa bei ya chini.

Ghala la Mtama kulikuwa na tani 821.87 daraja la kwanza na bei ya juu ilikuwa Sh 2,727 na chini Sh2,660 kwa kilo moja ya korosho ghafi. Alisema ghala la Nangurukuru Wilaya ya Kilwa kulikuwa na tani 684.100 daraja la kwanza iliyouzwa Sh 2,667 na bei ya chini ilikuwa Sh 2,511.

Korosho daraja la pili iliuzwa kwa sh 2,329. Zilikuwapo tani 88.786 za korosho ghafi. Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi mwambao, Nurdini Swallah alisema kampuni zilizoomba kununua korosho mnada wa kijiji cha Nyangao zilikuwa 10, barua za maombi 45.


Chanzo: Habari Leo
 
Hata mim chenga tu maana toka nikifatilia Mambo haya miaka yote tunakusanya tani 180000-200000 sasa hapa tani 4 000.000 ufafanuzi kidogo mtoa mada
 
Uzalishaji haujawahi fika Yani Laki 3 kwa Mwaka inakuwaje leo wanauza Tani Milioni 4? Au walizitunza kwa miaka 15?
 
Uzalishaji wa korosho Tz nzima haujawahi fika Laki 3 kwa mwaka. Inakuwaje wanauza tani milioni 4?
 
Kweli wewe ni kilaza mkubwa hizo tani hata dunia haizalishi kwa mwaka@elivina shambuni,
 
Masasi tumeuza korosho kwa bei ya tsh 2500/= hapa itakuwa hata hii bei tumegipwa changa la macho
 
Warudishe mfumo wa zamani wa wanunuzi wenyewe kupeleka magunia wao wenyewe
Naambiwa kuna changamoto kubwa sana ya magunia, mfano hapo matajiri walitaka tani 13,000 lakn kwa kuwa hakuna magunia wameuziwa tani 2111.. Mkulima ana korosho ila gunia za kuhfadhia hakuna. Serikali itatue hili tatzo, ikiwezekana msimu ujao wakulima aidha wajinunulie wenyewe au wachangie kupitia makato kwa kilo kuepusha usumbufu huu.
 
Huyu mleta mada ni hopeless kabisa! Zaidi ya tani milioni 2!!! Kwa nchi nzima hatujawahi kuzalisha hata tani laki 3 kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom