Tangu ninaishi na huyu mchumba sijawahi kula chakula chake

Jana Ulirudi Usiku

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
2,363
2,261
Ni miezi 11 sasa, tunaishi pamoja ila simuamini bado kiasi chakula chochote alichoandaa pasipo mimi kujua wala kuona kwa macho yangu.

Kama ni kulala basi tunalala vyumba tofauti, ni ngono ndiyo inatuweka chumba kimoja kwa muda. Issue kubwa ni kuwa ninakwepa kulishwa limbwata na kuwekewa dawa zingine za kipuuzi.

Kwa mama n'tilie na hotelini nakula kwa sababu kule huwezi wekewa limbwata. Ila yeye hajui sababu hasa ni nini na ananishangaa mpaka leo. Ila msimamo wangu ni ule ule.

Hebu semeni, ananipataje huyu? Yaani nipo makini sana, hata nikimuoa nimeshamuambia mwendo ni huu, sitohitaji chakula chake, only that.

Naonekana wa ajabu, najua hili ila ndivyo nilivyo, binadamu hatuwezi kufanana.
Ameshaanza kuwaambia shoga zake na mpaka nyumbani amewaambia. Nishaitwa sana ila msimamo wangu ni ule ule.

Sababu kubwa nawaambia sipendelei tu kwa sababu uchumba wetu ni mchanga.

Najishangaa why nimekuwa hivi? Wivu pia sina kabisa yaani. Sina historia ya kuwa na wivu, naweza hata kumpa lift au kumtoa lunch mwizi wa mke wangu na siwazi wala nini. Sijui ndiyo nini hiki!

Ooooosh
 
Nashauri mafunzo ya jando yatengenezewe mfumo rasmi wa kistaarabu wafundishwe vijana kwenye somo la sayansikimu huenda tutajenga jamii yenye vijana imara kwenye mahusiano ya uchumba/ndoa.
 
Back
Top Bottom