Mwenzenu nimekuwa nakwazika na lile tangazo la Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) linalotolewa na baadhi ya vituo vya televisheni kuhusu umuhimu wa kupewa risiti unaponunua mahitaji yako dukani...Yule mwenye duka (wa kwanza) ana lafudhi ya watu Fulani kutoka eneo moja nchini mwetu...Huyu mwenye duka inaonekana kuwa ni mkwepa kodi...lakini yule mwenye duka wa pili inaelekea siyo mkwepa kodi, kwani anatoa risiti haraka haraka kuliko yule wa kwanza ambaye anafoka pale anapoulizwa kuhusu risiti...sasa mimi napata tafsiri tofauti...ikiwezekana waliotengeneza tangazo hilo warekebishe kuhusu suala la lafudhi ili isionekane watu hao na ambao ni watanzania wenzetu ni wakwepa kodi.