Tangazo la maelezo ya ajira - MSD

Tangazo la maelezo ya ajira - MSD

HONGERENI MULIO ITWA KWENYE USAILI...mimi hakuna cha sms wala kupigiwa simu,..ndo ishakula kwangu
 
HONGERENI MULIO ITWA KWENYE USAILI...mimi hakuna cha sms wala kupigiwa simu,..ndo ishakula kwangu
Usikate tamaa mkuu, endelea kuomba maeneo mengine zaidi. Inawezekana haikuwa bahati yako hiyo.
 
Wakuu sina haja ya kuzingua mtu humu sikujui hunijui, nikuzingue ili iweje, hujalazimishwa kuamini, mie nawaambia kitu halisi
Wamenitumia Ujumbe unasema "Ndugu (JINA LANGU) MSD inakukaribisha kwenye usahili kwa nafasi uliyoomba ya Software Developer itakayofanyika siku ya jumamosi tarehe 29/4/2017 saa 4.30 asubuhi chuo cha IFM, Dar es salaam. Tafadhali fika na kitambulisho chako. MSD haitahusika na gharama za usafiri. Kwa maelezo zaidi piga 255 222860890/7
Tupe mrejesho wa interview...vipi mlikua wengi ?..pepa ilikuaje
 
Dahhhhhhhhh........!!!!!hawa jamaa wameitwa kweli bhana,kuna brooo amenipa mtonyo kwamba kuna rafiki yake ametumiwa msg pamoja na kupigiwa simu ametoka kufanya juzi nyomi la maana,ANYWAY TULIOKOSA KUITWA TUSIKATE TAMAA .
 
Tupe mrejesho wa interview...vipi mlikua wengi ?..pepa ilikuaje
kusema kweli Software Developer hatukuwa wengi total tulikua 39, Accountants na Pharmacist ndo walikua wengi sana hata pepa walifanya kwa batch.
pepa was amptitude kupima uwezo wa kufikiri no field question, tulipiga kwa computer 20 min tu ,maswali 50 na ni kuchagua.

wamesema tukifikia alama zao bas watafanya utaratibu kama huu waliotumia kutuita
 
Mkubwa kwa kada za administrative officer, marketing and sales vp walikuepo au, niliapply@ meshack
 
Mkubwa kwa kada za administrative officer, marketing and sales vp walikuepo au, niliapply@ meshack
mkuu sina hakika na hilo, ila tulikua kwenye hall moja ivi wote ndipo wakatuambia IT waende huku, accounts waende huku na phamarcist vivyo hivyo, IT tulikua wa mwisho tulipotoka ile hall ikawa empty..
 
Msd in hustori ya kuingiliwa na matapeli kwenye ajira
 
View attachment 488948

TAARIFA KWA UMMA UTAPELI KUHUSU KUITWA KWENYE USAILI

Hivi karibuni Bohari ya Dawa (MSD) ilitangaza nafasi za kazi mbalimbali,ambapo imekamilisha kupokea maombi tangu tarehe 14/3/2017. Kwa sasa MSD ipo katika Hatua za kukamilisha uchambuzi wa sifa za waombaji kulingana na nafasi walizoomba. Waombaji wote watakaokidhi vigezo wataitwa kwa ajili ya usaili na hata wale ambao hawataitwa kwa ajili ya usaili watajulishwa kwa utaratibu ambao Ofisi itauweka. Kumezuka matapeli wanaowapigia wananchi simu za kuitwa kwenye usaili. Wananchi wote mnaombwa kupuuza simu mnazopigiwa na watu hao wanaodai kuwa ni wa Bohari ya Dawa, zikidai kuwaita kwenye usaili na kuombwa kutuma shilingi 70,000/= au fedha yoyote. Watu hao ni matapeli na hawahusiki na Ofisi ya Bohari ya Dawa (MSD). Endapo unahisi kuna mtu anakupa taarifa hizo tafadhali piga simu na omba kuongea na Ofisi ya Rasilimali Watu au tuma Barua pepe kwa anuani:
maoni.dg@msd.go.tz ,

Kwa ufafanuzi zaidi, wasiliana moja kwa moja na MSD kwa kupiga simu ya mezani namba +255 22 2860890 - 7

Imetolewa na
Etty Kusiluka
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bohari ya Dawa (MSD)
22/03/2017

“ Tumedhamiria Kuokoa Maisha Yako ”
ila na nyie mmezidi toka march mpaka leo mnaendelea na mchakato,RAIS ashakataza haya mambo ya mchakato......muda mrefu mnaochukua toka kutangaza kazi na kuwaida ndo yanaleta mazingira haya ya utapeli na rushwa ndani yake.Kama hamjajipanga msitangaze mpaka mjipange wenyewe ndani ndo mtangaze.....HAMKO SEROIUS!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kusema kweli Software Developer hatukuwa wengi total tulikua 39, Accountants na Pharmacist ndo walikua wengi sana hata pepa walifanya kwa batch.
pepa was amptitude kupima uwezo wa kufikiri no field question, tulipiga kwa computer 20 min tu ,maswali 50 na ni kuchagua.

wamesema tukifikia alama zao bas watafanya utaratibu kama huu waliotumia kutuita
Vipi hao accountants nao walifanya kwa computer au ilikuwa ni written paper nao vipi waliulizwa Maswali kama yenu au kulikuwa na tofauti ya Maswali
 
Back
Top Bottom