SHOOyaKIBABE
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 2,181
- 1,707
TAARIFA KWA UMMA UTAPELI KUHUSU KUITWA KWENYE USAILI
Hivi karibuni Bohari ya Dawa (MSD) ilitangaza nafasi za kazi mbalimbali,ambapo imekamilisha kupokea maombi tangu tarehe 14/3/2017. Kwa sasa MSD ipo katika Hatua za kukamilisha uchambuzi wa sifa za waombaji kulingana na nafasi walizoomba. Waombaji wote watakaokidhi vigezo wataitwa kwa ajili ya usaili na hata wale ambao hawataitwa kwa ajili ya usaili watajulishwa kwa utaratibu ambao Ofisi itauweka. Kumezuka matapeli wanaowapigia wananchi simu za kuitwa kwenye usaili. Wananchi wote mnaombwa kupuuza simu mnazopigiwa na watu hao wanaodai kuwa ni wa Bohari ya Dawa, zikidai kuwaita kwenye usaili na kuombwa kutuma shilingi 70,000/= au fedha yoyote. Watu hao ni matapeli na hawahusiki na Ofisi ya Bohari ya Dawa (MSD). Endapo unahisi kuna mtu anakupa taarifa hizo tafadhali piga simu na omba kuongea na Ofisi ya Rasilimali Watu au tuma Barua pepe kwa anuani:
maoni.dg@msd.go.tz ,
Kwa ufafanuzi zaidi, wasiliana moja kwa moja na MSD kwa kupiga simu ya mezani namba +255 22 2860890 - 7
Imetolewa na
Etty Kusiluka
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bohari ya Dawa (MSD)
22/03/2017
“ Tumedhamiria Kuokoa Maisha Yako ”