Tangazo la Coca Cola Lisilo na Maadili

Kwatozakuku

Member
Oct 4, 2015
24
14
Tangazo hili kwangu binafsi naliona halina maadili ya kitanzania kwani linahamasisha mapenzi kwa wanafunzi mbaya zaidi wakiwa shuleni. Tangazo hili linaonekana karibia TV nyingi hapa Tanzania na wadau tunaliona bila kulichunguza kwa makini madhara take kwa watoto wetu. Naamini hili tangozo limetengezwa nje ya nchi na kuletwa nchini bila kufanyiwa uhariri was kina kuhusu madharaye. Naomba wizara husika ikiwemo time ya mawasiliano Tanzania waliangalie tangazo kama linajenga watoto wetu au linaboa kwa ajili ya masilahi ya wachache. Natumai nimeeleweka
 
Mkuu, katika matangazo yanayonikera mojawapo ni hilo. Sijui mamlaka husika waliruhusu vipi hili tangazo linalichochea vijana kutongozana wakiwa skuli. Au labda hawalioni au wanaliona lakini hawaangalii mantiki ya tangazo hilo.
 
Back
Top Bottom