Tangazo la biashara duka la mchaga

Tangazo la biashara duka la mchaga

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
1,222
Reaction score
786
Tunauza, Mikate, Kisusio, matofali, mchele, kokoto, oil chafu, nyama choma, matunda, nondo, cement, firigisi za kuchoma, majeans, kofia, maziwa fresh, mtindi, mkaa, baiskeli, dizeli, matairi, tunaziba pancha na kutengeneza baiskeli, chakula cha mifugo, pumba za mahindi, maziwa mtindi, mbao pamoja na magogo. Karibuni sana.
 
umesahau mkuu na used spare part from Japan. Pia kukodisha muziki, tarumbeta na mapambo kwenye sherehe.
 
umesahau...simu,mikate, dawa(kwa binadamu na mifugo )
 
sumu ya panya, kunguni, viroboto, mapunye na fangas
 
Jamani,tukiachana na utani,duka la namna hii nimelishuhudia kwa macho yangu pale makorola Tanga,yaani nyama ya ng'ombe,unga wa ngano,vifaa vya ujenzi,udalali wa nyumba za kupanga na viwanja n.k.
 
Iyo bora angeiita mixed Mini supermarket.
 
kinacho mata ni mkwanja tu siunajua kale kamsemo (Mungu Onesha Sasa Hela Ilipo - MOSHI)
 
Jamani,tukiachana na utani,duka la namna hii nimelishuhudia kwa macho yangu pale makorola Tanga,yaani nyama ya ng'ombe,unga wa ngano,vifaa vya ujenzi,udalali wa nyumba za kupanga na viwanja n.k.

Kaka acha hiyo Makorola, Nenda Arusha utachoka mwenyewe, sasa huwa sielewi elewi kwamba ndo formula sahihi ya kutafuta pesa au inakuwaje...maana sumu na vyakula ndani, spare parts na Pembejeo ndani...yaani ni soooooo
 
:confused2:
Umesahau ndugu,kulikuwa pia na kibao kimeandikwa "vyumba vipo"
 
Nilienda sehemu inayoitwa Mang'ula huko Morogoro. Kuna duka moja wanauza bidhaa mchanganyiko vikiwemo mbolea za chumvichumvi. Ule mzani wanaotumia kupimia sukari, unga n.k ndio pia unatumika kupimia mbolea kwa wateja wanaonunua kiasi kidogo cha mbolea.
 
hivi jamani, hapa leseni ya biashara inakuwa imeandikwa biashara gani? Sheria si zinagomba namna hii? Hii nimeona pia kwa Wakinga, yaani ukiingia duka la mkinga unamaliza mahitaji yako yote kuanzia ya sokoni, ujenzi, kilimo na common needs.
 
Back
Top Bottom