Tangazo la ATCL halina Mvuto-(Halina Ubunifu)

Tangazo la ATCL halina Mvuto-(Halina Ubunifu)

Nilikuwa naangalia itv leo nikalifananisha na la serengeti bia yaani la atcl ni bomu,yale mapicha wamekatakata wakapachika imetoka, wanatia aibu atcl
 
Jana tu apa nilikoment kuhusu hilo jambo ktk uzi wa ujio wa ndege mpya zingine,mtu mmoja kawatetea jamaa km yeye.....
 
Nyie watu mmechanganyikiwa soon mtaingia mitaani kuokota makopo
 
Wana bodi habari za jioni.

Nimebahatika kuona mara kadhaa tangazo la ATCL (Air Tanzania) mara kadhaa tangu waanze kunadi safari zao za ndani kwa ndege mpya aina ya Bombadier hasa baada ya kuanza safari za ndani.

Ukweli ni kwamba halina mvuto na halina ubunifu kabisa yaani ni baya kiasi kwamba tangazo linaweza kuwa sababu ya kukosa abiria.

Ushauri:
Kitengo cha Promotion sijui PR au Marketing ki-outsource kazi ya kutengeneza hilo tangazo au waitishe kitu kama shindano la mtu/watu/ kampuni au taasisi kwa kuandaa kitu kama audition au shindano kwa kutengeneza Tangazo na baadaye atakayetengeneza Tangazo bora linalokubalika na jopo la waamuzi apewe zawadi na awe ni balozi wa Bombadier ATCL-Tanzania

Ikumbukwe pia kupitia Tanganzo la bombadier zitangazwe icon za nchi yetu ei. Twiga, Milima Kilimanjaro etc (Jiwe moja ndege wawili)

Nafahamu wapo watanzania wengi wenye ubunifu wa kufanya hizo kazi kisasa sana hasa ukizingatia Technology ya kufanya video ipo juu sana na inawezekana.

Management ya ATCL idara ya masoko shirikisheni wadau mpate Tangazo Bora kwa biashara endelevu.

Naomba kuwasilisha
MNAPIGA KELELE KAMPUNI INAJIFIA IKATOE DILIZA NJE MAPEMAAA SANA PLS

WELIELEWEE TUKIWASAWA TUTAWAOMBA MJE
 
Diaspora wanawaweza kusaidia. Shirika kufanikiwa sio PR au marketing tu, ni package nzima. Kila mfanyakazi wa shirika ana mchango muhimu kuhakikisha shirika linafanikiwa na kuvuka malengo.
 
Diaspora wanawaweza kusaidia kwa shirika kufanikiwa sio PR au marketing, ni package nzima. Kila mfanyakazi wa shirika ana mchango muhimu kuhakikisha shirika linafanikiwa na kuvuka malengo.
Diaspora wanaweza lkn wameshirikishwaje.....hiyo ndio hoja!
 
Diaspora wanaweza lkn wameshirikishwaje.....hiyo ndio hoja!

Sina uhakika na ushirikishwaji wa diaspora katika serikali hii ila nina uhakika baada ya kusoma hapa watafikiria mara tena na kuona ni jinsi gani nguvu kazi iliyo nje ya nchi inaweza kutumika kuinua mashirika yaliyokufa na viwanda tarajiwa.
 
Sina uhakika na ushirikishwaji wa diaspora katika serikali hii ila nina uhakika baada ya kusoma hapa watafikiria mara tena na kuona ni jinsi gani nguvu kazi iliyo nje ya nchi inaweza kutumika kuinua mashirika yaliyokufa na viwanda tarajiwa.
Ukumbuke pia mazingira ya kuwekeza Tanzania si mazuri ref Kiwanda cha cement cha Dangote!!
 
Back
Top Bottom