Tangazo la ATCL halina Mvuto-(Halina Ubunifu)

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,539
12,395
Wana bodi habari za jioni.

Nimebahatika kuona mara kadhaa tangazo la ATCL (Air Tanzania) mara kadhaa tangu waanze kunadi safari zao za ndani kwa ndege mpya aina ya Bombadier hasa baada ya kuanza safari za ndani.

Ukweli ni kwamba halina mvuto na halina ubunifu kabisa yaani ni baya kiasi kwamba tangazo linaweza kuwa sababu ya kukosa abiria.

Ushauri:
Kitengo cha Promotion sijui PR au Marketing ki-outsource kazi ya kutengeneza hilo tangazo au waitishe kitu kama shindano la mtu/watu/ kampuni au taasisi kwa kuandaa kitu kama audition au shindano kwa kutengeneza Tangazo na baadaye atakayetengeneza Tangazo bora linalokubalika na jopo la waamuzi apewe zawadi na awe ni balozi wa Bombadier ATCL-Tanzania

Ikumbukwe pia kupitia Tanganzo la bombadier zitangazwe icon za nchi yetu ei. Twiga, Milima Kilimanjaro etc (Jiwe moja ndege wawili)

Nafahamu wapo watanzania wengi wenye ubunifu wa kufanya hizo kazi kisasa sana hasa ukizingatia Technology ya kufanya video ipo juu sana na inawezekana.

Management ya ATCL idara ya masoko shirikisheni wadau mpate Tangazo Bora kwa biashara endelevu.

Naomba kuwasilisha
 
lile tangazo ni bovu, kama tumenunua ndege kwa cash, tunashindwaje kuweka budget nzur kwa ajili ya advert. mlifanyie kazi hili ni muhimu sana.
 
Hawa jamaa hovyo sana, mpaka leo website yao iko kama ya mwaka juzi! yaani kwa sbb wanauhakika wa mishahara ndo wanafanya kazi kama ya baba yao! waongeze kasi ya matangazo watu waone tofauti ya ATCL mpya na ya zamani
 
Mkuu serikali haina pesa za kutengeneza matangazo ya gharama. Tumetengeneza hilo ili kubana matumizi..
Nashukuruni kwakua mmejua ni tangazo la nini..

Tanzania ya bombadia ishakua na sasa msubiri ya viwanda!!
 
Tangazo bovu kupita maelezo halafu liko kishamba shamba flani utafikiri ni tangazo la redioni na sio TV hafu huwa naona wanatangaza TBC ambako nadhani watazamaji ni wachache.
 
kama tangazo halina mvuto kwa wananchi wa kawaida, je litakuwa na mvuto kwa watalii\abiria kutoka nje ya nchi?...
 
Kumbe kuna watu wanamuda wa kuangalia TBC ? Ni ukosefu wa hela ya ving'amuzi au ni kukosa nini ?
 
Back
Top Bottom