Tangazo la ajira za muda tume huru ya uchaguzi

Naomba kuuliza juu ya Tangazo hili kama ni la kweli, maana linasambaa sana.

View attachment 2966688
Yeah ni tangazo halali kabisa we jiandae uombe kama una sifa
Kazi za walimu hizo akina Mpwayungu Village
Nakumbuka Watu waliopata ajira za namna hii kwenye ule Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 walikuwa aidha Mawakala wa Siri wa TISS na/au Mapolisi, karibia wote wale walitoka huko. Watu wengine ambao hawakuwamo huko, waliambulia patupu licha ya kwamba walijaribu bahati zao ktk kuomba kazi hizo.
Huenda mwaka huu inaweza ikajirudia tena.
 
Nakumbuka Watu waliopata ajira za namna hii kwenye ule Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 walikuwa aidha Mawakala wa Siri wa TISS na/au Mapolisi, karibia wote wale walitoka huko. Watu wengine ambao hawakuwamo huko, waliambulia patupu licha ya kwamba walijaribu bahati zao ktk kuomba kazi hizo.
Huenda mwaka huu inaweza ikajirudia tena.



Mkuu unazungumzia nafasi za kusimamia uchaguzi au hizi za kuandaa taarifa za wapiga kura? Nadhani ume-overrate sana
 
Upo sahihi lakini ukiwa katika kutafuta FURSA usije kuwa na mtazamo kuwa ili upate FURSA Fulani lazima wngine wasiombe

Hilo linakuwa tatizo la akili huitwa scarcity mind set
Acha kua myopic,huoni wasio na ajira ni wengi,kwanini wasizingatiwe?
Nyie ndo mkipata madaraka mnataka kila kazi mfanye,pasipo kufanya kitu kinaitwa mgawanyo wa majukumu.
 
Hapana mkuu , Mimi natamani Asali imfikie kila MTU .
Sasa itatufikiaje wote ilhali kwenye kazi kama hizi,unakuta mtu ana ajira ya kudumu serikalini halafu unakuta kapanga foleni kwenye ajira hata hizi za ambazo sisi jobless tunaona zinaeeza kutu-boost?
Muda mwingine tunalaumu waheshimiwa kurundikiwa vyeo,kumbe na baadhi yetu tuna hulka hizohizo tu.
 
Kitendo cha kushusha kwa watendaji wa kata,ni dhahiri wametengeneza mazingira ya RUSHWA,kama tu kipindi cha SENSA.Wanaotoa haya matangazo,wanakua kama vile hawajui utamaduni wa hapa Tanzania.Hapo Kuna barua hazitapelekwa kwa Wakurugenzi,zitaachwa makusudi kwa sababu za itikadi za vyama,wengine hazitapelekwa kwasababu ya watendaji wa kiume kukataliwa kupewa rushwa za ngono na mambo mengine mengi.
Mimi nataka niombe ila KWA jinsi nimesoma maelezo naona bila connection hupati,

Sasa sijuh niandike tu nipeleke huko kwa mtendaji duh
 
Wajinga sana watoa tangazo,na wanajua dhahiri watu wengi wapo mitaani hawana ajira,wengine ni wahitimu wa vyuo,halafu tangazo linasema NA WALE walioko kwenye ajira pia waombe... ujinga mtupu.
Ngoja watendaji waingize wake zao,mademu zao na ndugu zao.... nchi Ina viongozi wengine wajinga sana,bora zingeombwa online,mchakato ufanyikie juu Kwa juu,kuliko kuwahusisha watendaji,hata kupeleka hizo barua.
Mimi ntapeleka maombi Kwa Mkurugenzi mwenyewe,na ikiwezekana ntatoa MAONI yangu kabisa ofisini kwao kuhusu urasimu ambao nina mashaka,utafanyika kama kipindi cha SENSA.
Kwahyo inawezekana kuipeleka kwa MKURUGENZI WEWE mwenyewe bila kupita KWA mtendaji ?
 
Back
Top Bottom