Tanganyika Law Society: TAARIFA YA DHARURA juu ya Muswada wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanganyika Law Society: TAARIFA YA DHARURA juu ya Muswada wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Apr 11, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Tarehe 9 Aprili, 2011
  DAR ES SALAAM


  Uundwaji wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara na Majukumu yake


  Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (“TLS”) ni Taasisi ya Wanasheria wa Tanzania Bara iliyoanzishwa kwa Sheria ya Chama cha Wanasheria cha Tanganyika, Sura ya 307 Toleo la 2002. Kwa mujibu wa Sheria hii, Chama kina, pamoja na mambo mengine, jukumu la kuisaidia Serikali katika mashauri yanayohusu utungaji wa sheria na utekelezaji na matumizi ya sheria, na pia kulinda na kusaidia umma katika masuala yote yanayohusika na kadhia za sheria.

  Chama cha Wanasheria kinatoa taarifa hii kwa mujibu wa mamlaka mahsusi ya sheria.

  Mazingira ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011

  Tarehe 11 Machi, Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011 (kwa kifupi “Muswada”) ulitangazwa katika Gazeti la Serikali la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Toleo Namba 1 Jarida Na.2. Chama kilipata nakala ya Muswada huo Jumanne, tarehe 30 Machi, na kilisambaza hizo taarifa kwa wanachama wake siku ya Alhamisi tarehe 31 Machi ili kupata maoni yao. Siku ya Jumamosi tarehe 2 Aprili, Chama cha Wakufunzi wa Chuo cha Dar es Salaam (UDASA) waliendesha mjadala wazi kuhusu Muswada, mjadala ambao uliripotiwa kwa mapana katika vyombo vya habari. Siku ya Jumanne, tarehe 5 Aprili, Chama chetu kilialikwa kupitia Kurugenzi ya Kamati za Bunge (“Kurugenzi”) kushiriki katika mjadala juu ya Muswada ambao ulipangwa kujadiliwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge (kwa kifupi “Kamati”) tarehe 7 Aprili Dodoma, kama ilivyopangwa awali. Mnamo mwisho wa siku hiyo Chama chetu kiliulizia maendeleo kuhusu mijadala bayana, na kikahabarishwa kwamba sasa sehemu mpya tatu (3) zimetajwa kwa ajili ya mijadala bayana, yaani Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar; aidha taarifa tulizopata ni kwamba mijadala itafanyika tarehe 7 na 8 Aprili, na ikibidi tarehe 9 Aprili. Kutokana na uthibitisho huu,Chama chetu kikaahidi kushiriki kikao cha Dar es Salaam.

  Jumanne tarehe 5 Aprili Muswada uliwakilishwa Bungeni kwa Hati ya Dharura isomwe mara ya kwanza. Tarehe 7 Aprili, Rais wa Chama chetu aliipelekea Kamati - kwa maandishi - maoni na mapendekezo ya wanachama wa Chama cha TLS kuhusu Muswada. Tarehe 8 Aprili, Rais wa Chama cha TLS alitoa mapendekezo kwa mdomo.

  Baada ya kushiriki katika mijadala ya umma, Chama kilitiisha mdahalo kuhusu Muswada kwa wanachama ili kuhakikisha mawazo ya wanachama wengi iwezekanavyo yanakusanywa kuthibitisha msimamo wa wengi katika Chama.

  Hoja na Maoni

  UTANGULIZI


  Kwa kuwa Chama cha TLS kimejizatiti kwa dhati kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria nchini Tanzania, kwa kujua kwamba sheria inapozingatiwa ipasavyo, utawala wa sheria huwalinda wananchi dhidi ya matumizi ya kibabe ya mamlaka ya Serikali; kwa kuwa tunaafiki dhana kwamba sheria zote lazima zitungwe kwa shabaha ya kuenzi Utawala wa Sheria, utawala bora na nyanja ya demokrasia ambayo imejengewa misingi imara katika falsafa ya haki ya nchi yetu na ambayo inashabihiana na viwango vya kimataifa na vyenye ubora maridhawa; kwa kuwa Chama kinaamini kwa dhati kwamba hatima na mchakato mzima kuhusu marejeo na utungaji wa Katiba mpya unapaswa kupata uhalali muafaka kwa njia ya ushirikishwaji wa wananchi; na kwa kusisitiza kwamba haki haitakiwi tu ifanyike, bali pia ionekane kwamba inafanyika, Chama kinaeleza msimamo wake mintarafu ya Muswada kama ifuatavyo:

  1. Kuhusu lugha ya Muswada: Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba Muswada utangazwe katika lugha ya Kiswahili, kwa kuzingatia dhana ya haki kupatikana (jambo ambalo linamaanisha mtu wa kawaida kupata nakala na uelewa) kwa Watanzania wote (wanaoishi vijijini na mijini, wananchi wa kawaida, wenye mapato ya kati na wa matabaka ya juu), ikiwa ni sambamba na lugha inayotambulika ya toleo rasmi la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya
  Tanzania, 1977 (kwa kifupi “Katiba”);

  2. Kuhusu jina la Muswada: Chama kinashauri kwa dhati kwamba jina la Muswada lisomeke ‘Muswada wa Kutunga Katiba Mpya, 2011’ ili kuonyesha dhahiri nia ya wananchi (kwamba wanataka Katiba mpya, siyo marekebisho yake) katika mchakato mzima;

  3. Kuhusu maelezo ya awali la Muswada: Chama kinapendekeza kwamba tamko la awali lirekebishwe na lioneshe wazi madhumuni: MUSWADA wa Sheria itakayoweka mfumo wa kutunga/kuweka Katiba mpya inayokidhi vigezo vinavyokubalika kimataifa vya demokrasia na utawala bora’;

  4. Kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa rasimu ya Katiba mpya: Chama kinatoa tahadhari kwamba Katiba ya sasa haisemi lolote kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa katiba mpya; kwa mujibu wa Ibara ya 98, ni utaratibu pekee unaotajwa wa kufanya marekebisho.

  Kutokuwepo kwa vipengele vya suala hili kutafanya michakato yoyote ya kuunda Katiba mpya kuwa batili.


  Hivyo basi kama jambo la lazima, Chama kinapendekeza kwa dhati yafanywe marekebisho ya Katiba, kuwekwe vipengele vitakavyoruhusu utaratibu wa ukomo wa Katiba iliyopo na utungaji wa Katiba mpya.

  5. Kuhusu kifungu cha 5 cha Muswada - Uundwaji wa Tume: Chama kinashauri kwa dhati kwamba Tume iundwe moja kwa moja na Sheria hii. Lugha inayotumika katika Muswada inakasimu kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania mamlaka ya kuunda Tume ambapo Rais atakuwa na uhuru wa utendaji. Aidha Rais analazimika kuunda Tume hiyo baada ya tarehe 1 Juni 2011 (tarehe ambapo sheria hii itaanza kutumika), lakini hakuna kikomo kinachotajwa cha jukumu hili.

  Ili kurekebisha kasoro hizi, kifungu hiki kisomeke, “Tume ya Katiba inaundwa kwa Sheria hii.”

  6. Kuhusu kifungu cha 6 cha Muswada - Uteuzi wa wajumbe wa Tume: Chama kinatoa maoni na mapendekezo yafuatayo:

  • Uwakilishi katika Tume: Muswada unapendekeza Tume iwe na uwakilishi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa idadi sawa. Lakini kifungu hiki hakizingatii hata kidogo tofauti ya ukubwa wa idadi ya watu na kwamba Katiba ya Muungano inahusika na Zanzibar pale tu masuala ya Muungano yanapotajwa. Hivyo basi, ili kuhakikisha kuna uwiano stahikikatika Tume (yaani unaozingatia sura halisi ya mambo), idadi ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na kutoka Visiwani izingatie idadi ya watu.
  • Muundo wa Tume: Tume iwe Jopo la Wataalamu watakaoteuliwa kutoka mchanganyiko wa kada za taaluma, mashirika na jumuiya mbalimbali kwa kuzingatia jinsia, dini na ngazi za utaalamu. Aidha kif. 6(2)(e) kinampa Rais mamlaka ya kuteua kwa hiari yake wajumbe wa Tume wasiokuwa katika makundi ya watu waliotajwa katika fasili (a) hadi (d)- jambo ambalo linaweka mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka.
  7. Kuhusu Kifungu cha 8 cha Muswada - Hadidu za Rejea (kwa kifupi “hadidu”) za Tume: Kwa ajili ya uwazi na uwajibikaji, Chama kinapendekeza kwamba hadidu ziandikwe na chombo huru na ziidhinishwe na Bunge la Tanzania, badala ya Rais.
  8. Kuhusu Kifungu cha 14 cha Muswada – Gharama za Tume: Muswada unadhihirisha dhamira ya Serikali kwamba matumizi ya Tume yatalipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali. Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba kuwe na mfumo wazi, bayana na wa uwajibikaji katika kuidhinisha na kutoa taarifa za matumizi.

  9. Kuhusu Kifungu cha 16 cha Muswada – Kutoa taarifa kwa Rais: Ili pawe na mfumo wazi na bayana, Chama kinapendekeza kwamba Taarifa ya Tume iweze kupatikana kwa umma, yaani wananchi waione na waruhusiwe kutoa maoni yao juu yake, hata kama taarifa inapelekwa kwa Rais.

  10. Utekelezaji: Ili kuhakikisha kwamba Watanzania hawaachwi nje ya mchakato huu, Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba shughuli ya Tume – kwa mtizamo wa kawaida – zifanyike mikoa yote 26 ya Tanzania, na siyo katika baadhi tu ya mikoa, kama msimamo ulivyojitokeza kwenye mijadala bayana iliyoendeshwa na Kamati ya Bunge.

  11. Kuhusu vipengele visivyoruhusiwa kuguswa – Kifungu cha 9 (2) na 20 (1):

  Muswada unafanya vipengele vya msingi vinavyohusu ibara za msingi za Katiba visiguswe. Kwa mfano, kif. 9 (2) kinataka mambo ya Muungano na suala la ofisi ya Rais, mambo yote mawili ambayo yaliyowekwa na Katiba, yasiguswe. Kif. 20 (1) kinakinzana na Ibara 26(2) ya Katiba ambayo inalinda haki ya mwananchi kupinga uhalali wa kikatiba wa sheria za nchi. Kuviacha vifungu vibaki pia ni kukiuka utekelezaji wa Utawala wa Sheria.

  12. Kuhusu kasoro za uchapishaji zimebainika, lazima ziepukwe kwa uangalifu: Usahihi wa Muswada unategemea uandishi na rejea sahihi. Kwa mfano, kif. 19 kinatakiwa kurejea kif. 18 na siyo kif.19; na kif. 20 (3) kirejee kif. 20(2) na siyo kif. 20 (1). Athari ya hili la pili, kwa mfano, ni kumtwika tuhuma ya jinai mtu yeyote anayeamua kufungua shauri mahakamani kupinga Sheria hii – jambo ambalo ni kinyume na Katiba, na ni ukiukwaji wa haki na wajibu wa msingi.

  13. Kuhusu Kifungu cha 21 cha Muswada - Kutangazwa Baraza la Kutunga Katiba: Muswada unatamka kwamba Rais ana mamlaka ya kuunda Baraza la Kutunga Katiba na kwamba anaweza kutamka Bunge lijigeuze kuwa Baraza la Kutunga Katiba.


  Chama kinapendekeza kwamba Rais asiwe na mamlaka ya kuligeuza Bunge kuwa Baraza la Kutunga Katiba, na kwamba muundo wa Baraza uamuliwe na wananchi watakaoteuliwa kutoka kada mbalimbali (yaani taaluma na uzoefu, mashirika, taasisi za kidini na makundi mbalimbali).

  14. Kuhusu Kifungu 26 cha Muswada – Kusimamia kura ya maoni (referendum): Inaonekana kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi si mahala pake kuratibu suala la uhalalishaji wa Katiba. Chama kinapendekeza kwamba taasisi za jamii, vyama vya siasa na watu binafsi na makundi mengine waruhusiwe kushiriki kwa uhuru uelimishaji wa umma kuhusu upigaji wa kura ya maoni.

  Hatimaye Tume ya Katiba idhibiti uenendeshaji wa upigaji kura ya maoni.

  15. Kuhusu sehemu ya VI – Uhalalishaji wa Katiba: Chama kinapendekeza kwamba mchakato wa uhalalishaji uendeshwe na Tume, siyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kuwa imeundwa na Katiba.

  Mpango wa Chama wa Hitimisho:

  a) Chama kinashauri kwa dhati kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aiondoe Hati ya Dharura iliyoambatanishwa na Muswada uliowasilishwa Bungeni. Kwa ushauri wa Chama Muswada ufuate utaratibu wa kawaida ili Wabunge na umma wote upate fursa ya kutosha kujadili na kutoa maoni kuhusu Muswada.


  Hali halisi, Halmashauri ya Chama cha Wanasheria kimeamua kumtembelea Mtukufu Rais ili kumfikishia yeye binafsi ujumbe huu.

  b) Chama kinaisihi Serikali isitafute kugundua upya gurudumu katika mchakato huu – kwa kadiri inavyowezekana, Serikali ijifunze kutoka uzoefu wa nchi nyingine, kama vile Kenya na Uganda.


  c) Chama chetu kiko mbioni kuunda Kamati ya Katiba, ambayo- pamoja na mambo mengine- itaishauri Halmashauri yetu juu ya maendeleo ya mchakato unaoendeshwa na Serikali, itatoa msaada wa kitaalamu na utatoa mapendekezo stahiki kwa Halmashauri yetu, umma na vyombo vinavyohusika na mchakato wa kutunga Katiba.


  Kama hapana budi, Halmashauri ya Chama itapanua majukumu ya Kamati hii ili iweze kuwa msemaji kwa niaba yake kuhusu mijadala, ambayo yaweza kuhitaji hatua zaidi.

  Imewakilishwa kwa niaba ya Chama cha Mawakili Tanzania Bara
  Francis K. Stolla
  RAIS
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kwa kweli imani kwa wanasheria wengi wakitanzania ilikuwa imepotea. kwa hili nawapongeza kwa dhati wanasheria nyie ni watu muhimu kwenye huu mchakato uzalendo mbele wapendwa
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  printable version mkuu invisible hii ni taarifa muhimu sana
   
 4. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TLS wameonyesha nia ya dhati juu ya nafasi yao kam wanataaluma katika uandikaji wa katiba mpya, wamechambua mapungufu na kutoa mapendekezo yao kwa. Nimefurahi pia kwa azimio lao la kumwona Mh. Raisi "personnaly" ili kumfikishia ujumbe wao.
   
 5. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  Invisible, nimeanzisha similar thread with attachments of the same content.

  Tafadhali muiondoe ile ya kwangu ku-avoid unnecessary multiplications.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wameonesha uzalendo.

  Lakini pia tayari wameshachakachuliwa akili...
  Vipi wao wanajiita watanzania bara, Tanzania mainland...hapa nashindwa kuwaelewa hawa wasomi wetu-
  Chama chao kinaitwa Tangayika law society...lakini wanajiita watanzania mainland....wajameni si ndio wamekubali kuchakachuliwa hawa.

  Bora wabadilishe jina kutoka Tanganyika law society to Tanzania mainland law society. It will make sense.
  :: Tanganyika Law Society Official Website ::
  Halafu hakuna mtanzania bara wala mtanzania visiwani..kuna mtanzania tu ambaye ama ni mtanganyika au mzanzibari.
  These "msomis" iko confuse us!
  They are confused or brainwashed and they want to confuse us.
   
 7. L

  Lutifya JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 261
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Angalau sasa wanasheria wetu wameanza kuamka baada ya muda mrefu kushiriki kwenye mikataba mingi ya kifisadi kwa muda mrefu sasa. Hongereni kwa maoni yetu. Nadhani werema na kombani watosoma na kuzingatia observations zenu.
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Tulitegema wanasheria wetu wasaidie kwenye hili, kwani mwananchi wa kawaida hawezi kugundua haya yote!!! Big up TLS!!!
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhana TLS wameonyesha njia na kama Serikali ina NIA ya DHATI ya Kutunga KATIBA MPYA haya madokezo ya TLS yanatakiwa yatiliwe maanani sana..

  Hiki kipengele hapa chini kinatakiwa kuchukuliwa kwa taadhari kubwa zaidi:-
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  • Jamani huu(kwenye RED) ndio mwisho wa fikra za wanasheria wetu as far as Zanzibar concerned?
   
 11. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii imetulia.

  Wanasheria muwe hivyo kwa utengamano wa nchi yenu!! Msikubali kutumiwa na wanasiasa, hususan serikali ya CCM kwa masilahi ya wachache.

  Thanks invisible.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Angalau TLS wamepata muda kuliongelea hili kama wanataaluma.

  Kwa muda mrefu kabisa wamekuwa kwa makusudi mazima kimya kabisa juu ya miswada mbalimbali mibovu inayowakilishwa bungeni na serikali yetu. Nilishawaweka kundi moja na waganga wa kienyeji ambao kazi yao kubwa ni kukusanya fedha toka kwa wateja wao kwa njia za kitapeli. Wasiishie hapo tu.

  Tunawatarajia 2015 waende kwa wingi Bungeni kwenyewe. Wanasheria wa Kenya wameweza sana. KATIBA ya Kenya sasa hivi ni moja ya katiba nzuri hapa Afrika.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Walau hiiii nchi sasa kuna watu wanafikiri nilidhani wanasheria woote wamekuwa kama WAREMA!
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  thank u Mr/Miss Invisible
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu ulitaka iweje wewe kwa mawazo yako kwangu mimi naona ni sawa! Unless kuwa na serikali ya tanganyika pia!
   
 16. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  What...?
   
 17. t

  tandala Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikutaka kucheka
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Unajua hata kama wewe ni tajiri huwezi kuamka na kuamua kumuoza mwanao just because una pesa....lazima watu wakae vikao hata kama hawakuchangii pesa watakuchangia mawazo......huu muswada na serikali yetu ni sawa na huyu tajiri wangu
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  TLS ni Tanganyika Law Society.........
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,576
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  MHhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...