Sisi Tanzania tuna tatizo moja kubwa, hakuna elimu yoyote kuielimisha jamii kuhusu huu muungano wetu adhimu na adimu, hivyo wengi hawaujui huu muungano wetu zaidi ya kujua kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuunda nchi moja ya Tanzania. Hivyo naomba nikupige darasa la muungano.
- Kuna aina 3 za miungano duniani, union, federation na confederation
- Union na muungano wa nchi mbili zaidi kuunda nchi moja.
- Federation ni muungano wa nchi mbili au zaidi kuungana kuunda taifa moja, lakini zile nchi zina utawala wake wa ndani.
- Confederation ni nchi kuungano kuunda nchi moja huko kila nchi ikijitegemea kwa mambo yake ya ndani.
- Muungano wetu ni muungano very unique, kimataifa ni muungano wa union, zile nchi zote zinakufa, inabaki nchi moja mpya, Tanganyika ilikufa na Zanzibar ilikufa, ikazaliwa Tanzania. Hivyo kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja, rais mmoja, uraia mmoja wa JMT.
- Kitaifa muungano wetu ni wa federation ya nchi moja yenye, kasehemu kanakojitegemea (Zanzibar) yenye serikali mbili, serikali ya JMT ambayo ndio serikali ya nchi, na SMZ, ambayo ni serikali ya kale kajisehemu kanakojitegemea mambo yake ya ndani, hivyo sehemu yenye mambo yake ya ndani ni Zanzibar tuu, Tanzania haina mambo yake ya ndani ni mambo ya kitaifa.
- Tuna marais wawili, rais wa nchi JMT, na rais wa kale kajisehemu.
- Tuna urais mmoja wa Tanzania, ila wale wa kale kasehemu pia wana utambulisho wa ziada wa ukaazi. Wanzanzibari wana haki zote za Utanzania, ila Watanzania ambao sio w kale kajisehemu hawana haki ya kule kwenye kajisehemu, wenye haki hiyo ni wale wakaazi tuu wa kale kajisehemu.
- JMT ina katiba yake ya nchi nzima, ila kale kajisehemu kana kajikatiba chake cha kale kajisehemu kwa mambo yake ya ndani ya kajisehemu ambayo hayaihusu JMT.
- Katiba ya JMT haiitambui katiba ya kajisehemu, kwasababu katiba yake iko kinyume na katiba ya JMT.
P