kimbendengu
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 6,094
- 10,416
mikoa yote ya pwani habari ya mjini ndio hiyo
Kweli Bora mtoto Wako ubaki nae ndaniHii ya Tanga sijawahi Iona ni mvua nzito utadhani ghalika kuu.
Msiwaachie watoto kwenda shule
Sipati picha Magaoni na kuanzia pale Shule ya Magaoni
Hapana kakaJamani watu wa Tanga poleni sana. Hapo ndio nyumbani nilipozaliwa na kukulia.
Mapango ya Amboni (Kiomoni) hayawezi kuathirika kwa sababu mto Mkulumuzi utabeba maji yote kwenda baharini.
NGUZO wewe sio mtu wa Kiomoni kweli? Nina swahiba wangu pale.
Poleni sana Wana Tanga!Salam wakuu,
Mpaka naandika bandiko hili Muda huu, mvua kali sana bado inashuka eneo la Tanga mjini na vijana vyake. Ni mvua ambayo Kama ikiendelea kupiga namna hii non-stop basi Kesho tutegemee mengine kwenye front pages. Haijakata tangu saa9 usiku wa kuamkia leo na hapa bado inapiga.
Maafa (ambayo hayadhibitishwa na mamlaka rasmi):
1. Mtu mmoja amoteza maisha eneo la kange baada ya kusombwa na maji
2. Nyumba tatu zimebomoka
3. Barabara ya makorora imafungwa na mamlaka ya jiji kuepusha maafa. (Hii imedhibitishwa)
Waungwana sala zenu zinahitajika kwa wana Tanga. Hii mvua tunayoiomba tunaomba iwe na kiasi...
Amen.
UPDATES:
Barabara ya kuelekea kasera imefungwa na hivyo waliopo eneo Hilo ni Kama wapo kisiwani. Ninavyoandika hapa, wanamaji na polisi wamefika kuwapa pole wahanga ambao wapo upande wa pili wa barabara, (walikuwa wanatoka mjini kwenda kasera). Na wamekwama. Kwa hesabu ya haraka hawapungui watu Mia mbili. Ni janga
Wakazi wa Sahare beach wako mbioni kufutwa kwenye ramani ya tanga ikiwa mvua hii itapiga kwa masaa mengine manne mfululizo kuanzia sasa.
Maeneo korofi Kama kwanjeka na mikanjuni Kesho watahitaji usafiri mbadala kutoka makwao. Sala zenu waungwana.
Umeme umekatika.... Kwa Hali ilivyo Nadhani kuna nguzo itakuwa imeanguka. Tusubiri tamko.
...wewe omba yakusombe yakakutupe Mombasa;Chumbageni pia hali ni tete. Yani ikiendelea tena kwa masaa mawili tu nyumbani kwetu kutakumbwa na mafuriko pia.