Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,310
- Thread starter
-
- #41
wanakudanganya hao
wanakudanganya hao
Waja leo warudi leo msemo huu ni maarufu sana masikioni mwenu na moja kwa moja mtu akiusema unajua hiyo ni Tanga line, Tanga Raha, Kunani paleee, Makorora Wadeka, Chuda Raha au mapenzi yalipozaliwa. Tanga ni mji wenyesifa kemkem miongoni mwa miji ya pwani na watu wake ni wakarimu sana. Nipo safarini naelekea Tanga natamani ile ahadi ya "barabara ya baharini" iliyotolewa na Mhe Mzirai ingeibwa na watawala ili ni enjoy sea view on my way to Tanga. Naenda Tanga kusalimia wazee, na zaidi ya hapo nikipata kimwana nitachumbia maana umri unaenda. Shosti ameniambia yeye toto la Tanga. Natamani angenielekeza kwao niwaone ndugu zake maana yeye yupo "kichina zaidi" na si kihalisia kama wanawake wengi humu jamvini. Naanza kusinzia na kuishiwa na mawazo kikubwa safari sio kifo nikirudi nitawaletea zawadi.
Usijali sana hata hivyo nimepata mwenyeji mdada wa kidigo mwenye macho mazuri amenikirimu na kunisuuza moyo wangu. Hivi sasa nakunywa chai, makopa, maadazi ya hiliki, vitumbua na mbaazi za kuungwa na nazi. Si unakumbuka kuna salam nilipewa kwa shemeji yetu wa chumbageni bi Rehema?
Waendao Tanga hawaagi shossi........Tanga kuna kiduku na si mduara, Tanga kuna kibao kata na si mdundiko,....Tanga kuna samaki,pweza na upepo wa Mwambao,na siiii nyama choma au kitimoto kama arusha, ila nakufahamisha uwe mwangalifu kwani kuna mtu alikwenda tanga kwa ajili ya semina,.........hadi leo hajarejea si yeye wala kabrasha la semina.
Safari njema na wasalimiw majani mapana na mabanda ya pappa
Karibu Tanga kwetu Shossi.......🙂
Ulikuwa ndani ya Raha Leo? Wasalimie washikaji pale Ocean Breeze
Usisahau kupita na Kisosora. Safari haitakamilika kama hautapata Anjari na embe viringe! Salaaam.