Tanga kunani? Mbona viwanda vimekufa?

adamtupa92

Member
Jun 29, 2016
27
24
Tulio zaliwa miaka ya 90's hii itakuwa ni stori kwetu kusikia babu zetu na baba zetu wakituhadisia Tanga ilivyo kuwa hodari ya viwanda miaka ya nyuma, nafurahi sana kusikia habari hizo lakini furaha yangu najikuta haidumu kukumbuka ninayo ambiwa ni kama hadithi za sungura na fisi (yaani imebaki stori).

Naona ni kama mazoea sasa kwa Tanga na mimi nimepata habari za kuwasimulia wanangu na wajukuu zangu kwa kushuhudia kiwanda kama cha Afritex (CIC) na kiwanda cha kuzalisha sabuni ya unga (FOMA) navyo VINAKUFA.

Ushauri wangu kwa wahusika Tanga hatuna haja ya viwanda vipya Tanga tunahaja ya kufufuliwa viwanda takrikani 60's vilivyo kufa.
Mashaalaah tumeanza safari Dodoma na imeshafanikiwa kwa asilimia fulani.
NAOMBA WAHUSIKA TUHAMISHE FIKRA ZETU TANGA KUANZA SAFARI YETU YA TANZANIA YA VIWANDA...!!!!
 
Kusubiri WAFUFUE mtasubiri sana kasema ni zamu ya wazawa kuwekeza kwenye viwanda, watu wa Tanga shaurianeni muanze na kipi kati ya hivyo vilivyokufa,.
 
Usiwe na haraka juzi nimeonge na Bakhresa, ghafula hili la mwanafunzi wa mbeya limeingilia kati !! Tanga msiwe na Shaka !!
 
Hata tukijenga viwanda 1000 kama wananchi wenyewe hamjawa tayari kuvilinda na kuvitunza ni kazi bure vitakufa tu.

Ni wakati sasa wananchi sisi wenyewe tubadilike tuwe na utayari na uzalendo wa kulinda mali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Ni jambo la kushangaza sana kuwa viwanda vyote hivyo vimekufa wakati wananchi wenyewe hatujui vimekufaje ilihali sisi wenyewe tulikua ni sehemu ya viwanda hivyo
 
SSM inaweza kukupa jibu sahihi.Baba wa Taifa atakumbukwa daima kwa viwanda.Lakini Sera ya ubinafsishaji imeacha madhara ambayo ni pamoja na kufa kwa viwanda vilivyobinafsishwa.Ni rahisi kubadilisha Teknolojia ya kiwanda kuliko gharama ya kujenga kipya.Hivi viwanda vingekuwa bado vipo situngebadilisha teknolojia,pole sana kila mahali kulikuwa na viwanda hila sasa hivi uamebaki majengo tu yaliyo badilishwa matumizi.
 
Tulio zaliwa miaka ya 90's hii itakuwa ni stori kwetu kusikia babu zetu na baba zetu wakituhadisia Tanga ilivyo kuwa hodari ya viwanda miaka ya nyuma, nafurahi sana kusikia habari hizo lakini furaha yangu najikuta haidumu kukumbuka ninayo ambiwa ni kama hadithi za sungura na fisi (yaani imebaki stori).

Naona ni kama mazoea sasa kwa Tanga na mimi nimepata habari za kuwasimulia wanangu na wajukuu zangu kwa kushuhudia kiwanda kama cha Afritex (CIC) na kiwanda cha kuzalisha sabuni ya unga (FOMA) navyo VINAKUFA.

Ushauri wangu kwa wahusika Tanga hatuna haja ya viwanda vipya Tanga tunahaja ya kufufuliwa viwanda takrikani 60's vilivyo kufa.
Mashaalaah tumeanza safari Dodoma na imeshafanikiwa kwa asilimia fulani.
NAOMBA WAHUSIKA TUHAMISHE FIKRA ZETU TANGA KUANZA SAFARI YETU YA TANZANIA YA VIWANDA...!!!!
Swala la viwanda kufa tanga muulize Mzee mkapa ndiye anajua kila kitu kuhusu Sera yake ubinafsishaji na kuua viwanda vyote nchini......

Amejenga pia Nyumba binafsi tanga yenya thamani ya millions of dollars
 
Tukiielewa vizuri sera ya uchumi wa Viwanda Tanzania utafuta thread hii maana utajikuta wewe ni mmoja wa wadau wanaopaswa kuwa na kiwanda Tanga.

Unasema hutaki viwanda vipya ila vya zamani vifufuliwe, unajua vilijengwa na nani, historia yake mpaka vinakufa?

Taja japo kiwanda kimoja na ueleze nini kimepelekea kife/kuacha kufanya kazi au kufanya kazi kwa kusuasua.
 
Back
Top Bottom