TANESCO yatoa ufafanuzi juu ya ombi la kushusha bei ya umeme kwa EWURA

kuna faida gani ya kuwa na ewura......kwanin tanesco isijitegemee
yaani kuoimba had ibembeleze hivyo
 
ngoja nyumbu waje maana wamezoea kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano wakati mgombea wao alitusababishia matatizo makubwa kwenye mkataba wa dowans na richmond
 
Pokeeni salamu Za pongezi wana JF wote Kwa kupigana hadi sasa TANESCO wame uona ukweli kuwa service charge Ni mzigo mzito,sasa wana amini kuwa social network Zina nguvu,siku wahi kuona Chambo chochote Cha Habari wana lalamika kuhusu tatizo hili ila ndani ya JF watu wali lipigia sana Kelele Kwa hoja Za nguvu
 
1.1% ni kidogo sana,haina impact yeyote ningeshauri 10%.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO

VYA HABARI KUHUSU OMBI LA TANESCO KUSHUSHA BEI YA UMEME


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewasilisha ombi la kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) pamoja na kuondoa kabisa gharama ya maombi ya awali kwa wateja wapya (gharama za Fomu) ya Shilingi 5,000 na gharama za huduma (service charge) ya Shilingi 5,520 kwa mwezi kwa wateja wote wa majumbani.


Maombi hayo yamewasilishwa baada ya TANESCO kufanya tathmini ya kina ya kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wake wanaweza kupata ahueni ya gharama kwa kuzingatia mazingira ya sasa.


Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vimepotosha ukweli huo hivyo TANESCO inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mosi, Kwa mujibu wa sheria, TANESCO inapotaka kubadilisha bei za umeme, iwe kushusha au kupandisha ni lazima iwasilishe maombi hayo EWURA kwa kuwa ndiyo mwenye mamlaka ya kisheria ya kubadilisha bei za umeme.


Pili, TANESCO huwasilisha maombi yake pamoja na takwimu halisi zinazoshawishi mantiki ya kubadilishwa kwa bei hizo na kwa maombi yaliyowasilishwa EWURA Februari 24, 2016 ndivyo TANESCO ilivyofanya.


Tatu, Baadhi ya mambo muhimu yanayoendana na mazingira ya sasa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa gesi tofauti na ilivyokuwa hapo kabla na pia kuongezeka kwa ujazo wa maji katika mabwawa hasa Mtera.


Nne, japokuwa kiasi cha madeni kilichotajwa na vyombo vya habari sio sahihi, madeni hayo yamezingatiwa kikamilifu katika mapendekezo haya ya kushusha bei, hivyo si kweli kwamba kwa kushusha huko bei TANESCO itafilisika.


Aidha, kusema kwamba Serikali inailazimisha TANESCO kushusha bei ya umeme na kwamba kwa kufanya hivyo Shirika litafilisika sio sahihi hata kidogo kwani tathmini ya kitaalamu imefanyika na pia kwa mujibu wa sheria EWURA itafanya tathmini yake kabla ya kuidhinisha bei mpya.


Ieleweke kwamba Serikali ya awamu ya Tano imeshatoa fedha nyingi za kusaidia miradi ya umeme zikiwepo zaidi ya Shilingi Bilioni 100 zilizotolewa hivi karibuni kwa maelekezo ya Mh. Rais kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kinyerezi II unaotekelezwa na Kampuni ya SUMITOMO ya Japan.


Pia Serikali imeendelea kulipa madeni ya umeme ya taasisi zake na hadi sasa sehemu kubwa ya madeni ya taasisi za Serikali yamelipwa.


Hivyo, TANESCO inaishukuru Serikali kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kushughulikia changamoto za umeme nchini.


Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano,

TANESCO Makao Makuu.
 
Wasalamu, Ndugu zangu nimenunua umeme tanesco wa elfu kumi nikapata unit 70 jana nikaenda kununua Maxmalipo elfu kumi nikapata unit 28 Je umeme imeshuka bei? au ukienda tanesco ndio umeshuka ukinunua maxmalipo paypoint bado haujashuka kama serikali imeshusha bei unit moja ni 100 Iweje elfu kumi kwa matumizi ya nyumbani nipate unit 28? nawasilisha
 
Mkuu bei ya umeme imeshuka ila inategemea upo kwenye tarrif ipi kama upo tarrif 4 unit 75 za kwanza kila mwezi utauziwa kwa sh 100 na zikizidi hapo utauziwa kwa 350 yani kuanzia unit ya 76 na kuendelea kwa aliye ktk tarrif 1 yeye atapata unit moja kwa sh 292
 
~~~>Nimenunua wa 9,000/= nikapata Unit 70.......>>>

>>>>>>Angalia hiyo risiti ya MaxMalipo imeonyesha mchanganuo mzima.
 
Mkuu bei ya umeme imeshuka ila inategemea upo kwenye tarrif ipi kama upo tarrif 4 unit 75 za kwanza kila mwezi utauziwa kwa sh 100 na zikizidi hapo utauziwa kwa 350 yani kuanzia unit ya 76 na kuendelea kwa aliye ktk tarrif 1 yeye atapata unit moja kwa sh 292
Mkuu ikitokea kesi kama hii inamaana mwezi ujao tarehe moja nitafudishwa kwenye tarrif yangu au ndio nimeamishwa moja kwa moja? Mana namimi nadhan nilizidisha matumiz mwezi huu
 
Mkuu ikitokea kesi kama hii inamaana mwezi ujao tarehe moja nitafudishwa kwenye tarrif yangu au ndio nimeamishwa moja kwa moja? Mana namimi nadhan nilizidisha matumiz mwezi huu
Kwa kawaida system huwa inarun average ya miezi 3 so kama average yako itakidhi vigezo basi watakurudisha
 
Yaani apa sijaelewa kwamba. Mwezi ukianza ukinunua umeme wanachaji 75@100. Lakini ukatumia na mwezi ujaumaliza ukaisha watakuchaji 1@350 kama walivyosema
 
add82dbde9e3f30aef2633e637bbb78f.jpg
 
Back
Top Bottom