TANESCO yatoa ufafanuzi juu ya ombi la kushusha bei ya umeme kwa EWURA

Koleba

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
376
83
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO

VYA HABARI KUHUSU OMBI LA TANESCO KUSHUSHA BEI YA UMEME


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewasilisha ombi la kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) pamoja na kuondoa kabisa gharama ya maombi ya awali kwa wateja wapya (gharama za Fomu) ya Shilingi 5,000 na gharama za huduma (service charge) ya Shilingi 5,520 kwa mwezi kwa wateja wote wa majumbani.


Maombi hayo yamewasilishwa baada ya TANESCO kufanya tathmini ya kina ya kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wake wanaweza kupata ahueni ya gharama kwa kuzingatia mazingira ya sasa.


Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vimepotosha ukweli huo hivyo TANESCO inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mosi, Kwa mujibu wa sheria, TANESCO inapotaka kubadilisha bei za umeme, iwe kushusha au kupandisha ni lazima iwasilishe maombi hayo EWURA kwa kuwa ndiyo mwenye mamlaka ya kisheria ya kubadilisha bei za umeme.


Pili, TANESCO huwasilisha maombi yake pamoja na takwimu halisi zinazoshawishi mantiki ya kubadilishwa kwa bei hizo na kwa maombi yaliyowasilishwa EWURA Februari 24, 2016 ndivyo TANESCO ilivyofanya.


Tatu, Baadhi ya mambo muhimu yanayoendana na mazingira ya sasa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa gesi tofauti na ilivyokuwa hapo kabla na pia kuongezeka kwa ujazo wa maji katika mabwawa hasa Mtera.


Nne, japokuwa kiasi cha madeni kilichotajwa na vyombo vya habari sio sahihi, madeni hayo yamezingatiwa kikamilifu katika mapendekezo haya ya kushusha bei, hivyo si kweli kwamba kwa kushusha huko bei TANESCO itafilisika.


Aidha, kusema kwamba Serikali inailazimisha TANESCO kushusha bei ya umeme na kwamba kwa kufanya hivyo Shirika litafilisika sio sahihi hata kidogo kwani tathmini ya kitaalamu imefanyika na pia kwa mujibu wa sheria EWURA itafanya tathmini yake kabla ya kuidhinisha bei mpya.


Ieleweke kwamba Serikali ya awamu ya Tano imeshatoa fedha nyingi za kusaidia miradi ya umeme zikiwepo zaidi ya Shilingi Bilioni 100 zilizotolewa hivi karibuni kwa maelekezo ya Mh. Rais kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kinyerezi II unaotekelezwa na Kampuni ya SUMITOMO ya Japan.


Pia Serikali imeendelea kulipa madeni ya umeme ya taasisi zake na hadi sasa sehemu kubwa ya madeni ya taasisi za Serikali yamelipwa.


Hivyo, TANESCO inaishukuru Serikali kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kushughulikia changamoto za umeme nchini.


Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano,

TANESCO Makao Makuu.
 
Mhmm umeshushwa kwa asilimia 1.1, okay ni step lakini. Ila hiyo ya service charge (big up)
 
Afadhari maana gharama zilikuwa kubwa kweli mpaka friji tumezima.. Na nyinyi Ewura fanyeni haraka kulidhia ombi hilo ili Watanzania tuanze kuufaidi umeme wa majumbani.
kweli hivi tutawasha kweli vifiriji vyetu ambavo vishakuwa na kutu!!
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewasilisha ombi la kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1
Nimerudia mara mbili kusoma hizi asilimia..Kwa kweli huu ni mzaha. Asilimia moja haitaleta tofauti yoyote. Tanesco punguzeni angalau kwa asilimia 10%. hapo mnaweza kuleta afueni.
 
Kupandisha hilo halina shaka lazima muombe ila kushusha bei sioni haja ya kuanza kusubiria procedures za EWURA kuwaruhusu unless labda wawaambie kiwango mlichopendekeza kushusha ni kidogo sana, fanyeni labda 10% discount badala ya hiyo 1.1%!

Else, mmefanya vyema kuanza kufikiria kumpa unafuu mraji naye especially kuondoa service charge, hebu hili anzeni kutekeleza instantly kuanzia leo tu!

Pia watu wa TRA pia ondoe kodi ya VAT katika huduma za umeme kwa wananchi. Iweje mtu ananunua umeme wa Tshs. 5,000 eti mnamkata kodi?

Mwisho pamoja na unafuu huu tunaotarajia kuanza kupata, basi umeme nao uwe wa uhakika basi. Otherwise hakutakuwa na maana yoyote kushusha bei za huduma hii muhimu halafu upatikanaji wake unakuwa ni tatizo....mgawo, mgawo au ule wa washa na kukata ovyo!!
 
Afadhari maana gharama zilikuwa kubwa kweli mpaka friji tumezima.. Na nyinyi Ewura fanyeni haraka kulidhia ombi hilo ili Watanzania tuanze kuufaidi umeme wa majumbani.
Kama ulikuwa huwezi kuwasha friji kabla hata sasa hutaweza, yaani wameweka tuu neno kupunguza, ila umeme umepunguzwa asilimia 1.1 yaani ni kama shilingi moja kwa Unit. Labda uniambie kuhusu service charge, ila sio umeme (Google kuhusu wakiwa wanaongeza bei kama wamewahi kuongeza kwa asilimia 1.1) hii haya wangepunguza kimya kimya usingeona utofauti. Naona tuu serikali anataka sifa watu waambiane umeme umepunguzwa bei ila kiuhalisia hamna kitu (na Wabongo tusivyopenda kufuatilia figures)
 
Nasikia mkurugenzi wa EWURA amekataa,amesema atafikiria,tanesco wamejitahidi kweli kumbembeleza lakini kadai ngoja ajifikirie kwanza
 
Nimerudia mara mbili kusoma hizi asilimia..Kwa kweli huu ni mzaha. Asilimia moja haitaleta tofauti yoyote. Tanesco punguzeni angalau kwa asilimia 10%. hapo mnaweza kuleta afueni.
Lakii mkuu kwa kuondoa service charge nayo ni hatua kubwa sana aiseee....
 
Nasikia mkurugenzi wa EWURA amekataa,amesema atafikiria,tanesco wamejitahidi kweli kumbembeleza lakini kadai ngoja ajifikirie kwanza

Kwahiyo anaenda kujadiliana na mkewe siyo!
Huyo ni jipu.
 
Tanesco inaomba kushusha bei,?
Usanii mwingine bana.

Hiyo Ewura iwe Tanesco jumla
 
Back
Top Bottom