TANESCO Yatangaza Mgao Kabambe Nchi nzima!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO Yatangaza Mgao Kabambe Nchi nzima!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Jan 21, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TANESCO yatangaza mgawo kurejea

  Habari mbalimbali[​IMG]Tanesco ilitoa taarifa hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi Dar es Salaam jana na ilieleza kuwa kwa mwaka 2010, makadirio ya mahitaji ya umeme ni megawati 907 wakati uwezo wa uzalishaji ni megawati 647.

  Wabunge walielezwa kuwa mbali ya upungufu wa uzalishaji, tatizo lingine linalochangia uhaba wa umeme ni ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na kuunganishwa kwa migodi ya Buzwagi na North Mara.
  Kwa mujibu wa Tanesco, bwawa la Kidatu lenye uwezo wa kuzalisha megawati 204 kwa sasa linazalisha megawati 180 pekee wakati Kihansi lenye uwezo wa kuzalisha megawati 180 linazalisha megawati 75 tu.

  Mtera linazalisha megawati 66 badala ya 80, Hale linazalisha megawati tano badala ya 21, Nyumba ya Mungu linazalisha megawati nne badala ya nane na Ubungo inazalisha megawati 70 badala ya 120.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Fedha na Uchumi, Dk. Abdallah Kigoda, alisema pamoja na upungufu huo, Serikali imeahidi kuwa itapambana kuhakikisha kuwa mgawo hautokei.

  Alisema Kamati yake imeishauri Serikali kuwekeza katika umeme ili kujiepusha na matatizo ya mgawo ambao unaathiri ukuaji wa uchumi.

  Kamati hiyo ambayo ilichambua umuhimu wa umeme katika ukuaji wa uchumi, ilielezwa pia kuwa kukosekana kwa megawati moja ya umeme taifa linapata hasara ya dola 1.1.

  Kwa upande wa Zanzibar, Dk. Kigoda alisema Serikali imesema kuwa kila mwezi katika kipindi hiki cha mgawo, visiwa hivyo vimekuwa vikipata hasara ya dola za Kimarekani milioni 45.

  Alisema Tanesco imeazimia kuchukua hatua za dharura za kujenga mitambo ya kilovoti moja kutoka Chalinze kupitia Hale hadi Arusha na mikoa ya Mtwara hadi Arusha.

  Mradi mwingine na kiasi cha megawati zitakazozalishwa kwenye mabano ni Mnazi Bay (300), Kinyerezi (240), Mitambo ya Ubungo (100) na Mwanza (60).
   
Loading...