TANESCO yatangaza Kiama

TANESCO yatangaza Kiama

viatu virefu

Senior Member
Joined
May 25, 2015
Posts
165
Reaction score
20
Operation inaendelea vizuri na kwa Operesheni hii hatutamuonea mtu aibu, awe Kigogo awe mtu wa kawaida tutamfikia. Kila mkoa kuna vikosi vinafanya kazi.

Mikoani tuna vitengo vya kudhibiti mapato Revenue Protection Unit (RPU) vinafanya kazi kisiri siri. Hatutangazi na tuna kwenda na vyombo vya habari television, magazeti na redio. Lakini pia tunaambatana na vyombo vya usalama.

Tumetoa siku saba wateja wote ambao mita zao hazifanyi kazi yaani hazisomi au zimechezewa watoe taatifa haraka ofisi za TANESCO. Baada ya muda huo kwisha hali itakuwa mbaya. Tutafuata sheria ya Uhujumu uchumi.

Kwa kampeni hii, wateja wasio waaminifu na wanaoiba umeme tutawafikia tu.

Wasijidanganye au kujipa matumaini kuwa hii ni nguvu ya soda.
 
Mbona wafanyakazi wenu wanapiga dili kila kona. Tumelipa umeme toka May hadi sasa hivi. Wakifika site saa sita wanarudi wanasema hakuna sijui bolt, mara waya aibu tupu. Hili tangazo lao wangewatanganzia hao mafundi uchwara wao kwanza.
 
ha ha ha haaaaa.... TANESCO, mlikuwa wapi mda woteeee, watu wanaiba umeme mnashangaa.... Sasa fanyeni kazi, sio kubaki kulimbikizia watu bili na kuwawekea viwango ambavyo wateja hawastahili kulipa....!!
 
Kwa mgao huu tunapigana mwikwala..
umeme unakatika hovyo alafu wanajifanya kuchaluka..
 
Kihama ndio nini? Wewe ndio msemaji wa shirika? Kihama au nini sijaelewa hapo bado,
 
Mbona wafanyakazi wenu wanapiga dili kila kona. Tumelipa umeme toka May hadi sasa hivi. Wakifika site saa sita wanarudi wanasema hakuna sijui bolt, mara waya aibu tupu. Hili tangazo lao wangewatanganzia hao mafundi uchwara wao kwanza.

Wapi huko umelipa mwezi wa tano? Muda wa kuunganishiwa umeme huanza kuhesabika pale unapokuwa umelipia service line
 
Ukiona watu wanakukosoa basi edit fasta....kihama=kiama
 
Bora muje huku mtaani kwangu tupambane muraa maana mmeniunguzia vifaa vyangu sana katika zima-wacha yenu kira mara ....nami natangaza vita muraa
 
Nahisi zoezi hili linahamasishwa na ujio wa Dk. Hon. President inapendeza sana..

Mhe uncle Mramba, ni zoezi zuri sana na lengo ni kuongeza Pato la Tanesco wale wanaokamatwa wakalipe lakini nakuhakikishia kinachoendelea Kariakoo, Magomeni na Kinondoni ni biashara tupu

Mhe. Mwenye nyumba anapigiwa anambiwa njoo ukalipe milioni mbili Makao Makuu, else njoo utupe nusu tunakufungia na mita mpya.

Wapendwa michezo hii iko na watu wa Gongo la Mboto sana tu. Shabani, Hamad na wengineo wanajua wanachowafanyaga watu. Michael Rafael, huyu ndio kiongozi wa hizi bussiness.

Muwe makini, mnaweza kuwa na nia ya kuongeza mapato zoezi likawa linawanufaisha watu
mifukoni.

Nawambieni kuna group likiondoka asubuhi likipita nyumba kumi na tano hawakosi mil kumi mpaka tisa na hizo ni zao..

Tunaomba muwasimamie wanaofanya zoezi hili na kuhakikisha hakuna utapeli. Anakamatwa mtu analipa faini..

 
Back
Top Bottom