Mr. Mramba, Kama ni wafanyakazi wako wanahujumu shirika weye sema usiogope. Hii kata, washa mnavyopenda, inakukumba weye kweli?? Toeni basi kataarifa kidogo. Ni aibu na fedheha kwa Tanesco ltd. Shirika kongwe kuliko shirika jingine lolote lililo hai hapa Tz.
Maji ya bureeeee, nguzo ni miti tunapanda wenyewe halafu mnawaza kuthibiti wadokozi wa wats badala ya hayo makilowati yanayo potelea hewani kwa kushindwa kuyatumia.
Ni aibu, tz kukatikiwa umeme kila saa. Hakuna siku itapita salama. Tumeshindwa hata kubajeti vyakula kwa sababu vingi tunamwaga kwa kuharibika.
Badala ya woote kuhama ofisi kukimbilia mitaani kusaka mita mbovu, gawaneni kazi wengine mjifungie mahali mkifanya kautafiti muondoe hii kadhia ya washa, zima, washa, kata. Mmetumalizia vyombo majumbani.
Nasikia ati unaitwa Injinia Mramba, uliupataje huo uinjinia kama hata kaubunifu huna?