Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,478
- 34,362
Hakuna kitu kama hicho! Lakini pia jiulize kama kipo inakuwaje udaiwe bilioni 50 halafu ulipe 0(sifuri) na kisha udai 'umeme wa gharama nafuu'? Huoni pamoja na kutukana watu una ji-contradict ndugu yangu!Ukiwa mjinga ni bora unyamaze,
Kwa wasiofahamu, ngoja niweke wazi.
Tanesco haijaisamehe zanzibar isipokuwa ni mkataba baina ya nyerere na Karume waliokubaliana kuhusu nishati ya umeme.
Ikumbukwe kuwa zanzibar ilikuwa na vyanzo vyake vya umeme kama generator na mashine maalumu zilizopo ndani ya meli, na umeme ililetwa toka nchi za arabuni. Baada ya kuungana Nyerere akamuomba karume asitishe ule mpango na kumuahidi kuwa watapata umeme wa gharama nafuu kama ule wanaoupata znz.
Kama hamjui ulizeni sio mkurupuke.. HUU NI MKATABA NA SIO FADHIRA.
Pili, kama kuna mkataba, kwanini TANESCO(shirika la umma na serikali) waendelee kudai kitu ambacho wanajua hakina malipo.
Tatu, lini alisimama kiongozi wa SMZ na kusema huu ni mkataba, maana waziri amekiri kuwa wamesamehewa. Hivi kuna mtu anaweza kusamehewa mkataba. Unataka kutuambia wewe unaufahamu zaidi ya waziri na serikali yako! please acha kutueleza hadithi za kwenye vigenge vya kahawa.
Ndiyo maana nasema kila siku, mvuvi akikosa samaki atasema Nyerere huyo!
Mzbar akikabwa na nyama, Nyerere huyo! akipata constipation, Nyerere huyo!
Hebu tufafanulie maswali hayo ili nasi tujue mkataba wa umeme! phew!