TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/-

TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/-

Nimeamini Tanzania hii hawa viongozi wa CCM hakuna mwenye mapenzi na sisi wananchi wa hali ya chini hivi unafuta deni kwa Wazanzibar halafu unapandisha bei kwetu sisi Bara! sasa naona mwisho wenu umekaribia. kwanza nafikiri Ngereja hajui watanzania wanatozwa Tsh. ngapi kwa unity wao wamezoea kukaa bure kila kitu bure matumizi yao makubwa ni kwenye starehe tu.
 
Then nani anaepaswa kuchukua hilo deni ina maana mbara mimi, wewe na yule............. nadhani imefika wakati kuwashitaki hawa watu mahakamani kwani sioni mantiki wengine watumie sisi tulipe. Lawyers hii ni kesi ya kuanza mara moja tafadhali
 
Hii nchi ina ombwe la uongozi, haiwezekani TANESCO inasema hiko hoi ki fedha alafu, inasamehe madeni yake... Okay, ngoja twende tutaona kitakachotokea mbeleni...
 
wakati shirika la umeme zanzibar (zeco) likipandisha bei ya umeme kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi kwa asilimia 40, imethibitika kwamba limefutiwa deni lake la muda mrefu kwa shirika la umeme tanzania (tanesco), linalofikia zaidi ya sh bilioni 50.

meneja mkuu wa zeco hassan ali mbarouk alithibitisha kufutwa kwa deni hilo alipokutana na waandishi wa habari jana na kusema hali hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya pande mbili za jamhuri ya muungano wa tanzania.

mbarouk alisema deni hilo lilifutwa baada ya uongozi wa shirika hilo kuwasilisha malalamiko yake ya muda mrefu na baadaye kukutana na aliyekuwa waziri wa nishati na madini, william ngeleja, na kupitia malalamiko yote na kuonekana kwamba deni hilo halina uhalali wa kuwapo.

uongozi wa zeco ulikuwa ukipinga ongezeko la bei ya umeme ambayo iliongezwa mwaka 2008.

"tunamshukuru sana waziri aliyekuwepo wakati ule (ngeleja), alikutanisha pande mbili, tanesco na zeco na kusikiliza malalamiko na alikubaliana nasi na kutaka kufutwa kwa deni hilo kabla ya kuingizwa katika kero za muungano," alisema mbarouk.

alifafanua kuwa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu na sasa zeco imekuwa ikilipa umeme inaonunua tanzania bara kwa awamu, lakini hawana deni linalotokana na malimbikizo au kubambikiziwa.

"tunalo deni la kawaida tu kutoka kwa tanesco la kununua umeme…hatuna deni linalotokana na utata wa kubambikiziwa," alieleza meneja huyo. Mapema, shirika la umeme zanzibar lilieleza kwamba lipo katika hatua ya kutekeleza miradi miwili ya kuongeza vituo vya kusambaza umeme unguja na kufadhiliwa na serikali ya japan.

mradi unaofadhiliwa na serikali ya japan ni kwa ajili ya kujenga vituo vitatu vya kusambaza umeme kikiwamo cha mpendae ambacho kitakuwa kikisambaza umeme katika ukanda wa uwanja wa ndege na chukwani ambayo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kuzidiwa nguvu.

meneja huyo wa zeco alisema bado wanaendelea na mikakati ya kutafuta wawekezaji katika miradi ya umeme mbadala kwa lengo la kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

source: Habari leo

my take: Inasamehe madeni wakati yenyewe kila siku inalia njaa na kukopa mabilioni katika mabenki

kufutiwa kwa deni kwa serikali ya zanzibar ni hongo la kudumisha muungano???!!!!!!
 
Bila shaka bodi ya Tanesco inafikiri kwa kutumia vifaa alivyovitanabahisha Mhe. Masaburi!
 
Duh hii hatari kubwa siwezi kuamini kinachofanywa na wanasiasa wetu watukufu.
 
WAKATI Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) likipandisha bei ya umeme kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi kwa asilimia 40, imethibitika kwamba limefutiwa deni lake la muda mrefu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalofikia zaidi ya Sh bilioni 50.

Meneja Mkuu wa Zeco Hassan Ali Mbarouk alithibitisha kufutwa kwa deni hilo alipokutana na waandishi wa habari jana na kusema hali hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbarouk alisema deni hilo lilifutwa baada ya uongozi wa shirika hilo kuwasilisha malalamiko yake ya muda mrefu na baadaye kukutana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na kupitia malalamiko yote na kuonekana kwamba deni hilo halina uhalali wa kuwapo.

Uongozi wa Zeco ulikuwa ukipinga ongezeko la bei ya umeme ambayo iliongezwa mwaka 2008.

"Tunamshukuru sana Waziri aliyekuwepo wakati ule (Ngeleja), alikutanisha pande mbili, Tanesco na Zeco na kusikiliza malalamiko na alikubaliana nasi na kutaka kufutwa kwa deni hilo kabla ya kuingizwa katika kero za Muungano," alisema Mbarouk.

Alifafanua kuwa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu na sasa Zeco imekuwa ikilipa umeme inaonunua Tanzania Bara kwa awamu, lakini hawana deni linalotokana na malimbikizo au kubambikiziwa.

"Tunalo deni la kawaida tu kutoka kwa Tanesco la kununua umeme…hatuna deni linalotokana na utata wa kubambikiziwa," alieleza Meneja huyo. Mapema, Shirika la Umeme Zanzibar lilieleza kwamba lipo katika hatua ya kutekeleza miradi miwili ya kuongeza vituo vya kusambaza umeme Unguja na kufadhiliwa na Serikali ya Japan.

Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Japan ni kwa ajili ya kujenga vituo vitatu vya kusambaza umeme kikiwamo cha Mpendae ambacho kitakuwa kikisambaza umeme katika ukanda wa Uwanja wa Ndege na Chukwani ambayo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kuzidiwa nguvu.

Meneja huyo wa Zeco alisema bado wanaendelea na mikakati ya kutafuta wawekezaji katika miradi ya umeme mbadala kwa lengo la kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

Source: Habari leo

My Take: Inasamehe madeni wakati yenyewe kila siku inalia njaa na kukopa mabilioni katika mabenki


Nafikiri habari hii imeandikwa kwa nia ya kuichafua Znz na Zec na waZnz kijumla.

Usahihi ni kuwa deni hilo limefutwa na sio Kusamehewa kwa sababu Tanesco walikiuka makubaliano na ZEC na hivyo kuisababishia ZEC kupata Hasara ya Bilioni 65 kutokana na Tanesco kushindwa kutimiza masharti ya kupeleka umeme Znz muda wote na kuwa umeme unakatwa katwa Znz kutokana na uchkavu wa mitambo ya Tanesco hususan ile ya Usafirishaji.

Ndio maana hata kukiwa na mgawo Tanganyika lakin Znz lazima umeme uwepo kutokana na mkataba.Kwa hiyo Tanesco inadaiwa bilioni 65 kutokana na kukiuka makubaliano.

Gazeti hilo limepotosha ukweli. Kwani Tanesco yenyewe taabani vipi isamehe deni.

waandishi hao wamechoka na kuamua kuitukanisha Znz.

Someni Znz leo imeandikwa kwa kina.

 
Sasa ni wakati muafaka wakufanya uchunguzi ili tupate kujua serikali ya magamba inanufaika na nini hapo Znz kwakuwa inafanya njia zote kuwaridhisha wazanzibar maana najua kama waznz wakiamua kung'ang'ania rais ajae atoke znz magamba watakuwa teyari kwa hilo kuna kitu wananufaika nacho hawa magamba si kawaida hata kidogo!

Mimi nafikiri wa Tanganyika msisubiri uchaguzi. Kumbukeni Tanesco ni shirika la Umma kwa maana nyengine ni shirika la wananchi wote wa Tanganyika. Mna kila haki ya kulifikisha mahakamani kama mlivyoweza kufikisha suala la kupinga Tuzo ya mrithi wa Richmond kulipwa mabilioni.

Tumieni njia hiyo hiyo kupinga msamaha huo na sharia itachukua mkondo wake. Na sio kukaa na kuanza kulalama chooni.

Acheni uzuzu zindukeni mlinde mali zenu na jasho leni lisiliwe na wajanja.

 
Hivi unawezaje kusamehe deni lisilo lako tena ukiwa wakati huna hela? Tanesco imeundwa na kupewa dhamana ya uzalishaji usambazaji na uuzaji wa umeme. Mtaji wake ni kodi zetu, mikopo yetu na kodi za wafadhili/ washiriki wa maendeleo. Hawana "mandate" ya kufanya walichofanya.
 
Huyu Ngeleja itabidi afuatwe huko huko ili ajibu hizi tuhuma za kusamehe hili deni na kama halikustahili kusamehewa achangie kulilipa, pia lifufuliwe upya
 
Safi sana Taane siko. Samehe deni halafu hangaika kutafuta mahali pa kukopa. Hongera ngeleja na wote mliohusika katika hujuma hii dhidi ya sisi walalahoi.
 
WAKATI Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) likipandisha bei ya umeme kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi kwa asilimia 40, imethibitika kwamba limefutiwa deni lake la muda mrefu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalofikia zaidi ya Sh bilioni 50.

Meneja Mkuu wa Zeco Hassan Ali Mbarouk alithibitisha kufutwa kwa deni hilo alipokutana na waandishi wa habari jana na kusema hali hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbarouk alisema deni hilo lilifutwa baada ya uongozi wa shirika hilo kuwasilisha malalamiko yake ya muda mrefu na baadaye kukutana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na kupitia malalamiko yote na kuonekana kwamba deni hilo halina uhalali wa kuwapo.

Uongozi wa Zeco ulikuwa ukipinga ongezeko la bei ya umeme ambayo iliongezwa mwaka 2008.

“Tunamshukuru sana Waziri aliyekuwepo wakati ule (Ngeleja), alikutanisha pande mbili, Tanesco na Zeco na kusikiliza malalamiko na alikubaliana nasi na kutaka kufutwa kwa deni hilo kabla ya kuingizwa katika kero za Muungano,” alisema Mbarouk.

Alifafanua kuwa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu na sasa Zeco imekuwa ikilipa umeme inaonunua Tanzania Bara kwa awamu, lakini hawana deni linalotokana na malimbikizo au kubambikiziwa.

“Tunalo deni la kawaida tu kutoka kwa Tanesco la kununua umeme…hatuna deni linalotokana na utata wa kubambikiziwa,” alieleza Meneja huyo. Mapema, Shirika la Umeme Zanzibar lilieleza kwamba lipo katika hatua ya kutekeleza miradi miwili ya kuongeza vituo vya kusambaza umeme Unguja na kufadhiliwa na Serikali ya Japan.

Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Japan ni kwa ajili ya kujenga vituo vitatu vya kusambaza umeme kikiwamo cha Mpendae ambacho kitakuwa kikisambaza umeme katika ukanda wa Uwanja wa Ndege na Chukwani ambayo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kuzidiwa nguvu.

Meneja huyo wa Zeco alisema bado wanaendelea na mikakati ya kutafuta wawekezaji katika miradi ya umeme mbadala kwa lengo la kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

Source: Habari leo

My Take: Inasamehe madeni wakati yenyewe kila siku inalia njaa na kukopa mabilioni katika mabenki

Apo kwenye red hampaoni au mnapenda kutengeneza mada yenu mpya? Sisi vilaza huku kwetu tulijadili uhalali wa deni hilo na tukalikataa hadharani bila ya kumung'unya maneno. kama mnadhani ni kwa hisani ya muungano basi poleni na uvivu wa kufikiri nyie mliomo humu jukwaani. wengine mlifanya wimbo wa taifa eti tunaibeba zenji kwa deni hili, kimkataba mzigo wa richmond hautuhusu na kesi tungeshinda hata kama jaji ungekua wewe, mimi naona uchangie jinsi gani usivotupenda tu kuliko kutafta sbb ambazo hazipo.
 
huu sasa ni ushenzi...wanafutiwa deni ili kuwalainisha wabakie kwenye muungano...Mi nawashangaa wazanzibari..wanapiga makelele kila siku hawataki muungano wanataka wawe kama nchi peke yao wakati hata umeme wa kwao wenyewe hawana...
 
Hii ni fedheha-wamewasamehe @ our expense..
sijui hawa watu wanaopewa dhamana za uongozi huwa wanafanya nini?tangu lini tukawa generous kiasi hiki?kama tanesco hawataki hizo pesa si wangechukua hata wakopeshe wanafunzi wa vyuo-huu ni up$$$zi
 
Tanzania sio maskini hadi tunasemehe madeni kwenye nchi maskini kama zanzibar.
 
Mantiki gani hii, angalau ningeelewa kama Tanesco wangekuwa wamewaongezea bei ya umeme (maana bei kwa Zanzibar bado ni chini, yaani subsidized na bara). nashangaa kwa sababu;
  • Tunawauzia kwa umeme wa chini, tumepandishiwa umeme karibu mara mbili ili Tanesco iendesheke (na haya madeni ni baadhi ya sababu ya kupandisha umeme),
  • Ni 'wrong timing' kwa sababu hili deni lingebaki hadi hapo watakapoonekana ni 'credible',
  • Hatujawapandishia bei ya umeme ili na bara wapate unafuu wa bei ya umeme
  • Tanesco haikupandisha umeme kwa Zanzibar na
  • Kama hawakulipa wanaweza bado wakaendelea kutokulipa kwa mazoea ya nyuma.
 
Nafikiri tutafute njia nyingine iliyo bora zaidi ya kuwabembeleza ndugu zetu wazanzibar kuhusu Muungano kuliko kulazimishwa kuendelea kuumia kwa kupandishiwa gharama za umeme. Kuna haja gani ya kuwasamehe deni wakati wao weneyewe wanadai hawana fedha hata za kuweza kumudu kuiendesha mitambo yao vyema kwa mwezi? Ni maamuzi mengine ninayoweza kusema si ya busara. Kama kweli 'waserikali' wangekuwa serious na ishu ya muungano wangeanza na hawa jamaa wa uamsho toka zenji wanaovunja katiba mchana kweupe kabisa
 
hovyo kabisa.
Hawa si ndo wanaimba wimbo kuwa hawana hela?
Upuuzi gani huu wanafanya?
 
Hata aliyekuwa hajui ubaya wa muungano sasa ataushitukia na kuuchukia, walichokuwa wanakitafuta naamini sasa wamekipata. USHIRIKIANO MZURI! %*-!!!/%+&/%+*****&***/

kizunguzungu kikiisha nitarudi.

Waendelee kuwa wavivu, kazi kucheza bao na kulalamika. Ipo siku tutasikia wanagawiwa fedha pale darajani kila jioni ili wakidhi mahitaji ya ukwaju na urojo.
 
Back
Top Bottom