TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yaisamehe Zanzibar deni la bilioni 50/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kazidi, May 11, 2012.

 1. k

  kazidi Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  WAKATI Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) likipandisha bei ya umeme kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi kwa asilimia 40, imethibitika kwamba limefutiwa deni lake la muda mrefu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalofikia zaidi ya Sh bilioni 50.

  Meneja Mkuu wa Zeco Hassan Ali Mbarouk alithibitisha kufutwa kwa deni hilo alipokutana na waandishi wa habari jana na kusema hali hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mbarouk alisema deni hilo lilifutwa baada ya uongozi wa shirika hilo kuwasilisha malalamiko yake ya muda mrefu na baadaye kukutana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na kupitia malalamiko yote na kuonekana kwamba deni hilo halina uhalali wa kuwapo.

  Uongozi wa Zeco ulikuwa ukipinga ongezeko la bei ya umeme ambayo iliongezwa mwaka 2008.

  “Tunamshukuru sana Waziri aliyekuwepo wakati ule (Ngeleja), alikutanisha pande mbili, Tanesco na Zeco na kusikiliza malalamiko na alikubaliana nasi na kutaka kufutwa kwa deni hilo kabla ya kuingizwa katika kero za Muungano,” alisema Mbarouk.

  Alifafanua kuwa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu na sasa Zeco imekuwa ikilipa umeme inaonunua Tanzania Bara kwa awamu, lakini hawana deni linalotokana na malimbikizo au kubambikiziwa.

  “Tunalo deni la kawaida tu kutoka kwa Tanesco la kununua umeme…hatuna deni linalotokana na utata wa kubambikiziwa,” alieleza Meneja huyo. Mapema, Shirika la Umeme Zanzibar lilieleza kwamba lipo katika hatua ya kutekeleza miradi miwili ya kuongeza vituo vya kusambaza umeme Unguja na kufadhiliwa na Serikali ya Japan.

  Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Japan ni kwa ajili ya kujenga vituo vitatu vya kusambaza umeme kikiwamo cha Mpendae ambacho kitakuwa kikisambaza umeme katika ukanda wa Uwanja wa Ndege na Chukwani ambayo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kuzidiwa nguvu.

  Meneja huyo wa Zeco alisema bado wanaendelea na mikakati ya kutafuta wawekezaji katika miradi ya umeme mbadala kwa lengo la kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

  Source: Habari leo

  My Take: Inasamehe madeni wakati yenyewe kila siku inalia njaa na kukopa mabilioni katika mabenki

   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Bora muungano uvunjike kuliko hii hasara tunayoipata
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Halafu wale jamaa wanabwabwaja kuhusu Muungano

  Nimesikitika sana na huu msamaha... wanamnyonya muuza kashata Kinondoni kwenda kumsamehe yule jamaa mwenye matusi kwa Tanganyika
   
 4. o

  osalwenye Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hili halihusiani na Muungano?...Kwa kweli Tanganyika inannyonywa..Nini MAONO yetu jamani WATANGANYIKA?
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Bado Wazanzibar wanakosa shukrani kabisa.
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hata aliyekuwa hajui ubaya wa muungano sasa ataushitukia na kuuchukia, walichokuwa wanakitafuta naamini sasa wamekipata. USHIRIKIANO MZURI! %*-!!!/%+&/%+*****&***/

  kizunguzungu kikiisha nitarudi.
   
 7. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nkiyaangalia haya manyaya makubwa ya gridi ya taifa yanayokwenda huko, ukafahamu rate wanazolipa watumiaji wa umeme, ukiwasikilza ***** wanaoongea kuhusu muungano unaweza kutapika.
   
 8. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Janjaweed!

  Punguza Munkari bana!

  Hivi husomi Alana za nyakati? You should be able to read in between the lines. Tanesco wamekuwa wakipatiwa Ruzuku kubwa sana na Serikali do you know why? Serikali ya CCM ndiyo yenye hisa 100% kwenye shirika la mgao wa Umeme. Hilonshirika ni chuma ulete ya Viongozi wa CCM.

  Nitatoa mfano mmoja just be patient. Kuna Kampuni hewa inaitwa IPTL imeweka mitambo kumi pale Tegeta ya kufua umeme, kisheria ile Kampuni ilikwishafilisiwa sasa iko chini ya Liquidator.

  Hiyo Kampuni iliingia mikataba ya kufua na kuuza umeme kwa Tanesco na ni mikataba mbovu kuliko yote hapa duniani! Wakati mikataba inafanyika aliyekuwa Waziri wa fedha ni Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu alikuwa Cleopa Msuya rais alikuwa Mwinyi.

  Serikali ya Mkapa ikaridhia huo mkataba na Kampuni ikaanza kufua umeme mwaka 2000 Kama sikukosea!, Mramba akwa analipa Ruzuku ya shillingi Biloni moja na na nusu Kila mwezi kwa miaka mitano Hadi mwaka 2005!

  Hadi Leo hii hiyo Kampuni inalipwa Dola milioni 3 za kimarekani Kila mwezi iwe imezalisha au isizalishe umeme na pia serikali inapaswa kununua Mafuta yasiyopungua thamani ya Tshs. 15bn kwa mwezi! In short Zanzibar walichosamehewa ni pea nut actually kwa mahesabu hayo Zanzibar ilipaswa wapatiwe umeme bure siibui mjadala but that is the reality.

  Kuhitimisha hizo pesa nyingi kiasi Hicho zinaifanya Tanesco inunue umeme bei kubwa kutoka kwa hayo makampuni yaliyobaki ya Ristam kwa kutumia formula ya IPTL one to one kwa hiyo as long as CCM iko madarakani Tanesco can never turn around. Juzi tu serikali imetoa guarantee tanesco wakopeshwe Biloni 400 ambazo kwa mchanganuo wake zote anazichukua Rostam na washiriki wake akiwemo Jakaya Kikwete of course.

  Sasa kumtoa Kafara William Mhando haisaidii hata akija malaika bila kubadili na kukata hiyo Mirija iliyoasisiwa na Baba Mwanaisha just wasting your time.

  Zanzibar kusamehewa 50 billion wamepumbazwa wanatakiwa wafaidi zaidi hata ikibidi wapewe bure ukiona wivu jinyomge.....Kidumu ccm na familia ya Baba Mwanaisha! Tunakuza deni la Taifa??
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  ..Wajinga ndio waliwao!!!...wana bendera yao ya Taifa, wana wimbo wao wa Taifa na si ajabu muda si mrefu wakawa na pasi zao za Taifa za kusafiria na hata pesa zao na Serikali hii ya Wadanganyika itaendelea kuangalia pembeni kama hawajui kinachoendelea!!! kisa nini!!!? WANADUMISHA MUUNGANO!!!!...TANESCO inahangaika kwa ukosefu mkubwa wa pesa ili kuboresha huduma zake nchini halafu wanasamehe deni la shilingi 50 Billioni!!!! Kweli Magamba ni Vingwendu!!!!
   
 10. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hichi kisiwa tunaking'ang'ania cha nini?

  Hivi hawajapata mwekezaji tukampa hichi kisiwa? Wameuza bara wakaacha Zanzibar wakati ni nchi moja.

  Tanesco acheni ujinga mnawasamehe wakati deni tunabebeshwa sisi huku kwenye bills zenu za kukadiria na kukimbiza mita.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Hawa TANESCO si ndio jana tumeambiwa wanahitaji 1.2 Trillion ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi? Sasa una hali mbaya unaomba huku unawasamehe wadaiwa wako madeni; mbona haiingii akilini?
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kumbukeni hii si mara ya kwanza. Zanzibar hawajalipa umeme tangu umevushwa. Mwenye ushahidi wa malipo aweke hapa.Kuna mishahara inakwenda huko kutoka kodi zilizobaki za Watanganyika baada ya mafisadi kujichukulia chao

  Wakati Mzanzibar akiwa analala umeme unawaka mzigo huo anatwishwa mkulima wa Pamba na Kahawa kama si tumbaku.
  Wakizinduka wanakaa katika viyoyozi vinavyotumia umeme huo kukashifu muungano hauwasaidiii.

  Kana kwamba hiyo haitoshi, wamefikia mahali pa kuwachoma moto wanaowalipia umeme. Ukiwa mkulima wa kahawa ukaenda kuanzisha genge la kahawa Zanzibar wewe ujue kibiriti unacho tu. Utachomwa moto na Wazanzibar.

  Jusa akachukua kipaza sauti kinachotumia umeme unaolipiwa na Mtanganyika na kupiga marufuku mtanganyika kupata ajira, heri apewe Mrwanda, Mtaliano au Mwarabu lakini si Mtanganyika. Amesahau kipaza sauti kinalipiwa na Mtanganyika

  Hawa wamejaa Kigamboni wakifanya shughuli hatusikii wakichomwa moto wala kubughudhiwa. Wamepewa mashamba hatusikii wakibughudhiwa. Ni marufku na mwiko kwako Mtanganyika kupata ardhi Zanzibar vinginevyo utageuzwa nyama choma, watakuchoma moto

  Wenye division 4 wanapata nafasi za upendeleo elimu ya juu. Wakija huku wanapewa mikopo kama mtu mwingine. Hawabaguliwi hata kidogo. Ole wako Mtanganyika uonekane Zanzibar, petrol na njiti za kibiriti halali yako.

  Wazanzibar wana hulka ya unafiki, wanakshifu muungano na hawana jema la kusema kuhus muungano. Nyuma yake wanafaidika na muungano kuliko mlipa umeme wa Moorogoro au Shinyanga.
  Hakuna kuoneana haya hawa ni kuwaambia ukweli wakati umefika.
   
 13. M

  Murrah Senior Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rushwa kwa Wazenji hawana shukrani wote ni kama Jusa, Umeme bure yote matunda ya Muungano
   
 14. M

  Makfuhi Senior Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii ndoa! Naanza kufikiria nyumba ndogo ili kuachana na hizi BP za kila kukicha
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hii ni tamu kuliko utamu!
   
 16. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usizungumze vitu hauna uhakika navyo Sheik wangu,ebu uliza hawa wabara wako huku wangapi wanafanya biashara na hawajachomwa moto na kwenye hayo makongamano ya uamsho wanaudhuria,ebu usilete fitina,chuki,tashititi na uchochezi usiokuwa na maana na inavyoonekana lile jambo la kuchoma vibanda hujui undani,so usibwabwaje kushikilia unachomwa,unachomwa,unachomwa,ukaleta chokochoko,kama jambo hujui uliza jambo,acha fitina na si wazanzibar wote hatuutaki muungano kwani wote tunafuata kikundi cha umsho watu tukomakwetu wale unaowaona ndo wanaitika hatutakiii,sisi tunataka urekebishwa SHEIK WANGU EBU ACHA JAZBA.
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sasa ni wakati muafaka wakufanya uchunguzi ili tupate kujua serikali ya magamba inanufaika na nini hapo Znz kwakuwa inafanya njia zote kuwaridhisha wazanzibar maana najua kama waznz wakiamua kung'ang'ania rais ajae atoke znz magamba watakuwa teyari kwa hilo kuna kitu wananufaika nacho hawa magamba si kawaida hata kidogo!
   
 18. p

  popobaawa Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Walichokuwa wanakidai Zanzibar kina uhalali, na wala hawajafanyiwa hisani. Walikataa kupandishiwa bei ya umeme kwa hoja ya kwamba ongezeko hill limechangiwa zaidi na uzembe, ufisadi na kutokuwajibika kulikofanywa na Tanesco na wadau wake, na si kutokana na mfumuko wa bei. Niliwahi kumsikia mwakilishi mmoja akihoji kuwa vipi madhara ya rushwa iliyoliwa na mtendaji wa Tanesco ailipe mzanzibari??? Hivyo wakataka iwekwe unit cost ya kuzalisha umeme bila ya kuingiza fidia wanazolipwa Richmond na gharama nyenginezo wanazopata Tanesco kwa kuingia mikataba mibovu

  Ikumbukwe katika mikataba kuna kipengele kinachoeleza kuwa upande mmoja hautowajibika kutokana na uzembe (negligence), uharibifu (damages) au ufisadi (corrupt practices) utakaofanywa na upande wa pili au washirika wake. Kimantiki Zanzibar wanahoji uhalali wa ongezeko la bei ya umeme kuanzia mwaka 2008 na wako tayari Tanesco walete mchanganuo wao wa gharama za matumizi ili ibainike kwa kiwango gani ongezeko limechangiwa na mfumuko wa bei na kuongezeka kwa gharama za maisha, na kwa kiasi gani limechangiwa na ubadhirifu na utendaji mbovu, ili kila upande ubebe msalaba wake mwenyewe
   
 19. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Mkuu hizo ukiwapa wanatafuna tu hawana lolote hawa TANESCO.
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,688
  Trophy Points: 280
  Tanesco....Tunayashangaza maisha yako.......
   
Loading...