TANESCO yageuziwa kibao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO yageuziwa kibao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Oct 11, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Na Abdallah Bawazir
  11th October 2009


  • Wabunge sasa kuhoji menejimenti kesho
  • Wangefuata ushauri mgao usingekuwepo
  Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kesho itaiweka 'kiti moto' menejimenti ya Shirika la Mgao wa Umeme nchini (Tanesco), ili wajieleze ni kwanini wameshindwa kutekeleza mapema ushauri uliotolewa na kamati hiyo kuhusu namna ya kumaliza tatizo la mgao wa umeme nchini na kusababisha mgao kujirudia.

  Kamati imechukuwa hatua hiyo baada ya kuona kuwa Tanesco imeshindwa kutekeleza mapema ushauri wake iliyoutoa mapema mwaka huu wa jinsi ya kushughulikia kwa haraka tatizo la umeme ili lisitokee tena nchini.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema kamati yake imeamua kuiita menejimenti ya Tanesco ili ijieleze kwanini mgao wa sasa umetokea, wakati ulikuwepo muda wa kutosha na fedha za kushughulikia tatizo hilo.

  Huku akionyesha kukerwa na mgao wa umeme uliopo sasa nchini, Shelukindo, alisema kuwa kimsingi tangu mpango wa Tanesco kutaka kununua mitambo yenye utata ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Dowans kugonga mwamba, Tanesco ilitakiwa kutafuta njia mbadala ya kushughulikia tatizo la umeme.

  Lakini inashangaza kuona hadi sasa hakuna kilichofanyika na matokeo yake nchi imeingia katika mgao mwingine wa umeme ambao ungeweza kuzuilika.

  "Ujue kuwa suala la Dowans lilishaamuliwa tangu Desemba mwaka jana na kulikuwa na fedha za kutosha kununulia mitambo mingine, tunashangaa hakuna kilichofanyika, sasa tumewaita kwenye kamati Jumatatu (kesho) ili watueleze kilichotokea hapo katikati hadi ukaja mgao mwingine wakati tulishauri na kutahadharisha mapema" alisema.

  Alisema pamoja na hatua hiyo ya kuiita menejimenti ya Tanesco ili itoe maelezo, kamati yake imekwenda hatua mbele zaidi, kwa kuteua timu ya wabunge watatu kutembelea baadhi ya mabwawa yanayozalisha nguvu za umeme nchini, ili kujiridhisha kama kuna upungufu mkubwa wa maji unaopelekea mgao wa umeme kama ilivyoelezwa na Tanesco.

  "Tumeunda kamati ya wabunge watatu wameenda Kihansi, Hale na Bwawa la Nyumba ya Mungu kujiridhisha kama kweli kuna upungufu wa maji unaopelekea kuwepo kwa mgao wa umeme.....baada ya kamati hii kumaliza kazi yake itatoa taarifa kwenye kamati yetu ili tujue la kufanya", alisema Shelukindo.

  Alipotakiwa na gazeti hili kueleza hatua ambazo zitachukuliwa na kamati yake baada kukutana na menejimenti ya Tanesco na kupokea taarifa ya kamati iliyoundwa, alisema kwa sasa hawezi kusema lolote hadi hapo watakapopata taarifa kamili.

  Alipoulizwa kuhusiana na maoni ya baadhi ya watu kuwa kamati yake ndiyo inayostahili kubeba lawama kutokana na kushupalia mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans isinunuliwe, Shelukindo, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, alisema ukweli kuhusu nani anastahili kubeba lawama utajulikana muda si mrefu baada ya kukutana na menejimenti ya Tanesco.

  "Baada ya kikao chetu na Tanesco Jumatatu (kesho) itajulikana nani anastahili kubeba lawama, ukumbuke sisi tulitoa ushauri wetu mapema sana na tukatahadharisha kabisa Tanesco ishughulikie suala hili mapema badala ya kusubiri mgao mwingine utokee", aliongeza kusema.

  Mapema mwaka huu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idrisa Rashid, alionya kuwa endapo serikali isingenunua mitambo ya Dowans, taifa lilikuwa katika hatari ya kuingia katika matatizo makubwa ya mgao wa umeme kuanzia Sepemba mwaka huu.

  Lakini baada ya pendekezo la shirika lake kutaka kununua mitambo ya Dowans kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa wabunge wa Kamati ya Madini na Nishati, hatimaye shirika hilo lilisitisha mpango huo japo kwa shingo upande.

  Hata hivyo, siku chache baadaye, Dk. Rashid, aliibuka na kuonya kuwa shirika hilo analoliongoza lisilaumiwe nchi ikiingia gizani, baada ya mipango ya kutaka kununua mitambo ya Dowans kugonga mwamba.

  ``Wananchi wa Tanzania watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakuwa imegubikwa na kiza, mahospitali hayatoi huduma, viwanda havizalishi na wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu tulishindwa kufanya maamuzi`` alikaririwa akisema Dk. Rashid wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Kauli hiyo ya Dk. Rashid, iliwashtua wananchi wengi, huku Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiieleza kuwa siyo ya kawaida na kuieleza kuwa ilikuwa na lengo la kuwatisha wananchi ili wakubaliane na ununuzi wa mitambo hiyo yenye utata ya Dowans.

  Tangu kauli hiyo ilipotolewa, wananchi wengi na wadau mbalimbali waliingiwa na hofu kuwa huenda tatizo la uhaba wa umeme nchini lisishughulikiwe haraka katika kile kinachoonekana kutaka kukomoana kati ya Tanesco na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyokuwa ikipinga mitambo hiyo kununuliwa.

  Baada ya Tanesco kusalimu amri kutonunua mitambo ya Dowans, haijajulikana ni lini na njia gani mbadala itakayotumika kuondoa tatizo la mgao wa umeme ambalo linaendelea kuathiri uchumi wa nchi na harakati za wananchi wengi kujiletea maendeleo.

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wameonyesha wazi hofu yao kama ipo dhamira ya dhati katika kushughulikia tatizo la umeme nchini na badala yake wanaona suala zima linaendeshwa zaidi kwa maslahi ya kibiashara na kisiasa.

  Wananchi hao wamesema kuwa wamechoshwa na malumbano hayo na sasa wanataka kuona inafanywa mikakati ya uhakika kushughulikia tatizo la umeme nchini kabla mambo hayajaharibika zaidi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema mwaka huu wakati akitangaza uamuzi wa Tanesco kuachana mitambo ya Dowans, Dk. Rashid, alisema hali ya ukuaji wa uchumi nchini inafanya ongezeko la mahitaji ya umeme kukua kwa kiwango cha megawati 75 kila mwaka na kwamba kwa sasa kuna nakisi ya megawati 150 na kutahadharisha kama hali hii itaendelea bila ya kuwapo uzalishaji wa ziada, nakisi itakuwa megawati 225 ifikapo Desemba mwaka huu.

  Jitihada za gazeti hili kumpata Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idrisa Rashid, ili aweze kueleza kama menejimenti yake imepata barua ya kuitwa mbele ya kamati ya bunge na mikakati ya shirika lake kutatua tatizo la umeme ilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu jana bila ya kupokelewa.

  Jitihada nyingine za kumpata Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ili aweze kueleza msimamo wa serikali katika suala hilo nazo ziligonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana hewani na alipotafutwa naibu wake, Adam Malima, naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila ya kupokelewa.

  Tanesco imekuwa katika mvutano mkubwa na Kamati ya Bunge na Nishati ambayo inapinga vikali kununuliwa kwa mitambo ya Dowans kwa kile inaichoeleza kuwa mitambo hiyo imerithiwa kinyemela kutoka kampuni yenye utata na Richmond na pia ununuzi wake utakwenda kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ambayo inakataza serikali kununua mitambo chakavu.

  Chimbuko la Dowans ni mkataba wa mradi wa ufuaji umeme wa dharura wa megawati 100 kati ya serikali, Tanesco na kampuni ya Richmond uliofikiwa mwaka 2006. Richmond baada ya kushindwa kutekeleza mradi huo iliuza mitambo hiyo kwa Dowans.

  Mkataba wa Richmond ulizua mvutano mkubwa kiasi cha kusababisha bunge kuunda kamati teule kuchunguza ikiongozwa na mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, ambapo ripoti yake ilimfanya Waziri Mkuu Edward Lowassa ajiuzulu.

  Pia mawaziri Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Dk Ibrahim Msabaha (Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki) nao walijiuzulu kwa kashfa hiyo.


  Mtazamo wangu;

  Kwanza nawaachia wadau walizame hili jambo. Hapa ndio tutakapoona uozo wa serikali ya kikwete kama kweli wao wako transparent watupe ripoti ya walichokizungumza humo kikao na sio kutupa matokeo.

  Pili Serikali inajua tatizo la Tanesco liko wapi watueleze na wao wamelishughulikiaje bungeni na sio kutwambia tu jujujuu.

  Tatu Tanesco kimtazamo wangu madeni mengi, mlimbikizano wa wafanyakazi wasio waaminifu, na misingi duni ya uendeshaji wa shirika kiufanisi (mfano hadi sasa tunatumia umeme wa maji, wakati india na china wanatumia umeme wa makaa ya mawe ambao ni rahisi) ndio inayorudisha nyuma maendeleo. But Tanesco watafanyaje mipango endelevu wakati serikali haitoi pesa na ikitoa wakubwa wanazitolea macho (wanataka chao) unategemea nini???
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wakati nasikitishwa na Taifa kuingia kwenye mgao mwingine... lakini nina furaha sana kwamba wakati wa kuheshimu taaluma na watendaji unakuja?

  Sasa Shelukindo na Siasa zake atuletee umeme... Dr. Rashid aliongea na authority kwa kuwa alikuwa ana wahandisi wakum-backup sasa Mh. Shelukindo na wabunge wake wana taasisi yoyote jamani yakujua ukuaji wa mahitaji ya umeme nchini?

  Sasa siasa zao limezaa nchi kwenda gizani... yes politician should now understands the impact and effect of their bla bla bla.
   
 3. E

  Engineer JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo kamati kazi yao ni kufukuzia posho tu. Shelukindo mwenyewe alifilisi mashirika mangapi ya umma kabla ya kuwa mbunge?

  Hiyo TANESCO iuzwe tu maana Miafrika ndivyo tulivyo, tunashindwa kuongoza mashirika yetu. Kazi ni kuiba na kujipatia posho kwa hasara za wananchi.
   
 4. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 2,640
  Likes Received: 1,355
  Trophy Points: 280
  Sorry are you for 'kubali yaishe' rule of law?
  You should know that intervention by Shelukindo &Co. did not mean nor did it replace Tanesco management, but advised the latter to act (power plant procurement) within the law confines, period!

  The cost of acting extra-legally on public procurement is not only very expensive but also disastrous!

  I shall always believe that Shelukindo & Co. were and are still right!
   
 5. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,487
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kamati ya shelukindo pia inapewa ushauri na wana taaluma husika kabla ya kuja na maamuzi.

  - Mitambo ambayo Tanesco ilishauri tuinunue ni mitambo chakavu na ilikuwa na bei kubwa kuliko mitambo mipya.

  -Dowans ni kampuni hewa kama Richmond ilivyokuwa. Ingekuwa ni kichekesho cha hali ya juu nchi kutumia kiasi kikubwa cha pesa kununua mitambo chakavu kwenye kampuni hewa. Mitambo ingeanza kuleta matatizo tungekwenda wapi kulalamika ama kutaka ushauri wa kiufundi?.
  Dowans na Richmond ni kampuni hewa hazina address wala ofisi, tumeliwa mapesa yetu na Richmond na hatuwezi kuwapata, sasa kwanini turudie makosa tuliyoyafanya?.

  - Katika sheria za manunuzi ni lazima uwe na proforma invoice zaidi ya tatu katika kulinganisha bei na terms za manunuzi. Ilipaswa tuwe na quatations/ Proforma invoice nyingi kujua supplier yupi ni bora na kwanini kuliko kulazimishwa kununua mitambo ya dowans.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,572
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ..binafsi nahitaji kujua Tanesco wamefanya juhudi gani kutafuta mitambo mipya baada ya kuzuiliwa kununua mitambo chakavu ya Dowans.

  ..kulingana na taarifa za vyombo vya habari, suala hili hata Raisi alikuja kuliunga mkono na akaagiza mitambo ya Dowans isinunuliwe.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mie nakuunga mkono hapo paragraph ya kwanza. Ama kuhusu mitambo ya Dowans na Richmond ni mitambo ya kampuni hewa hivyo basi ingelikuwa vema swala la richmond likafikiwa tamati ili tukajua ile mitambo inaelekea wapi kama Tanesco inachukua au wenyewe wanaichukua.

  Kuhusu uchakavu kuna jambo pengine wadau hatulifahamu kama Dk.Rashid anavyosema hapa pana equilbrium problem (dd and ss au demand and supply kwa urefu). Wakati tanesco inazalisha kiwango fix cha umeme demand ya umeme inakuwa at geometric progression sasa matokeo yake ile supply itashindwa kufikia kiwango. Lazima tufahamu wadau matokeo yake ni kwamba ikiwa kuna uzalishaji finyu basi inabidi kuwepo power rationing maana wahitajia umeme tupo wengi kuliko wasambazaji umeme sasa solution hapo ni either tugawane kidogo kidogo au wengi wakose kabisa ili wengine wapate. Solution nyengine ni kwamba wapitishe muswada wa kwamba umeme iwe sekta huria makampuni binafsi yaruhusiwe kuwekeza katika hiyo sekta hivyo basi iwezekane kukidhi mahitaji (which pengine ndio wanasiasa wetu wanataka hivyo Tanesco ionekane bogus walete makampuni yao ya kifisadi wachume kwa mlalahoi).

  Kiufupi mitambo ya dowans nadhani ingelikuwa ni short term solution wakati wakitafuta njia zengine za uzalishaji umeme mbadala zaidi ya kutumia maji
   
 8. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,487
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo ndilo swali ambalo kamati ya Shelukindo wanataka kuwauliza Tanesco. Na kibaya zaidi Tanesco walikuwa tayari kununua mitambo ya dowans ambayo ilikuwa na bei kubwa kuliko mitambo mipya, sasa kwanini hakununua mitambo mipya hakuna anayejua.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu jamani leo hii mmekwisha sahau ya miezi michache tu iliyopita... Ya kuwa ni mtambo huo huo Dowans/Richmond walijaribu kuwauzia Songos baada ya sisi kukataa wakapigwa chini na mkurugenzi wa Songos alisema kuwa mtambo huo haufai na ni hafifu..Na kwamba Songos hawawezi kununua mitambo chakavu, ambayo haina hata guarantee.. haya maneno bado yapo akilini mwangu iweje leo sisi hapa ma mbumbumbu kama Shekilango tuanze kumsifia Dr. Idrissa ambaye pia ni mbumbumbu hana elimu wala uzoefu wowote unaohusiana na mitambo ya umeme.
  Hivi kweli mmekwisha sahau gharama ambayo walitaka kutuuzia jamani hivi kweli ukiwa na shida unaweza nunua hata gari bovu ili mradi linakwenda kwa gharama sawa na gari jipya kwa sababu tu gari hilo lipo nchini na linaweza anza kazi mara moja...
  Hivi kweli mmesahau pia kwamba Richmond baada tu ya kuwarithisha Dowans mabwawa yetu yalijaa maji lakini bado tanesco waliendelea kwa muda fulani mgao wa umeme hadi ilipokuja bainika kwamba mabwawa yote yamejaa maji na hata baadhi ya wafanyakazi ktk mabwawa haya walisema hapakuwa na tatizo la maji ila yalikuwa yamepungua kulingana na kiwango kinachotakiwa..Hivyo tulipewa mgao pasipo sababu kabisa na Tanesco wenyewe walikaja na siasa nyingine. Je, mmesahau kuna kiongozi mmoja wa Tanesco (mkurugenzi) ambaye alipinga ununuzi wa Richmond toka mwanzo akazungumza madudu yote yaliyotokea, matokeo yake akaondolewa ktk uongozi wa Tanesco, sijui yuko wizara gani sasa hivi..
  Jamani mbona mnakuwa wasahaulifu kiasi hiki!
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kaka uongozi si kujua kila kitu bali ni kuwa na plan, hekima na uvumilivu na sio kufahamu transforma inafanya kazi vp ingelikuwa hivyo ndugu yangu tusingelikuwa na viongozi. Obama amesomea economics mbona anainasua marekani katika recession, kwani Winston Churchill ni askari mbona aliweza kutengeneza marshall plan uongozi ni tafauti na utendaji mzee
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 60,065
  Likes Received: 38,198
  Trophy Points: 280
  Naam, hili ndiyo swali je baada ya Watanzania kupinga kununuliwa kwa mitambo ya Richmond/Dowans kama alivyoshauri Idrissa Rashid, Zitto na wengineo je, Waziri wa Ulinzi na kushirikiana na management ya TANESCO walichukua hatua zipi nyingine ili kuhakikisha mitambo mipya inapatikana haraka ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa kina cha maji kama lingetokea au ilikuwa ni lazima kununua mtambo wa Richmond/Dowans tu na si mtambo mwingine wowote!?
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,202
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  hivi tanzania ina raisi na waziri mkuu? inabidi niulize hivyo kwa sababu hii, itakuwa ni sawa na uhaini wa serikali dhidi ya watu wake? hii ni serikali gani inayo shindwa kufanya vitu kwa wakati? kila wakati wanatumia njia ya vitisho na mateso ili wananchi waridhie kuibiwa. nafikiri imefika wakati kwa bunge lillo mahiri kuchukua hatua zifaazo, maana umeme wenye ni 10% ya raia wake wanaupata lakini inakuwa bado ni tatizo, badala ya kufikiria ni jinsi gani angalau 50% ya raia wake wapate wao ndio kwanza hata hao 10% inataka kuwapunguza, hivi Pinda graduate wa mwaka 1971 udsm na kikwete 1975?ni kwamba elimu ya chuo kikuu ilikuwa mbovu mbovu nanma hii? inamaana magraduate wa sikuhizi na wale wa magraduate enzi za akina mwaikambo na sitta ni bomba zaidi yenu., na hiyo bodi ya tanesco inatakiwa kuvunjwa au waziri husika aende nayo, kama idrisa kawashinda kwa nini mnashindwa hata kuchukua madaraka yake na yeye muendele kumpa mshahara wake hadi hapo maktaba wake uishe au mnaweza mpa in advance aende zake kukaa nyumbani.
  au ndio hela za uchaguzi mwaka kesho ndio zinazo sumbua? au kununua mitambo ya dowans ndio kiini cha tatizo?
  halafi mtu anaenda kuhutubia mikutano ya kimataifa anasema tanzania imeridhia kyoto agreement kuhusu climate change na millenium goal challenge kuinua uchumi wa watu wake , wakati mtu huyo huyo anashindwa kutumia nafasi hiyo kuleta umeme ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kuongeza maeneo ya vipato.
  na chuo kikuu na rafiki yangu iddi simba wapo tu wanaangalia riwaya zao zinavyo fanya kazi.
  maana sasa naona vikao vya baraza la mawaziri vimekosa votu vya kuongea au ndio hivyo watu wanafurahi kama kawaida kwenda kula vitumbua na kuonana na raisi, ikiwa mambo muhimu ya kuhusu nchi kiusalama na kiuchumi vikiachwa vinaelea kama nchi haina wenyewe?
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,279
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160

  Hii nchi ilishasimama siku nyingi (it is at halt). Viongozi wamebakia majina tu. Ndiyo maana kila mtu ni kambare anatesa na sharubu zake! Kama si hivyo kwa nini Rashid alitutishia wakakaa kimya? Au ndio mchezo wa kutujenga hofu ili watafute pesa za kampeni kwa mbinu za kuzalisha umeme wa dharura?
   
 14. T

  Tom JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yote sawa, lakini TANESCO walikua na muda wa kutosha kutuletea mbadala ya mitambo ya DOWANS ambayo wadau wengi walipinga isinunuliwe. Hivyo kua na plan, hekima na uvumilivu pekee ni sifuri kama matokea yake ni sifuri, tunataka matokeo kitu ambacho Idrissa kashindwa kukamilisha, yaani busara na hekima zake kwa hili ni sifuri.
   
 15. M

  MkuyuMkubwa Member

  #15
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu wanachanganya mambo.Nchi hainunui kampuni ya Dowans, inanunua mitambo...kipi ni feki, mitambo ya Dowans au Kampuni ya Dowans?....kampuni feki inapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria..nchi inahitaji mitambo, na kinachopaswa kununuliwa ni mitambo......
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  MkuyuMkubwa,
  Jambo la msingi kwenye hili suala ni kuwa, gharama za kununua hiyo mitambo ya Dowans ambayo tayari imeshatumika (i.e michakavu) ni kubwa kuliko gharama ya kununua mitambo mipya yenye uwezo huohuo wa kuzalisha umeme. Kwahiyo TANESCO kama walikuwa na hizo fedha za kununua mitambo ya Dowans walitakiwa kuagiza mitambo mipya mara moja baada ya kukataliwa kwa ombi lao la kununua hiyo mitambo ya Dowans. Vinginevyo tunapata wasiwasi kuwa kulikuwa na ulaji kwa baadhi ya watu kupitia hayo manunuzi.
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 11,747
  Likes Received: 3,451
  Trophy Points: 280
  EWURA ni rubber stamp!
   
Loading...