TANESCO yaamriwa kuzima umeme

TANESCO yaamriwa kuzima umeme

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,179
Reaction score
37,475
Nimefinywa sikio warasimu ndani ya serekali ya Kikwete wameliamuru shirika la umeme TANESCO kuzima mitambo yake ya kuzalisha umeme sehemu kubwa ya nchi hasa miji mkubwa ili waTanzania wengi wasipate fursa hadimu ya kumsikiliza Jaji Warioba.

Hii ni baada ya wanaCCM wahuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa wahuni Tanzania Bwana Paul Makonda kushindwa kuzima kiu ya waTanganyika na waZanzibar kutaka kusikia maoni ya msomi Jaji Warioba kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nimeongea na wadau mbali toka mikoa mingi ya Tanganyika wamenithibitishia umeme umekatika katika maeneo yao.

Naomba kuwasilisha.

====================

Update:

Nimekuwa natembelea maeneo mbalimbali katika nch yetu na ukweli nchi iko kwenye mgao mkali wa umeme, mfano mkoani Morogoro maeneo ya chuo kikuu cha Jordan umeme unarudi jioni, jijini Dar hali ni hiyo hiyo.

Mgao huu unatokana na ukata mkubwa unaolikumba shirika la Tanesco, wameshindwa kabisa kununua mafuta ya kutosha kulisha mitambo ya kukodi.

Jambo la ajabu usalama wa taifa wamekuwa wakizunguka mikoani na kuwachukua wafanyakazi wa TANESCO wale walioko kwenye manejimenti kwa kuwalisha viapo kuwa wasitoe siri za mgao, kwa upande wa kilimanajro viapo hivyo vilifanyika katika hostel inayomilikiwa na kkt iitwayo uhuru hostel, na hapa dsm maeneo ya ikulu.

Naomba wabunge mwambieni Prof. Muhongo aache unafiki na uongo uliokubuhu kwani ukweli ni kuwa nchi iko gizani, na yeye yuko busy kudanganya kuwa hakuna mgao na kutetea wezi wa escrow.
 
Shetani Ameshahukumiwa,ni Suala La Muda Tu Kufungwa.Mbinu Za Kina Makonda Duni Sana
 
Njia ya Pangani Tanga umeme umekatika wakati Prof Baregu anataka kuanza kuongea
 
Mbona tutakoma nimepita maeneo ya soko kuu Arusha watu kibao wapo na simu zao wanamsikiliza Jaji Warioba mji mzima unazizima na majenereta.
 
Back
Top Bottom