kwa nini tanesco walizima umeme nchi nzima kipindi cha mjadala?
je walitumwa na profesa muhongo ilo wananchi wasione mjadala?
au wafanyakazi wa Tanesco hawampendi muhongo.. sasa walikuwa wanamhujumu kipindi cha bunge ili aonekane hawezi kazi na ni muongo sana maana aliwahi kutuahidi umeme kukatika itakuwa historia..
kama ni matatizo ya kiufundi kwa nini yayokeee wakati wa mjadala tu na tena nchi nzima?
mojawapo ya shirika gumu sana kuliongoza nchi hii ni tanesco maana ndio roho ya nchi.. na wafanyakazi wake wana umoja sana wakiamua kukuhujumu wanakutoa..
nakumbuka miaka ya nyuma wakitishia kulipua mitambo nchi nzima kama wazungu wa net group solution wasipowasikiliza madai yao na wakasikilizwa..
na inasemekana wafanyakazi wa tanesco wanalipwa vizuri sana na benefits kibao ikiwepo kupews umeme units 700 za luku kila mwezi kwa bei ya shilingi 6000 tu.. ambayo ni kama kupewa bure..
naomba mnaojua mnisaidie majibu kwa nini umeme ulikatwa sana kipindi cha bunge?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.