TANESCO wilaya ya Muleba ni jipu

TANESCO wilaya ya Muleba ni jipu

Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Kwa huku mtandaoni huwa mnanifurahisha kwa ushapu wenu wa kujibu.
Tumasubiri vitendo kwa huyo mteja.
 
Mteja anaweza kuchagua kutoa taarifa inbox au kwa njia nyingine anayoona inafaa kwake lakini sio vema kulalamika au kutoa tuhuma bila taarifa.Jm
Shirika linatakiwa libinafsishwe au ligawanywe ili kuongeza ufanisi .
 
Hivi kwanini Muleba umeme ukatika mara kwa mara, kwa wiki nadhani unaweza katika mara 4 na ukikatika kurudi ni majaliwa, na hili tatizo lipo zaidi ya miaka 3 hivi kweli hamjawahi pata ufumbuzi.Tanesco Muleba jirekebisheni
Hawa jamaa wababaishaji sana.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Taarifa ndo kama inavyosomeka hapo juu. TANESCO Muleba walifungua nyaya za umeme kupisha ukataji miti katika eneo la kijiji KAMISHANGO wilaya muleba mkoa wa kagera. Ila tatizo linakuja baada ya zoezi la kukata miti kuisha wamegoma kuja kuunganisha zile waya kwa hiyo hii siku ya tatu hatuna umeme na wakipigiwa simu hawapokei. Sasa mnahisi shughuli zinazotegemea umeme zitaendeshwaje?
 
Nashukuru TANESCO kwa usikivu hatimaye mafundi wamefika na tatizo limetatuliwa , sahizi tuko na umeme viwanda vimerudi kazini.
 
Taarifa ndo kama inavyosomeka hapo juu. TANESCO Muleba walifungua nyaya za umeme kupisha ukataji miti katika eneo la kijiji KAMISHANGO wilaya muleba mkoa wa kagera. Ila tatizo linakuja baada ya zoezi la kukata miti kuisha wamegoma kuja kuunganisha zile waya kwa hiyo hii siku ya tatu hatuna umeme na wakipigiwa simu hawapokei. Sasa mnahisi shughuli zinazotegemea umeme zitaendeshwaje?
Tutakufikia tafadhali weka namba ya simu wafike hapo.Jm
 
Mnaomba namba za simu, huku TISS wamejaa unategemea utapatiwa namba? Unategemea kwà mantiki hiyo matatizo ya tanesco mtayatatua?
Kuna uhusiano gani kati ya TISS na namba ya simu ya mteja anayelalamika kuhusu huduma ya umeme?
 
Back
Top Bottom