Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,840
MWENDELEZO WA TAARIFA KUHUSU KUKOSEKANA KWA MTANDAO WA LUKU
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa mwendelezo wa taarifa ya tatizo la kukosekana kwa huduma ya kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Mtandao lililoanza usiku wa kuamkia Februari 28, 2015.
Kama tulivyoeleza awali, Tatizo kubwa lilikuwa ni hitilafu ya kiufundi iliyotokea kwenye mfumo wa kununua umeme wa LUKU.
Baada ya kugundua tatizo, mafundi wa Tanesco na Kampuni ya Itron kutoka Afrika Kusini ambao ndio watengenezaji wa mfumo huo, wamefanikiwa kurejesha huduma ya kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Benki.
Benki za CRDB na NMB kwa kutumia simbanking na ATM kwa sasa wanaweza kuuza umeme. Pia Maxmalipo nao wameanza kuuza kwa baadhi ya vituo.Mitandao ya simu (M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money) bado hawajaanza kuuza.
Jana tuliwashauri wateja wetu kwenda kununua umeme kwa Mawakala wetu na baadhi walifanya hivyo lakini baadae tuligundua kuwa units (tokens) walizokuwa wametumiwa zilikuwa haziingii kwenye mita zao, hivyo tukasimamisha kununua kwa kutumia mawakala mpaka tutakapo rekebisha tatizo.
Tunawaomba Wateja wote ambao wana tokens ambazo hazikuingia kwenye mita zao wawe na subira kwani tutoa maelekezo baada tu ya mfumo kurudi kwenye hali ya kawaida.
Aidha tunawapa matumaini wateja wetu kuwa tatizo tutalipatia ufumbuzi muda si mrefu na wale wote ambao walishatuma pesa zao kwa njia ya simu na hawajapa tokens, mfumo ukitengamaa watatumiwa tokens zao.
Hakuna pesa ya mteja itakayopotea. Uongozi wa Shirika unaendelea kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.