Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Tangu juzi umeme katika jimbo la ukonga umekatwa. Umeme huu ulikatwa saa moja kamili wakati taarifa ya habari ya channel ilipokuwa inaanza. Kwa harakaharaka vijana walijiridhisha kwamba TANESCO walikata umeme ili watu wasione msafara wa Lowassa kwenda kuchukua form. Lakini hadi kufikia hivi leo umeme haupo. Basi jana jioni nilipopita vijiweni, hoja ilikuwa ni kukosekana kwa umeme iwe ni sababu tosha ya kuinyima kura CCM.
Vijana walikuwa wanashawishiana na kutiana nguvu kwamba Lowassa aliingia mkataba wa Richmond ili kupunguza tatizo la umeme, kwahiyo alifanya hivyo kwa kujali matatizo ya watanzania, kwahiyo wapo tayari kumpa kura ili amalize kabisa tatizo la umeme ambalo imeonekana kwamba kwa serikali ya CCM halijapewa kipaumbele.
Nilishuhudia mahali pengine vijana wakiwaambia mama nitilie waliokuwa wamewasha mishumaa kwamba shida yote hii inatokana na kuichagua CCM, kwahiyo mateso hayo wanayoyapata yawe fundisho kwao kwamba CCM haifai. Jana maeneo yote ya Majohe na Chanika story zilikuwa ni kuinyima kura CCM ili kumaliza tatizo la umeme.
Kwa harakaharaka nawaza kwamba kukatwa kwa umeme kwa siku mbili na ukimya wa TANESCO, kutowajulisha wananchi sababu za kukatwa huko kwa umeme, kuna nia ya kuwaudhi wananchi ili wasiichague CCM/ Magufuli na pia wasimchague Slaa ambaye ni mgombea ubunge kwa jimbo la Ukonga.