Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,579
- 13,268
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kufanikiwa kupunguza makali ya upungufu wa umeme kutoka wastani wa kati ya Megawati 200 hadi 250 wiki iliyopita hadi wastani wa kati ya Megawati 100 - 150 wiki hii.
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema wameendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto ya mgao wa umeme.
Akielezea jitihada za muda mfupi zilizokamilika tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba II na umeshaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 24 Novemba 2022.
Pia amesema wamekamilisha matengenezo ya mtambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo namba III na imeshaanza kuzalisha kati ya megawati 35 na 40 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 25 Novemba 2022.